Mwanamuziki Robert Kelly (R. Kelly) afungwa kifungo cha miaka 30 jela

Mwanamuziki Robert Kelly (R. Kelly) afungwa kifungo cha miaka 30 jela

Safi sana akafie jela
Kwa wasiojua tu huyu jamaa alikutwa kwenye laptop yake images za watoto wadogo mpaka miaka miwili wakiwa uchi akiwa ame download images zaidi ya Elfu tatu

Amebaka sana ameshiriki ngono kwa underage
Hakuna ubaguzi hapo bali alitenda madhambi yote
Kuna watu washenzi sana hivi unaanzaje kuwa na mapenzi ya kuangalia uchi wa mtoto wa miaka miwili au mitatu kama sio sicko?

Jeffrey Epstein alikuwa mweupe kafa na dhambi zake na alikuwa rafiki mkubwa wa Prince Andrew na watu wamemchukia Andrew kuwa na rafiki wa hivyo
Nae alikuwa na kesi kama hii hii ya Kelly na alihukumiwa miaka 20 jela na baadae kukutwa kafa jela ya Manhattan
Hizo ni story nyepesi nyepesi. Issue yake ni kupita na underaged girls sio watoto wadogo. Na katika hati ya mashitaka hakuna sehemu ambapo kumeandikwa alikutwa na ushahidi wa kutazama ngono za watoto wadogo wa miaka miwili au picha zao.

Kasome vema ile hati ya mashitaka. Ni racketeering, sex trafficking, sexual intercourse with minors, na battling with sexual abuse.

Na hizi tuhuma zote zimeletwa kwa sura ya allegations bila hard evidence, ushahidi ni testimonies za hawa wadada wanaotajwa kuwa victims ambao wamekuwa kimya kwa miaka mingi sana na kuibuka ghafla kwapamoja.

Nyuma ya pazia kuna watu wanapambana na huyu jamaa wameamua kutumia media na hizi kesi kumshinda nguvu.
 
Mkuu Ghislaine Maxwell kahukumiwa miaka 20 kwa kusaidia unyanyasaji. Hakuna suala la rangi hapa. Tatizo ndugu zetu wengi wakipata pesa na umaarufu wanageuka miungu. Wanataka kulazimisha kila wanachotaka.
Ubaguzi una play part kwa kiasi chake. Kwamfano katika kesi ya R Kelly anapambana na ubaguzi wa kijinsia na ubaguzi wa rangi.

Kesi imesimamiwa na judge mwanamke ambaye ni feminists. Nyuma ya waandaaji wa hii documentary wanaoitwa Lifetime, kuna kundi la mafeminist ni misandry by nature.

Inastaajabisha ghafla bin vuu hawa wadada kwa miaka yote walikuwa kimya na hakuna aliekwenda kufile kesi hadi leo hii ghafla wote waibuke kwapamoja?!

Kwann kaka yake R.kelly na mdogo wake walishiriki na kumsagia kunguni ndugu yao?! Juzi hapa yule mdogo wake R. Kelly anaitwa Carey nadhani , amefanya interview na mdada m'moja anakipindi chake, kwa maneno yake anatamka kwamba anajiskia vibaya kuona ndugu yake anakwenda chini na anasema kuwa alitumia hasira na jazba wakati wa ile documentary angejua asishiriki maana inamtafuna ndani ya nafsi yake.

Kuna aliyekuwa mkewe, sababu ya visasi na kuona jamaa alimtema alikuwa ameweka kihoro moyoni na kushiriki ile documentary kumsema vibaya.
Huyu pamoja na wanawake walioshirikishwa wengi ambao walikuwa na mahusiano nae miaka ya nyuma na hawapo nae tena ndio wametumika kutoa ushuhuda kuelezea ubaya wa r.kelly sasa ndugu yangu unategemea nini hapo, kwamba X wako uliyeachana nae vibaya atakusemea mazuri, na amelipwa kushiriki hiyo documentary ya kimchongo?!

Kwann watu wengine wanaomkubali R Kelly hawakushirikishwa kuna mabinti wengi sana ambao wamekiri kuwa na mahusiano nae na kulala nae ila walipopewa script ya maswali wakaona wanasetiwa kumsagia kunguni R kelly na wakaona documentary ni ya mchongo waka kataa na walimjulisha R Kelly mapema kuwa jamaa wanatutafuta wanatushawishi kuandaa documentary kwaajiri yako na wanatuahidi kitulipa, r Kelly ndio maana alikuwa anasema kuna watu wanataka kuniharibia na kunichafua na hawatapumzika hadi watakapofanikisha.

Mfano Celine Dion alisema wazi kupitia msemaji wake kuwa hana jambo baya la kusema juu ya R.kelly sababu hamjui kwa ubaya bali kwa mazuri yake. Ila alikataa kushiriki sababu waandaji wa ile Documentary walikuwa wakilazimisha aongee uovu ambao yeye haujui na hana ushaidi nao hivyo akakataa.

Ukitazama nyuma ya pazia kuna watu ambao wanachuki na R. kelly na ndio wamejiunga kumfanyia ubaya.

Ni sawa na Miaka 20 ijayo tuje kusikia kuwa mtoto wa kajala,Paula anamshitaki Rayvan kuwa aliingia nae kimahusiano akiwa mdogo so alimbaka. Kimsingi hapa jamaa kafungwa kimchongo.

Kuna watu wengi wanafaidika kupitia r. Kelly kuwa kifungoni. We jiulize kaka zake wa damu moja wameshiriki wakati r. Kelly ana washkaji zake ambao wamegoma kushiriki. Hii wamefanya kusudi sababu wametake advantage ya ugomvi uliopo katika ya r Kelly na ndugu zake ambao wamekuwa wakitaka mgao wa mali zake kitu ambacho yeye amekuwa anakikwepa sana.

So yote kwa yote watu weusi shida yetu ni taasisi imara. Hatujui kusimamisha taasisi imara za kututetea katika uso wa dunia.

Tazama Floyd Mayweather alipouwawa waafrika walilalamika ile ya kawaida ila wazungu walipoingia barabarani kuandamana kila sehemu na mataifa mbali mbali ndipo waafrika nao wakaingia barabarani na yule askari ndio akachukuliwa hatua.

Ila R Kelly hapa anafanyiwa uhuni jamik ya mwafrika tunaishia kukoment na kumchafua ndugu yetu.

Kama ana hatia kwann kesi yake ina makando makando mengi sana. Kwani unataka nambie kwa marekani mtu kulala na binti wa miaka 17 au 16 ni jambo anafanya r Kelly tu mbona wakisema wafanye ukaguzi watu wote wataenda ndani tena sio watu weusi tu hadi wazungu. Mabinti anaolala nao wengi ni vile vimicharuko vya huko uswazi vinajipeleka ili vimdangie. Mbona kuna mabinti kibao wamemkalia mbali. Kubaka ni neno zito ati. Inabidi mtu atumie nguvu za mwili kukulala, ila kama alikushawishi ukafuata mshipi mwenyewe usiite kupakwa hapo ulishiriki. Haya ndio mambo ya binti kupewa mimba halafu anafungwa mwanaume anasemwa kabaka.


Hapa wamemshambulia jamaa hawajamshitaki
 
Inasikitisha sana. Tukiendelea kuwa na tabia ya kufananisha na wazungu katika maswala ya haki tutaendelea kuonekana mbwa.

Tufike wakati mwafrika anapofanyiwa udhalimu tuwe wakali kama mbogo maandamano ya waafrika dunia mzima popote tulipo. Hii itatuma ujumbe jumuiya ya kimataifa kuwa makini.

Kama wanaweza kuua mtu mweusi kwa sababu yoyote then itakuwa rahisi sana kutufanyia dhuluma na ukatili mwingine wowote ule
 
Ni 30 without parole au with a possibility of parole?

Coz usishangae baada ya miaka 3 akawa uraiani
Bado wakili wake amepeleka pingamizi kuhusu adhabu so haijawa confirmed kuwa atatumikia moja kwa moja au hukumu inaweza kuwa revoked.
 
When woman loves[emoji848][emoji848]

Sema nini badae watampunguzia miaka tu

Si unaona Babu Bill Cosby nae alibaka akafungwa maisha badae kakaa zake miaka miwili akaachiwa[emoji848][emoji1745]


Naogopa asijiue asee mzee wa LONGEST TONE in the world
Kabaka kasingiziwa. We mtu walikuwa wanaenda wote geto wanatumia vilevi, wakishalewa jamaa kaomba gemu kapiga demu anasubiria miaka 50+ imepita anasema jamaa alinibaka. Mtu ashakuwa bibi.... Huo ujinga ni huko ulaya tu, Afrika hakuna ujinga kama huo utawafanyia watu!
 
Ila angekua gay wala asingekua nakesi
Kabisa. Yaani wazungu anaweza tokea mwanaume mtu mzima anaruka na bwana mdogo wa kiume miaka 17. Watahoji kama kulikuwa na consent watasema hakuna kesi hapo.

Ila mwanamke wa miaka 20+ anaweza lala na mwanaume asubuhi akaamka kaenda kituo cha polisi na kusema kabakwa na kukawepo na kesi.

Kwa kifupi kuna mifumo ya kibaguzi ipo sana maeneo ya jinsia na rangi ya muhusika.
 
Ni sawa kuna watu wanasingiziwa na wengine ni kweli kabisa wanafanya huyu R Kelly hasingiziwa bana, hata Tz sheria iwe kali mtu hata akimbusu mtoto sio wake afungwe
Wewe una ushahidi gani mbona yanakutoka maneno kama ulikuwapo mitaa anayoishi?!

Usipende kuhukumu mtu kutoka moyoni kwa kutumia tuhuma za kuambiwa. Siku akibainika kuwa hana hatia hayo uliyomnenea toka rohoni yatabakia na wewe kisasa kitahamia katika uzao wako au watu wako wa karibu. Ulichomnenea binadamu mwenzako ambaye haujakuwepo eneo la tukio utakiona kinatokea kwako halafu utapata ile ladha halisi ya yale maneno ya chuki umemsemea mtu usiyemjua.

Kitu unachoweza fanya kwa mtu usiyemjua na hauna uhakika wa ubaya wake ni kumuonea huruma basi. MUNGU ndie anahukumu.

R. Kelly tunamfahamu kama mwanamziki na tunapenda kazi zake. Haya mengine tunayasikia tu na yanaweza kuwa ni uvumi.

Rejea kesi ya 1989 THE CENTRAL PARK FIVE. Nenda hapo YouTube, katazame historia ya hii kesi. Hawa vijana walibambikiwa kesi ya kubaka binti. Wakiwa wadogo tu katika umri wa teenage. Donald Trump aliwanenea vibaya sana hawa vijana wakati huo kwa kuandika Makala magazetini na kusema wazi angekuwa na uwezo angewauwa kabisa.

Miaka ya 2002,muhusika aliyefanya tukio hilo la ubakaji, ambaye ni mzungu, alikamatwa kwa makosa mengine ila nafsi ilimuuma akaamua kuwa na utu na kuamua kusema ukweli kuwa muda wote huu hawa vijana wakisakamwa kwenye vyombo vya habari ni mimi ndie niliyefanya ubakaji sio wao. 2014 walilipwa fidia ya Us Dollar 41milion.

Donald Trump kipindi anagombea uraisi ile kashifa ikamrudia kama kuwa ni mtu mwenye chuki na watu weusi zile video zilirudishwa mitandaoni na watu waliziona namna alikuwa akiongea kwa chuki. Alijitahidi kujitetea ila unajitetea vipi na video inakuonyesha unatamka maneno kwa chuki na hasira as if unawajua hawa vijana kwa undani.

So nikuelekeze tu ndugu yangu, huyu R Kelly kuna watu wanamchukia na wanamtengenezea zengwe la wazi. Usimnenee mtu maneno ya chuki based on media allegations. Yeye hajakili kufanya haya. Mbona wengine wanakili why yeye akatae. Kwann mtu alazimishwe kukubali kosa bila kujitetea .
 
Hizo ni story nyepesi nyepesi. Issue yake ni kupita na underaged girls sio watoto wadogo. Na katika hati ya mashitaka hakuna sehemu ambapo kumeandikwa alikutwa na ushahidi wa kutazama ngono za watoto wadogo wa miaka miwili au picha zao.

Kasome vema ile hati ya mashitaka. Ni racketeering, sex trafficking, sexual intercourse with minors, na battling with sexual abuse.

Na hizi tuhuma zote zimeletwa kwa sura ya allegations bila hard evidence, ushahidi ni testimonies za hawa wadada wanaotajwa kuwa victims ambao wamekuwa kimya kwa miaka mingi sana na kuibuka ghafla kwapamoja.

Nyuma ya pazia kuna watu wanapambana na huyu jamaa wameamua kutumia media na hizi kesi kumshinda nguvu.

Hilo la picha za watoto wadogo halikuwa na nguvu sana likatupiliwa mbali na judge

Na kuhusu kesi hii haijaanza leo wala jana hii ni hukumu tu imetoka
Wanawake walikuwa wa rika lote wakiwemo wakubwa

Ila yote kwa yote amepambana kujitetea sana na mwisho hukumu ndio hiyo

Kama ni mipango au la ndio imekuwa hivyo
Jeffrey Epstein nae alikutwa na haya haya
Kesi huwezi kusingiziwa tu huko kwani kuna wana sheria na watetezi wa aina zote
Mwisho wa siku kila mmoja ataamini na kukubali anavyoona
 
Nambie mtu mweupe Maarufu aliepewa hiyo kesi akafungwaaaa...???
Taja mmojawapo aliyefanya makosa kama aliyoyafanya R kelly yakathibitika alafu akaachwa.Au magereza zote zilizoko uko zimejaa watu weusi tu.mnafanya ujinga alafu mnakimbilia kuhificha kwenye kichaka cha ubaguzi wa rangi.
 
Eminem anabaka daily...kimyaa wametuliaa[emoji57][emoji57]
Ata wewe unaweza kumshtaki.mamlaka haziwezi kufanya kila kitu kama hakuna mlalamikaji.Marekani haijaanza kua na watu weusi leo.Ubaguzi wa rangi upo dunia nzima ila weusi wenzetu wamezidi kufanya uhalifu wakijinga.Matukio ya kutumia silaha,madawa ya kulevya na unyanyasaji wakijinsia mara nyingi wanafanya watu weusi baada yakupata vipesa.
 
Ishu kama za MJ tu...hawataki black atoboe
Atoboe nini wakati mafanikio yote aliyokua nayo katapatia uko uko.Wako matajiri wengi tu wenye asili ya afrika na hakuna anayeangaika nao sembuse hao wanaopata viela kwasababu ya kuimba ndo wamarekani waone ni mafanikio yakukusumbua.
 

Mwanamuziki wa Marekani, R. Kelly leo amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la Sex Trafficking
---

Mwanamuziki wa Marekani wa miondoko ya R&B Robert Kelly amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa unyanyasaji wa kingono kwa wanawake na mabinti wadogo.

R. Kelly amepatikana na hatia za kulazimisha, kushawishi na usafirishaji wa kingono wa binti aliyekuwa chini ya miaka 18.

Tuhuma za uhalifu wa kingono wa Kelly ulijulikana kwa umma baada ya vuguvugu la #MeToo kuanza mnamo 2017. Hatimaye Kelly alikamatwa na Februari 2019 kwa madai ya unyanyasaji wa kingono uliokithiri.

===
R&B star R. Kelly was sentenced to 30 years in prison on Wednesday for charges related to nearly 30 years’ worth of allegations that he physically and sexually abused women and minors.

His 2021 trial was one of the most high-profile cases to spring from the #MeToo movement. It is also one of the most prominent cases in which the victims were mostly Black women.

Prosecutors had asked for a 25-year sentence while Kelly’s defense team had argued for 14 to 17½ years.

“The public has to be protected from behaviors like this,” Judge Ann M. Donnelly said as she delivered Kelly’s sentence, according to media reports.

“These crimes were calculated and carefully planned and regularly executed for almost 25 years.”

Last year, a jury in the U.S. District Court in Brooklyn found Kelly, 55, guilty of one count of racketeering and eight violations of the Mann Act, a law created to curb sex trafficking across state lines.

Kelly’s racketeering conviction included 14 underlying acts. Witnesses, for example, testified that the ’90s hitmaker fraudulently married R&B singer Aaliyah, who was 15 and believed to be pregnant at the time, by bribing a government official to give her a fake ID that claimed she was an adult.

Kelly did this to protect himself legally while he sexually abused Aaliyah, starting when she was 12 or 13 years old, according to prosecutors. She died in a plane crash at 22 years old.

As R. Kelly's career flourished, an industry overlooked allegations of abusive behavior toward young women

He was also convicted of traveling across state lines for illegal sexual activity, coercion and enticement, and transportation of a minor.
Industry ni noma sana. Hauchomoki wakikuhitaji
 
Ndo shida ya kujitoa freemason, bado Justin Bieber nae wanamnyoosha, hela ya shetani haiendi bure, shetani hana shukrani hata umpe ukoo wako wote. Akirudi kwa shetani na kesi atafutiwa.
Sure....LABDA ukiingia unapewa masharti ikiwamo kuwa sodomize watoto na wakubwa na huku ukirekodiwa kisiri Ili ukiwageuka wapate kukupiga kisheria...bora hilo la kufungwa kuliko adhabu ya kuuawa....wazee misuti sio watu wazuri
 
Back
Top Bottom