kwa Mkapa uko sahihi lkn usisahau Mkapa hakuwa mtu wa kujipiga kifua na hivyo watu wengi hata hawajui mambo ambayo Mkapa alifanya, mfano mdogo tu shule za Kata wanamsifia lowasa (RIP) wafuasi wake at least lkn hawajui kwamba ni brain ya Mkapa kupitia Paris club ambapo tulitimiza masharti na ku-qualify kusamehewa madeni na sharti lilikuwa hela ya msamaha wa madeni iende kwenye ujenzi wa Shule ndipo shule za Kata ziliposambaa nchi nzima sasa lowasa was at the right place at the right time akasema amejenga shule za Kata lkn hawaambii fedha alitoa wapi huo ni mfano tu, na hukuwahi kumsikia Mkapa akipigaia hiyo legacy alikaa kimya tu hata mradi wa maji ya Ziwa Victoria yote kazi alipiga Mkapa lkn wengine wakasema ni wao wamefanya.
Mkapa alifanya makubwa klk raisi yoyote yule sema inahitaji uelewa pia kuliona hilo, uchumi wote unaoshamiri Tanzania ni kazi ya Mkapa kuanzia Banking industry kama NMB au CRDB leo hii anasifiwa raisi samia kwa faida ya NMB, hata TRA kama ilivyo leo hii ilikuwa reformed na Mkapa, alianzisha EPZ kule barabara ya mandela Mabibo viwanda vya nguo Arusha yote Mkapa, kampuni zinazofanya vizuri leo hii TZ kama TBL kabla ya Mkapa hakuna aliyekunywa bia ya Tanzania bila kuumwa kichwa kesho yake, kiwanda cha Sigara ni success story yote brain ya Uongozi wa Mkapa kwanza unaweza kusema miaka 10 iliyofwata baada ya Mkapa ilikuwa ni lost decade.
hivyo kwa Mtanzania wa kawaida ni ngumu kuelewa kazi ya Mkapa usisahau hata waliita ukapa kipindi chake sababu ya fiscal discipline na kufight against wizi wa fedha za uma kama leo hii ambapo wanaambiwa wale kwa urefu wa kamba.
Usisahau pia Mkapa alijenga Bunge Dodoma hivyo alihamisha mhimili wa kwanza ktk Karimjee kwenda Dodoma, waliofwata walipaswa wahamishe Mahakama na Serikali lkn miaka 10 udom tu ilijengwa hata mpaka leo haijakamilika yote bado…