Mwanangu amepoteza uwezo wakusimama na kutembea

Pia mfanye maombi
 
Tusubiri mrejesho jumatatu MRI na CT scan nadhani tunaweza pata pa kuanzia achana na mambo ya kuwaza kulogwa kuna mda
akili inabidi itumike
 
Pole sana mkuu....

Ilitokea kwa binti yangu wa miaka 10 pia.
Walicheza sana shuleni, ilikuwa ni Ijumaa, wakawa na mashindano ya kukimbia.
Amerudi jioni akalalamika miguu kuuma, tukamwambia ni huko kukimbia, lala kesho utaamka sawa...
Jumamosi akaamka na maumivu, yukamkanda maji ya moto na kumchua dawa, kadiri muda unavyoenda mtoto anazidi kulalamika, tukampeleka hospital akapewa panadol tu.... Akinywa maumivu yanapungua, yakianza yanakuja makali zaidi. Tukabadilisha hospitali, akapima vipimo vingi, akakutwa na UTI, lakini Dr akahoji kama anapata choo vizuri, mtoto Akasema hakumbuki mara ya mwisho amepata haja kubwa lini... Akapewa dawa na maji mengi.... Baada ya muda akasema apelekwe haja, akajisaidia choo kingi.... Kutoka pale akaanza kupata nafuu, akatembea kidogo kidogo, Dr akasema shida ni kutopata choo vizuri imesababisha mgandamizo kwenye mishipa ya fahamu upande wa chini wa mwili.
Nilishangaa, mtoto alikuwa wa kubeba kutoa nje na kupeleka ndani.
Tatizo la mwanao linaweza kuwa zaidi ya huko kuanguka katika kucheza mpira. Mpeleke kwa madakitari bingwa unaweza kupata suluhu ya haraka zaidi mkuu.
Naelewa unayopitia, Mungu ampe nafuu mtoto wetu.
 
Asante mku tunaendelea kumpambania..naye kama siku 6 ivi alikuwa hapati choo kikubwa lkn kwasasa anapata choo vzr
 

Pole kwake, halafu pole Sana kwako! Ninaamini Ana shida zaidi ya mpira aliocheza, nashauri aende kwa daktary specially wa mifupa.

Ikishindikana huko pambana a na maombi, na sio Hawa manabii kama Mwamposa, hapana, watu wa kueleweka.
 
Wahi Hospital AFANYIWE,. MRI, T3, TSH tena KWA unangalizi wa doctor mzoefu tena haraka Ili ujue unafanya nn? Ila ikionekana hana shida Angalia upande wa pili (KIENYEJI) haya mambo huwa yapo ila changamka uende na muda[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Pole sana kaka. Hii case ni kama ya mtt wa jirani yangu yy wa kiume anahangaika sana na mtt anapata maumivu makali. Yeye kaambiwa mtt ana sickle cel sijui nimepatia kuandika nimesahau kidogo. Japo wazazi wanakataa kwa sbb kwao hakuna wenye historia ya huo ugonjwa, juzi yameibuka mapya mwanamke anasema mama mkwe wake ni mchawi anawaua wajukuu zake wa kiume maana kuna watoto wa shemeji zake na wifi zake wameshafiwa na wtt wao kiume, ngachokaaa. Cha msingi usichoke kuomba na kwenda hospital
 
Asante mku tunaendelea kumpambania..naye kama siku 6 ivi alikuwa hapati choo kikubwa lkn kwasasa anapata choo vzr
Polee sana ndugu. Namauombea Mtoto nafuu na suluhusho la ugonjwa lipatikane.
 

Hii kitu imeniuma Sana, hemu niambie unaishi Mkoa gani?
 
Mzee wajaribu kucheki uti wa mgongo, usiende kwa mganga utaharibu kila jambo, muombe sana mungu akufanyie wepesi, kama ni mambo ya wanadamj yeye anaweza kuondoa na kama ni ugonjwa kqa amri yake, pia yeye anaweza kuondoa.. We komaa hospital na dua kqenye moyo wako.
 
Pole kwake, halafu pole Sana kwako! Ninaamini Ana shida zaidi ya mpira aliocheza, nashauri aende kwa daktary specially wa mifupa.

Ikishindikana huko pambana a na maombi, na sio Hawa manabii kama Mwamposa, hapana, watu wa kueleweka.
Hapo kwenye maombi ndiyo unataka kumpoteza. Mwambie ikishindikan hosp za Tanzania ampeleke hosp za nje ya Tanzania, hakuna daktari aliyesomea kutibu kupitia maombi.
 
Hapo kwenye maombi ndiyo unataka kumpoteza. Mwambie ikishindikan hosp za Tanzania ampeleke hosp za nje ya Tanzania, hakuna daktari aliyesomea kutibu kupitia maombi.

Nje utamlipia wewe?
 
Hao madaktari ni wazembe sana, especially uliowafata baada ya mwanao kushindwa kutembea, wajinga kama hao ndo hufanya mauaji hospital bila kujijua, nimesoma nao wengi, wengine wanafaulu ila mtu unajua kabisa huyu hafai na hana maamuzi sahihi
Anyways, ningependa kujua au ungemuuliza mwanao aliangukaje na akielezee kiufasaha kabisa bila kupindisha neno(every small detail matter), kuna possibilities nyingi za ugonjwa wake ila the most ovious sitaki kuikimbilia uku sijamuona mgonjwa kabisa,
Ukimshika mguu wake bila hizo dawa za maumivu inakuaje, na ukimbinya kidogo kwenye nyama za mapajani au kwenye kigimbi inakuaje??
Na je anaweza kuhamisha mguu wake ata kidogo kwa sasa??
Nijibu please, maana uku Jf ni kusaidiana

Ila kikubwa umeelezwa vizuri na baadhi ya watu humu, nenda muhimbili tafta daktari mzoefu na alieona mengi, uzuri matatizo ya binadam hujirudia, ukipata mzoefu yawezekana ashaona mengi ya ugonjwa huo na pia ashafanya makosa mpaka akajirekebisa
Kuna vipimo inabidi wavifanye kama MRI na kupima fluid iliyoko kwenye vertabral colum, ni maumivu ila hey, bora maumivu ya maramoja na diagnosis ikapatikana
Kibaya cha magonjwa mengi ni kuchelewa kufika hospitalini, hao madaktari wa mwanzo ilibidi wajiulize kwann mtoto anaumia na anachechemea wakati hakuna palipoumia, ilibid wajue situation iliyomkuta, ila myb myb nao wanapata wagonjwa wengi ambao matatizo yao sio serious ndo maana wakaja na hizo judgement

So please nenda muhimbili pia tafta madaktari wazoefu ata kama wamestaaf wafate kwenye hospital zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…