Mwanangu amepoteza uwezo wakusimama na kutembea

Uti wa mgongo kipimo kimeonyesha upo sawa
 
Wahi kwa Mwamposa Kawe,kama uko mbali fatilia maombi ya operation komboa familia kila siku saa tatu usiku..Mungu awavushe,poleni sana
 
Ooh poleni sana mkuu, Mungu amsaidie binti taifa la kesho apone haraka, ana umri sawa na mdogo angu nimefikiria 😪. Poleni atakua sawa🙏
 
Uti wa mgongo kipimo kimeonyesha upo sawa
Basi sawa kaka, mfikishe muhimbili kwa wataalamu zaidi, wao watakuwa na majawabu. Usiache kumlilia mola wako na wala asikudanganye mtu kwenda kwa mganga.
 
Walikua wanauliza ameangukaje nikwamba anasema amengukia makalio..
-ukimshika mguu hapat maumivu yoyote
-ukimbinya nyama zinabonyea na ukimuachia zinarud kama kawaida
-hawezi kuhamisha mguu kabisa anafanya kuinyanyua kwamikono kuisogeza
 
Pole sana Mkuu,
i wish hao madaktrai hata wange brainstorm nakukupa mwanaga angalau ushauri basi dah..!

Kama wadau walivyoelezea jitahidi sana uje huku Dar, uende muhimbili,

Pia jaribu kuchanganya na mawazo ya wadau ujaribu kumdadisi daktari.
 
Pole sana Majan...Mungu akufanyie wepesi kwenye hili...

Ukiweza sana mpeleke na kwenye maombi..
Kwa sasa Anaendeleaje?
 
Pole Sana. Mpate Neuro physician haraka Sana. Wapo hospital kubwa. Pia mkande na Mafuta ya Karafuu. Pia ukipata Seaweed kiswahili Mwani inapatikana maduka machache Kariakoo mpatie. Pia maombi.
 
pole sana kwa changamoto iliyokupata

kuna mtoto wa jiran yangu nae alishawahi kupata ttzo linakokaribia kufanana na la kwako

ila huyu tatizo liligindulika Pale NSK hsp kwa dk wa mifupa anayekuja kutokea KCMc

mtoto aligindulika kuwa na jipu kwenye nyonga na alifanyiwa operation KCMC hsp na akapona

ila ndo mpk leo mguu wake mmoja ni mfupi.

usihangaike na waganga bado ni mapema mno
 
Pole Sana. Mpate Neuro physician haraka Sana. Wapo hospital kubwa. Pia mkande na Mafuta ya Karafuu. Pia ukipata Seaweed kiswahili Mwani inapatikana maduka machache Kariakoo mpatie. Pia maombi.
Hiyo mwani inatumikaje
 
kwasasa tunaendelea na tiba yakumchua kwa dawa zakisuni, yale maumivu makali usiku yameanza kupungua nakwasasa angalau vidole anaweza kuvichezesha
Cc Makiwendo
Safi Sana. Nijibu tu yote hapa. Umesema uko Mbeya na Mwani ni zao la Baharini. Inapatikana Sana DSM Yale maduka ya Kisuna na wanautoa Zanzibar. Binafsi ninautumia kama kirutibisho na tiba kwa mambo mengi hasa mifupa na misuli. Mwani au Seaweed iko ya Unga imesagwa na nzima. Ya Unga unakoroga kijiko kidogo cha chai kwa kikombe cha maji ya Moto unakunywa. Mtoto mpe nusu kijiko cha chai. Ulio mzima unachukua vipande viwili au vitatu unaloweka saa nzima(ni ngumu Sana) halafu unatafuna au unablend hata na matunda upate juice unakunywa). Itasaidia Sana. Kama Una ndugu mtume aende Kariakoo akutafutie akutumie. Ni maduka machache yanayouza Mwani hapo Kariakoo. Siku hizi mi ninaagiza Zanzibar maana bei pia iko chini kidogo Kwa 15,000 packet badala ya 20,000 Kariakoo. Naagiza za kunitosha hata 6 months. Ni food supplement nzuri Sana Kwa Sisi watu wazima umri umesogea mifupa na nerves zinachoka hivyo tuna boost.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…