Mwanangu amepoteza uwezo wakusimama na kutembea

Na
Nashukuru mkuu nitajaribu kuulizia kwa Tanga kama nitaweza kupata nina ndugu wengi huko
 
MPELEKE KWENYE MAOMBI KWENYE MAKANISA YA KIROHO..ANZIA KWA NABII ROLINGA MBEZI BEACH AFRICANA..MUNGU ATAMFUNGUA
Hap Sasa ndio umuhimu wa kina mwamposa inaonekana
Nashauri tu kuwa ukiwa unaendekea pia na tiba za hospital maombi pia kazania mkuu
 
Kuna mmoja alikuwa shemeji yangu, yeye alianza kuumwa mkono, aisee kimchezo mchezo akapelekwa mloganzila, kakaa pale karibu mwaka mmoja akiugulia maumivu lakini vipimo vinaonyesha hakuna kitu. Ikachukuliwa sample kwenda India ila majibu yakarudi yale yale. 11th March mwaka huu amefariki. Huwezi amani kama mtu anaweza umwa mkono mwaka mzima mpaka akafariki. Sina nia ya kukutisha ila kukuambia usichukulie masihara kwani unaweza mpoteza binti yako. Angaika kadiri uwezavyo.
 
Unachokisema kilimfanya mtu akapoteza binti yake(shemeji yangu) kwa kujua mtoto wake ana tatizo linaloweza tibika kisayansi.
 
Pole kwake, halafu pole Sana kwako! Ninaamini Ana shida zaidi ya mpira aliocheza, nashauri aende kwa daktary specially wa mifupa.

Ikishindikana huko pambana a na maombi, na sio Hawa manabii kama Mwamposa, hapana, watu wa kueleweka.
Ila babu usimidharau mwamposa mnk hata huyu wako Ni mtu tu Kama mwamposa

Muhimu Ni maombi
 
Pole mkuu nawasiwasi isijekua rare diseas kama ya mtoto wa masoud kipanya yule malcom au yule kijana wa Tanga jitahidi kuwaona wataalamu
 
Tafdhali sana Bab mtot j tatu utupe update za mwaneti

Mnk kwa sas unakuja dsm kufanya vipimo au unafanyia huko huko mbeya rufaha
 
Ila babu usimidharau mwamposa mnk hata huyu wako Ni mtu tu Kama mwamposa

Muhimu Ni maombi
Mwamposa binafsi huwa namwona kama tapeli au wakala wa shetani na hata KKKT aliwahi kufukuzwa. Japo inaweza kuwa kinyume chake.
 
Mm nilishashuhudia kabisa kijiji kwetu baba mmoja alipooza miguu ghafla walipeleka hosipital kupima hawaoni kitu ila alipoteza uwezo wa kutembea. Walileta mganga wa kienyeji ndani ya wiki yule baba alianza kuendesha mbaiskeli wanakijiji walikuwa wanashangaa na kushangilia miujiza. Haya mambo ushuhudie.Dunia Ina mengi yamejificha.
 
Kama wewe ni mkristo piga maombi
Kama wewe ni Muslim piga swala mkuu
Maombi maombi, acha upotoshaji ndugu. Nani alipona ugonjwa kwa kuombewa , toka lini kuongea kukatibu mwili wa mwanadamu
 
Mpeleke mhimbili haraka kwa madaktari wa neurosurgeon wakamwangalie, mtoto hajavunjika ila inaelekea kuna misuli imebanwa sehem
 
Zogwale, kama hutojali hebu leta faida kamili za mwani au seaweed, utakuwa umetufaidisha wengi, japo uzi hausiani na seaweed.

Sent from my D6616 using JamiiForums mobile app
Just Google Seaweed benefits also Seamoss benefits. Utaziona nyingi Sana. Ka packet nilicho nacho nacho kina benefits lukuki sema ndiyo hivyo Lugha gongana Sana.
 
Just Google Seaweed benefits also Seamoss benefits. Utaziona nyingi Sana. Ka packet nilicho nacho nacho kina benefits lukuki sema ndiyo hivyo Lugha gongana Sana.
Mwani nimeupata Jijini Tanga ambao haujasagwa wanapima kuanzia elf mbili,kilo moja 15000 sasa nimeambiwa kuna mwembamba na mnene sasa sijui best ni upi hapo mkuu
 
Mwani nimeupata Jijini Tanga ambao haujasagwa wanapima kuanzia elf mbili,kilo moja 15000 sasa nimeambiwa kuna mwembamba na mnene sasa sijui best ni upi hapo mkuu
Kaka, tujuze hali ya mtoto tafadhali.

Ulikwenda hospitali?

Vipimo vimeonesha nini?

Ana nafuu yeyote mpaka sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…