Mwanangu anashindwa kutumia common sense?? Hii ni shida gani?

Poleni sana kwa maumivu hayo ya ndani, kuna mwanadada mmoja pia yupo mahali anafanya shughuli zake namuona anashida kama hii uliyoielezea kwa kijana wako. Sina uhakika sanaa, lakini ninejaribu kufuatilia historia ya yule dada alilelewa na mama pekee, baba alikumbia akaiacha familia. Sasa nilikuwa nahisi pengine ni athari ya kulelewa na mzazi mmoja labda, sasa sijajua kwa upande wako mambo yapoje..? Na je tangu akiwa mdogo alikuwa ana-behave kwa namna gani?
 
Mpeleke kwa psychologist atamfanyia assessment na kutoa ushauri mzuri. Kuna mambo kadhaa ya kiafya (kama walivyochangia wengine) yanaweza kuwa sababu. Pia zingatia baadhi ya shauri zilizotolewa hasa ya kutathimini mawasiliano yako na yeye.
 
Common sense is not very common. Askari akikiongea na askari mwenyewe akataja neno magazine, yule mwenziwe anaweza kudhani kuwa linalitajwa ni chombo cha Kuhifadhi risasi; lakini mwandishi akitaja neno hilo hilo kwa mwandishi mwenziwe, huyo mwenzake anaweza kudhani kuwa kinachizungumziwa ni jarida. Inawezekana kabisa wewe ndiye usiyetumia common sense kwa sababu COMMON SENSE IS NOT VERY COMMON
 
Jaribu pia kumuelewesha umuhimu wa kile anachotakiwa kukifanya, hii itamsaidia sana kuzingatia na kuwa makini na kile anachokifanya. Imekuwa ni utamaduni wa familia nyingi kuwakurupusha watoto alfajiri na kuwataka wajiandae wawahi shule. Ni jambo jema lakini ukimuuliza mtoto kwa anaenda shule kuanzia j3 hadi ijumaa. Ni wachache sana wanaweza kukujibu kwa ufasaha.
 
Unaweza ukawa sahihi kwa upande wako ila naamanisha nachokisema hapa!!
vile vitu vya kawaida
 
ana behave hivyo akiwa mbele yako tu, nimefatilia huu Uzi na majibu yako kwenye comments,

nimegundua una tatizo kubwa sana.

ukitaka kumrekebisha mtu yeyote kiurahisi fanya in a positive way.

mfano kuna vitu vyake anavyofanya vizuri, hivyohivyo ndo unamsifia navyo

akiona wewe kama baba una appreciate anajiamini kwa kiasi kubwa sana na anaendelea kufanya vizuri zaidi

ila unavyojisifu kwa kumtandika mtoto wa miaka 17 unakosea,

huo ni unri flani ivi ambao mtu anajielewa sana kaa nae vizuri tuu, asione hata dalili za kwamba unamuona dishi limeyumba, haisaidii

hizo tabia zote nauhakika anaonyesha kwako ukiwa negative sana hautaweza kumuelewa

inabidi awe free kiasi kwamba hakufichi vitu, bila hivo utakua unasikia tuu kwa watu, anavuta bangi.. anafanyia hivi...

kwaiyo hiyo sio namna ya kumbadilisha mtu,
 
Nimelichukua hili
 
Hana tatizo la kusikia vizuri? Mimi nina tatizo la kusikia vizuri lilinikuta nikiwa around iyo iyo age ya mwanao mwanzoni ilikua ngumu kujikubali hata kitu ambacho sijasikia naitikia tu sometimes naulizwa kitu kingine najibu kitu kingine baada ya miaka kwenda nikajibali sasa hivi nikikutana na mtu sijuani nae mwanzo kabisa wa maongezi namwambia sisikii vizuri. Kama hana tatizo la usikivu basi chunguza kitu gani anapenda halafu muendelezo katika hicho hicho, binafsi naamini kila mtu ni genius katika angle yake.
 
Majibu yote ya maswali ya mtoa mada yatapatikana hapa.
Swali la kuongezea hapa je anaishi na mama wa kambo au mama yake mzazi?tatizo kubwa la mwanao kwa makisio yangu inahusiana na mambo ya saikolojia(lack of confidence).
Watu wa aina hiyo wakipataga nafasi ya kujiamini/confidence huwa wanakujaga kufanya maajabu na kila mtu anabaki mdomo wazi.
Hata mimi zamani nilikuwa naonekana hivyo mtaani kwangu na kwa jamii yangu lakini baadae nilikuja kuwaprove wrong na naweza kusema kwamba mimi ndio kijana niliyeonesha dira kwenye mtaa wangu na hakuna mwingine wa kunifananisha naye kwa mambo niliyowaonesha.
Kwa hiyo nikuondoe wasiwasi ndugu yangu,baadae atabadilika na utashangaa.
Watu wa aina hiyo huwa ni watu wa kutafakari sana kiasi kwamba akili inahama inakuwa iko mbali so wakati wewe unamuuliza swali fulani arakujibu tu ili mradi umuondolee kiwingu ili aendelee na tafakuri zake.
Ukimuuliza swali akakosea kujibu haimaanishi kwamba hajui jibu la hilo swali ila ni kwamba tu ubongo wake unakuwa bize na hataki umtoe kwenye reli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…