copernicucci98
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 1,232
- 2,362
Such a good hand writing!! Ananikumbusha enzi zangu. So neat!!Shule za msingi zinafungwa Leo, Niko hapa napitia mitihani na ripoti za wanangu!
Kuna swali hili; Mwamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu anaitwa nani? Mwanangu kajibu MWAMUZI kakosa, eti mwalimu kawaambia jibu sahihi ni REFARII.
Je, jibu sahihi ni lipi hapo? Kosa ni la mtoto au mwalimu ndo hajielewi?
View attachment 1807716
View attachment 1807714
Ndo hapo sasaLakini mbona swali la tisa kama vile mwalimu kachemsha pia kwa hio ngoma droo
Ndo hivo nakomaa nao wapo KAYUMBA! Sina mpango wa private schools hata kidogo! Kila siku tunasomaSijui niandike vipi, ila nahisi swali lenyewe kama kakosea kulitengeneza hivi.
Any way, ni udhaifu mdogo tuu mkuu wala usijali, hayo ni mambo ya kawaida + kibinaadamu.usipaniki
Ila mtoto wako genious asee[emoji2], hadi hati ya mwandiko inaonyesha. Kongole sana
Vizuri umekuwa Humble...umemkosea huyo mwalimu kusema "Hajielewi" sio vizuri.Kwanini mkuu
Hapana: ni mtoto yupo kayumba, sema namzingatia kufuatilia madaftali kila siku, tunafundishana jioni! NAIMANI TUTATOBOA TU KIBISHI maana private sina huo mpango!Huu muandiko mbona kama wa mtu wa sekondari?!!
Niko form two tukagewa mtihani ambao ulikua na section ya Question Tags.
Sikumbuki swali ila lilikua la 'I am ...' so naassume..
I am a doctor, ... ?
Mi nikajibu ' ain't I?' nikakosa.
Nikaenda kwa mwalimu kulalamika akanijibu siyo kwamba haupo sahihi lakini sahihi zaidi ni 'aren't I?'
Nafikiri inaapply kwenye swala la hili swali. Mahakamani kuna watu wanafanya maamuzi, bungeni, mpaka kwenye maswala ya ndoa. Plus kutokana na kiswahili kukosa misamiati mingi tunakopa sana maneno hivyo mwalimu kuweka hiyo nyanjo siyo kwamba mtoto hayupo sahihi ila sahihi zaidi ingekua 'refarii'
Case closed.Unajua mfundishaji wa watoto shuleni ni mfundishaji ndio lakini jina specific analoitwa ni mwalimu. Sasa ukijibu mfundishaji haujakosea Sana ila sio sahihi kwa 100%.
Ni sawa na ukamuita mtu mlimaji badala ya mkulima, au muendeshaji badala ya dereva.
Refarii ndiyo jibu sahihi kwa mujibu wa kingozi cha mwalimu (marking scheme).
Mwamzi ni jina jumuishi sana mfano mwamzi mahakamani anaitwa Hakimu/Jaji.
Nikiwa darasa la kwanza niliulizwa kwenye mtihani kuwa sare tunayovaa shuleni inaitwaje nikajibu ni sweta, shati na kaptura. Nilishindwa kabisa kujua kama yunifomu ni neno la kutumika katika Kiswahili, kati ya mitihani yangu pendwa ninayoitazama na kufurahia na ule upo.
Referee ni kiingereza , kiswahili n mwamuzi, mwalimu kakoseaUnajua mfundishaji wa watoto shuleni ni mfundishaji ndio lakini jina specific analoitwa ni mwalimu. Sasa ukijibu mfundishaji haujakosea Sana ila sio sahihi kwa 100%.
Ni sawa na ukamuita mtu mlimaji badala ya mkulima, au muendeshaji badala ya dereva.
Hadi hapa sijapata jibu sahihi inamaana huu mtihani na humu wote tungefeli au?Refarii ni (referee) ni neno la kiingereza, je kwenye kiswahili linatumika hivyo hivyo?
Kiplefti -Keep left
Imeishaje ? Hujui Referee n kiingereza na kiswahili ni Mwamuzi? Au wew ndio mwalimu nini?Thread imeishia hapa....safi sana mkuu shakir.
Jibu ni REFA
Neno mwamuzi limetumika kuuliza swali, kwahiyo huwez kulitumia kujibu swali. Mfundishe mwanao hii kitu isije kumuathiri huko mbele.
Tanzania ina shida hiiMkuu mwanao mjanja mjanja sana. Katelezea kwenye swali mule mule, mwamuzi wa mpira anaitwa, nae karudia mwamuzi!
Hivi mkuu nikikuuliza fundi wa ujenzi wa nyumba anaitwa nani utasema fundi au muashi
Tukiuliza askari wa usalama barabarani anaitwa nani utasema askari au trafiki
Tukiuliza muendesha ndege anaitwa nani utasema mwendesha ndege au rubani
Imeishaje ? Hujui Referee n kiingereza na kiswahili ni Mwamuzi? Au wew ndio mwalimu nini?
Umeona nimeandika kizungu hapo?Tanzania ina shida hii
Huon hapo unazunguka kwenye kizungu na kiswahili tu ?
Ndio wasomi lakn , mwalimu pamoja na wewe mmefeli
Traffic ni kimasai??Umeona nimeandika kizungu hapo?
Mtoto yuko sahihi. Sidhani kama tuna neno la Kiswahili zaidi ya kumuita refa.Shule za msingi zinafungwa Leo, Niko hapa napitia mitihani na ripoti za wanangu!
Kuna swali hili; Mwamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu anaitwa nani? Mwanangu kajibu MWAMUZI kakosa, eti mwalimu kawaambia jibu sahihi ni REFARII.
Je, jibu sahihi ni lipi hapo? Kosa ni la mtoto au mwalimu ndo hajielewi?
View attachment 1807716
View attachment 1807714
Kwahiyo katika kiswahili hakuna maneno yaliyoazimwa katika lugha zingine ikiwemo kingereza na yakawa rasmi?Traffic ni kimasai??
Referee ni neno la kiingereza, kiswahili ni mwamuzi