Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwanariadha wa Uganda, Rebecca Cheptegei, mwenye umri wa miaka 33, amefariki leo Alhamisi akipatiwa matibabu kutokana na majeraha mabaya baada ya kushambuliwa na mpenzi wake kwa kumwagiwa petroli na kuchomwa moto nyumbani kwake nchini Kenya.
Katika tukio hilo la kikatili, Cheptegei aliungua zaidi ya asilimia 80% ya mwili wake, na licha ya juhudi za madaktari kumsaidia, viungo vyake vilishindwa kufanya kazi usiku wa jana.
Cheptegei, ambaye alishiriki mbio za Olimpiki ya Paris mwezi Agosti, alikuwa akipatiwa matibabu maalum katika chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Moi Teaching and Referral Hospital, mjini Eldoret, Kenya. Shambulio hili linasemekana kutekelezwa na mpenzi wake, raia wa Kenya, ambaye alijaribu kumchoma moto kwa sababu ambazo bado hazijafahamika kikamilifu.
Shirikisho la Riadha la Uganda (UAF) pia limethibitisha kuaga dunia kwa Cheptegei katika andiko lao kwenye akaunti rasmi ya X, na kutaka haki itendeke likisema "aliangukiwa na vurugu za nyumbani. Tuna masikitiko makubwa kutangaza kifo cha mwanariadha wetu Rebecca Cheptegei mapema leo asubuhi, ambaye alihusika na dhuluma za nyumbani"