TANZIA Mwanariadha Rebecca Cheptegei aliyechomwa moto na mpenzi wake kutoka Kenya afariki dunia

TANZIA Mwanariadha Rebecca Cheptegei aliyechomwa moto na mpenzi wake kutoka Kenya afariki dunia

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mwanariadha wa Uganda, Rebecca Cheptegei, mwenye umri wa miaka 33, amefariki leo Alhamisi akipatiwa matibabu kutokana na majeraha mabaya baada ya kushambuliwa na mpenzi wake kwa kumwagiwa petroli na kuchomwa moto nyumbani kwake nchini Kenya.

Katika tukio hilo la kikatili, Cheptegei aliungua zaidi ya asilimia 80% ya mwili wake, na licha ya juhudi za madaktari kumsaidia, viungo vyake vilishindwa kufanya kazi usiku wa jana.

1725522183396.jpeg

Cheptegei, ambaye alishiriki mbio za Olimpiki ya Paris mwezi Agosti, alikuwa akipatiwa matibabu maalum katika chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Moi Teaching and Referral Hospital, mjini Eldoret, Kenya. Shambulio hili linasemekana kutekelezwa na mpenzi wake, raia wa Kenya, ambaye alijaribu kumchoma moto kwa sababu ambazo bado hazijafahamika kikamilifu.

Shirikisho la Riadha la Uganda (UAF) pia limethibitisha kuaga dunia kwa Cheptegei katika andiko lao kwenye akaunti rasmi ya X, na kutaka haki itendeke likisema "aliangukiwa na vurugu za nyumbani. Tuna masikitiko makubwa kutangaza kifo cha mwanariadha wetu Rebecca Cheptegei mapema leo asubuhi, ambaye alihusika na dhuluma za nyumbani"

1725522219543.png
 
Wanaume wanao kimbia vikao ndo wanatuaibisha.Sasa unachoma moto mtoto wa watu kwani umekua Mungu???.Waganda tafuteni kwa aina yoyote huyo mbulu kenge mkamalizane nae huko uganda.Hata kama ni mwanaume kampeni ujauzito zake.😭😭.
 
Kwa masikitiko makubwa, familia ya mwanariadha kutokea nchini Uganda Rebecca Cheptegei imetangaza kifo cha mwanariadha huyo ambacho kilitokea wakati akipokea matibabu jijini Nairobi,

Ikumbukwe kuwa, siku mbili zilizopita iliripotiwa kuwa Bi. Cheptegei alishambuliwa na mpenzi wake Bwana Dickson Ndiema kufuatia mzozo wa kugombania mali.

Imeripotiwa kuwa mshukiwa wa kesi hiyo alimchoma moto mwanariadha huyo kipindi wapo katika nyumba yao huko Trans Nzoia.

photo_5967624378394985417_x.jpg

Kipchegei alipata majeraha makubwa ya moto kufuatia tukio hilo ambapo takriban asilimia 80 ya mwili wake uliungua.

Kipchegei alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Moi iliyopo Eldoret kwa matibabu kisha baadae kuhamishiwa jijini Nairobi kwa huduma maalum.

Mume wa Bi Chepchegi yaani bwana Dickson Ndiema, naye pia alipata majeraha ya moto kutokana na tukio hilo na amelazwa hospitalini pia.

Source: Buzzroom Kenya
 
Attachments

  • photo_5967624378394985417_x.jpg
    photo_5967624378394985417_x.jpg
    45 KB · Views: 5
Kama sijaelewa, Bwana Dickson ndiye aliyegombana na mpenzi wake Rebeca kwa sababu ya mali, ikapelekea Rebeca kuchomwa moto, naye Dickson tena akaungua na moto kiaje au kivipi?
Mashuhuda wanasema walimuona Dickson akimwagia Rebecca petrol nje ya nyumba yake huku wakigombana.

Inawezekana wakati wanazozana kuna petrol kidogo ilimmwagikia Dickson pia.
 
Mwanariadha wa Uganda, Rebecca Cheptegei, mwenye umri wa miaka 33, amefariki leo Alhamisi akipatiwa matibabu kutokana na majeraha mabaya baada ya kushambuliwa na mpenzi wake kwa kumwagiwa petroli na kuchomwa moto nyumbani kwake nchini Kenya. Katika tukio hilo la kikatili, Cheptegei aliungua zaidi ya asilimia 80% ya mwili wake, na licha ya juhudi za madaktari kumsaidia, viungo vyake vilishindwa kufanya kazi usiku wa jana.
View attachment 3087577
Cheptegei, ambaye alishiriki mbio za Olimpiki ya Paris mwezi Agosti, alikuwa akipatiwa matibabu maalum katika chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Moi Teaching and Referral Hospital, mjini Eldoret, Kenya. Shambulio hili linasemekana kutekelezwa na mpenzi wake, raia wa Kenya, ambaye alijaribu kumchoma moto kwa sababu ambazo bado hazijafahamika kikamilifu.

Shirikisho la Riadha la Uganda (UAF) pia limethibitisha kuaga dunia kwa Cheptegei katika andiko lao kwenye akaunti rasmi ya X, na kutaka haki itendeke likisema "aliangukiwa na vurugu za nyumbani. Tuna masikitiko makubwa kutangaza kifo cha mwanariadha wetu Rebecca Cheptegei mapema leo asubuhi, ambaye alihusika na dhuluma za nyumbani"
View attachment 3087578
Huyu akamatwe na afanyiwe ukatili zaidi ya alivyofanya yeye.
 
Kwenye hizi posts, wanaume huwaoni. Ingekua mwanamke ndo amemchoma moto mwanaume wangesimamisha mishipa hapa.

Saizi dunia inaharibiwa na hao hao wanaume. Baba mzazi anabaka mtoto wake alafu yanakaa kuteteana. What a gender
Una mihemko sana kama mjamzito.
Uzi ndio kwanza umeanza,tulia wachangiaji waje.
Kwani katika makosa waliyofanya wanaume hayakuadhibiwa!??
Au unajisahaulisha!?
 
Back
Top Bottom