We jamaa unalipenda sana hilo neno "malaya", sijui ndio umeambiwa ni kati ya maneno ambayo ukiwaita wanawake wanaumia, kwa bahati nzuri au mbaya hawa wa kizazi hiki na vizazi vinavyokuja mtawaita majina yote ila hawaumii wala hawajali tena
Na wangekuwa wanajali basi mngeshaanza kuona mabadiliko ila ndio kwanza hao so called 'malaya' wanazidi kuongezeka, na matokeo yake wanaume ndio mnabaki kuumia kihisia kwa kukosa 'wife material', so ni either muanze kubadilika ninyi au muendelee kujifariji na kuwatukana wanawake hadi mwisho wa dahari
Yeye kutafuta attention ya wanaume wengine siyo kosa lake kwa sababu hapo alipo hana uhakika kama huyo mwanaume ndiye atakayemuoa, kwa sababu hata huyo mwanaume nina uhakika hapo alipo hana mwanamke mmoja na wanawake wengi wanajua hilo maana huwa mnasema wenyewe, sasa kwa tamaduni zetu anayeamua ndoa ni mwanaume
Mwanaume ndiye anayejua katika ya hao wanawake alionao atamuoa nani atamuacha nani ilihali mwanamke hajui kama yeye ndiye atakayeolewa hapo au la, kwahiyo hata akitafuta attention ya wanaume siyo mbaya pengine akiongeza wengine na probability ya kuolewa inaweza kuongezeka kuliko akiwa na mmoja, hivyo msiwalaumu wanawake jilaumuni wenyewe kwa umalaya wenu mlioupa jina la 'nature'
Hata population yenyewe tu inawakataa na hairuhusu kila mwanaume kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja, na kama ambavyo huwa mnasema mwanaume anatakiwa kuhudumia mwanamke ambaye yuko naye kwenye ndoa tu (japo huwa mnahudumia mpaka michepuko), basi vivyo hivyo na mwanamke anayetakiwa kutulia ni yule ambaye yuko kwenye ndoa tu