Mwanaume anaona uzito kumuoa binti baada ya kuona post zake na comments zake mtandaoni

Sio kweli! Kuna mtu atakupenda hivyohivyo ulivyo bila kuangalia unahusiana vipi na watu kwenye mitandao ya kijamii muhimu mkiwa wawili mnapeana amani na heshima.
Ni kweli kabisa Issue ni kwamba mtu anataka mtazamo wake au mawazo na hisia zake iwe ni final say
 
Tatizo si unacho post bali unachofikiri.

Ni muhinu kwa mtu kuoa mtu ambaye wataendana, kuepusha migogoro kwenye ndoa.

Sasa kwa msingi huo, ni muhimu kila mtu apost anachotaka, anachoona sawa. Bila self censorship.

Mwanaharakati anayependa mwanaharakati wa upinzani akimuona mwanaharakati mwenzake, atavutiwa, wataendana.

Mtu anayetaka mke mwenye maneno ya mipasho, atampata anayemtafuta.

Sasa mwanamke hajui uanaharakati, anajua mipasho, ajifiche kwa kutaka kuolewa tu? Akiolewa halafu akianza maneno ya mipasho kwenye ndoa, kwa mume anayependa mwanaharakati asiyependa mipasho, si ndiyo ndoa inaishia kwenye talaka ya haraka hapo?

Hakuna sababu ya mwanamke kujificha ukweli wa alivyo kwa kuhofia hataolewa, kwa sababu kwenye ndoa atakuja kujulikana tu.

Tuache maisha ya kua act sinema tuishi maisha ya uhalisi zaidi.

Pia, tujenge uchumi mzuri kiasi kwamba ndoa isiwe ndiyo lengo, kimbilio na wokozi wa mwanamke. Mwanamke aishi maisha yake anavyotaka hata asipoolewa awe anaweza kuishi bizuri tu.

Kwa sasa tumefanya ndoa kama lengo la mwanamke ili aweze kuishi vizuri.
 
Kabisa , kuna mdada anaposti ma pombe ila namwona huyu ni wife material kabisa, mwingine anahubiri injili naona hapa hakuna kitu
 
Wanaume wote wangeangalia tunayoyaandika mitandaoni basi wengine tusingeolewa.
Anajifanya hajui wanaume wengine wanachojali ni wowo mneso tu, wengine sura tu, wengine mtindi tu, wengine urefu tu, wengine akili tu, wengine vyote au kadhaa kati ya hivyo.
 
Kabisa , kuna mdada anaposti ma pombe ila namwona huyu ni wife material kabisa, mwingine anahubiri injili naona hapa hakuna kitu
Exactly.

Kwa sababu kila mtu ana type yake tofauti. Hakuna haja ya ku fake maisha ili tu mwanamke aolewe.

Mwanamke mpenda pombe akijifanya mlokole, akaolewa na mlokole, huko kwenye ndoa atapata tabu sana, kwa sababu yeye ataingia kwenye ndoa kama mtu asiyekunywa pombe, wakati anapenda sana pombe.

Kuwa fake kutamnyima kuishi kwa uhuru mpaka hiyo ndoa itapata matatizo. Ndiyo mwanzo wa mtu kunywa pombe kwa siri chooni halafu akagundulika na ndoa ikaishia talaka ya haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…