Mwanaume asiye na Pesa hukosa mvuto ndani ya Jamii

Mwanaume asiye na Pesa hukosa mvuto ndani ya Jamii

Jamii yetu imetufundisha kuona thamani ya mwanaume kupitia mfukoni mwake.

Ndio maana mwanaume asiye na pesa mara nyingi anaonekana hana mvuto, kwa sababu pesa imetafsiriwa kama usalama,uwezo na uongozi.

Mwanaume asiye na pesa hukosa uwezo hata wa kutoa maamuzi ndani ya familia yake mwenyewe na wakati mwingine hushindwa hata kujiamini.

Mwanaume asiye na pesa huweza hata kudharauliwa na kunyimwa nafasi aliyopaswa kuwa nayo ndani ya familia na Jamii kwa ujumla.

Watu wanataka kujua kesho itakuwaje, na kwa bahati mbaya pesa imekuwa ndio jibu la haraka.

Kwa hiyo kama huna pesa sasa, usikate tamaa. Jenga akili yako, jenga tabia yako,jifunze kutoka kwa wengine waliofanikiwa Ili nawe ufanikiwe
Na wewe maoni yako ni yapi ?
Hata Baba yako ni Mwanaume kumbuka hilo.

Je ana hela au hana ? Mvuto , heshima na ushawishi kwenye jamii anao ?

Muwe mnaandika vitu vinavyoakisi uhalisia wa mambo sio motivation speech ambazo hubaki bila maana yoyote.

Mwenye pesa na asiye na pesa bado wanabaki kuwa ni wanaume.
Pesa ni muhimu lakini character ni muhimu zaidi kwenye hqya maisha.

Mzee Lowassa (rip) pamoja na mipesa yake yote alishindwa kupata afya timamu. Tuwe tunafikiria kwa kina na mapana
 
Naona Muslimah ShesRise_1 umenipa like leo ntaota 😍
Nini maoni yako ukizingatia imani yako ya kidini ? Maana Uislamu ndio dini inayoelezea uhalisia wa maisha yetu hapa duniani
 
Naona Muslimah ShesRise_1 umenipa like leo ntaota 😍
Acha basi😅
Nini maoni yako ukizingatia imani yako ya kidini ? Maana Uislamu ndio dini inayoelezea uhalisia wa maisha yetu hapa duniani
Mwanaume iwe bible iwe Qur'an imemtaja kama kicwa cha familia
Hii ni Asili ya uumbaji

Mwanaume hapaswi kupimwa uanaume wake au mvuto kwa vile anavyovimiliki

Bali apimwe kwa character zake zina mfanya awe Mwanaume!

La mwisho Mwanaume kwa asili ni m miliki
So akimiliki pesa na mali nyingi
Huongeza mvuto na ushawishi hasa kwa dunia ya sasa
 
Heshima ya mwanadamu inatokana na uchamungu na tabia njema, Pesa, mafanikio na riziki ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu unaoweza kubadilika wakati wowote (Wangapi walikuwanazo lakini leo imebaki kuwa ndivyo sivyo ?). Utajiri unaweza kuondoka, lakini utu, imani na maadili ndivyo vinavyompa Mtu heshima ya kweli mbele ya jamii...

Kwanza hao matajiri wana majivuno, ni waoga wana mabodigadi wengi na hawachangamani na watu huo mvuto wana utoa wapi? 😅😅😅

Tutafute pesa tu lakini utu, imani zetu na maadili tuvizingatie
 
Acha basi😅

Mwanaume iwe bible iwe Qur'an imemtaja kama kicwa cha familia
Hii ni Asili ya uumbaji

Mwanaume hapaswi kupimwa uanaume wake au mvuto kwa vile anavyovimiliki

Bali apimwe kwa character zake zina mfanya awe Mwanaume!

La mwisho Mwanaume kwa asili ni m miliki
So akimiliki pesa na mali nyingi
Huongeza mvuto na ushawishi hasa kwa dunia ya sasa
Hii mada imekaa kichokozi kwa sababu hata Baba zetu ni Wanaume na bado we are still proud of them walitubeba viunoni mwao 😅

Hatuwezi kushusha hadhi ya Wanaume kwa sababu ya kukosa pesa, na wewe unaelewa hata hii riziki ni mtihani Allah humpa amtakae na humnyima amtakae... Huwezi ukakosa kabisa lakini utapata kile unachostahili..

Tafuta mawaidha ya Shehe Mohamed Omary - Starehe katika maisha yako ndio utaelewa.
 
Ni kweli
shukrani kaka🙏
 
Back
Top Bottom