Inatakiwa kuwa na utimamu wa akili kulijadili hili na sio akili za mlipuko wa hisia.
Sasa nitakuuliza mfano Mwanaume akaja muoa dada yako mzuri sana. Na huyo mwanaume anapesa na anatoka familia ya kujiweza. So dada yako ana uhakika wa kupata mahitaji yote atakayo hadi uzeeni.
Je umri unavyozidi kwenda dada yako ataendelea kuwa na uzuri ule ule wa usichana hata akifika umri wa miaka 40+ ?
Maana huyu mwanaume anauhakika wa kuendelea kuwa na pesa hadi wakati huo na pengine pesa zitaongezeka mara dufu.
Mwanamke na mwanaume wana mahitaji natural. Ukitaka kuyafahamu rejea maisha ya kijijini yale maisha ya asili bila hizi material things yaani haya maisha ya mjini. Hapo ndipo utajua kuwa mwanamke kwa sasa anahisia zinazoendeshwa kwa tamaa na sio ukweli au uhalisia.
Mwanamke anatazama video za muziki anaona ile lifestyle ya wanawake wa marekani mara wameshika iPhone 14 pro max, magari ya bei, nyumba, mavazi, zile hotel mitoko basi ubongo wake unashawishika kuvitamani vile vitu na anataka kijana wa kitanzania ambaye hata kumudu kumnunulia Infinix ya laki mbili ni mtihani ampatie hayo mahitaji ambayo jumla yake ni mamilioni ya shilingi.
So mwanamke ambaye anaendeshwa na tamaa anakuwa hana tofauti na mtoto mdogo anayeamini baba yake anaweza mnunulia chochote anachotaka hata akitaka usiku wa manane na asipopewa basi kilio kinaanza.
Sasa kama ndio wanawake wenyewe ndio wapo hivi na tunatakiwa kujenga nao familia na jamii basi tumeshafeli. Maana sisi wanaume tunaishi kwenye uhalisia na sio ulimwengu wa tamaa.
Hiyo miili ya wanawake unayosema tunavutiwa nayo ni maumbile waliyopewa free na MUNGU hawajalipia wala kugharamia hata mia moja wao kwann waweke dau ili sisi kuwa nao baada ya kuvutiwa na uzuri wao?
Sent from my JKM-LX1 using
JamiiForums mobile app