Mwanaume mzima unaishi Nyumba ya kupanga?

Mwanaume mzima unaishi Nyumba ya kupanga?

Makonde plateu

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
1,443
Reaction score
3,480
Kiukweli huo ni ujinga unajiitaje mwanaume au gentlemen halafu unaishi nyumba ya kupanga hio si aibu? Yaani kabisa unajiita gentlemen halafu unaishi ya kupanga mpaka leo kiukweli huo ni umama

Inashangaza kabisa nyumba zilivyokuwa rahisi halafu utamkuta mburula mmoja anaishi kwenye nyumba za kupanga anahama nyumba hii 😄 anaenda nyumba yeye miaka yake yote anaishia kwenye nyumba miaka hebu badilikeni bwana nyumba national housing zinauzwa kwa bei rahisi halafu wewe unajihangaisha na nyumba za kupanga kweli wewe ni mwanaume? Au mdada mwenye muonekano wa kiume?

Kuishi kwenye za kupanga huo ni umama yaani kiukweli mimi nikimuona au nikijua mwanaume anaishi nyumba za nyumba namuhisi akili zake hazipo sawa au ni mdada mwenye muonekano wa kiume.
 
Kujenga tunajenga sisi tusiokua na uhakika wa maisha, mtu anaweza kuwa na million 200 leo, lkn akipika hesabu hajua kama atawahi pata nyingine...kuwa safe na future anaamua kujenga....

Mtu hana uhakika kama watoto wake watapata ajira au watakuwa na maisha mbeleni- anajenga ili wawe na kwao...hakuna uhakika wa cash

Watu wanaiba, magumashi mengi...hawajui kama watapata nafasi hizo tena, kuwa safe na kupunguza matatizo ya mbeleni anaamua kujenga....

Waajiriwa-Government na Serikali- mtu akipiga mahesabu ya kustaafu au akipunguzwa kazi...anaona bora ajenge...ili kupunguz potential matatizo....

HIVYO TUNAKIMBILIA KUJENGA SABABU HATUNA UHAKIKA WA KESHO- NO CASH INAYOELEWEKA...

Nenda Masaki nimekuta wahindi wanapanga kwenye apartments mwaka wa 20...yaani wamezalia watoto hapo mpaka watoto nao wanajitegemea....Wanalipa tu 2.5 M kila mwezi, tena wakiamua wanalipa mwaka mwaka...

Kuna watu walijenga majumba, mikocheni, masaki, oysterbay huko, upanga....Sasa hivi wameyakimbia wanapangisha watu wenye liquidity na cash wapate kipato...wenyewe wanarudi mbezi beach huku..wengine nje ya mji huko..

Nimeona dada Mweusi kaolewa na Bwna wa Kizungu...Wana uza vifaa vya bomba, mashine etc...wamekaa sehemu mwaka wa 12....fully furnished property..kulipa kodi ni kama kununua kilo ya nyama....na hawana hata kiwanja na hawana presha ya maisha kabisaaa...

Hapo ndipo nilijifunza watu wenye uhakika wa kipato wanaulimwengu wao mwingine kabisa...wakati wewe unawaza kujenga kinyumba chako kwa kuungaunga..wao wanawaza vitu tofauti kabisa....
Na wakijenga wanajenga kweli nyumba....sio hizi sukuma wiki zetu..

Pia nimegundua..kwa miji mikubwa mfano DSM..Kuna wenye nyumba wengi ni maskini kuliko hata wapangaji wao....Na ndo maana mtu akichelewa mwezi tu..hali tete......

Nimefurahi juzi Rais Mama Samia katusii vijana tutengeneze uhakika wa vipato continuously na sio kutegemea mishindo ambayo haina mizizi...

MTOA MADA KIKUBWA NI KUWA NA UHAKIKA WA KIPATO CHA MIAKA....Waafrika tunakimbilia kujenga kwa sababu ya umaskini na kutokuwekeza kwenye future inayoeleweka..achana na hayo mawazo mgando..kama unawatoto watengenezee channel za mifereji ya pesa, waambie watafute pesa kwa haki...usiwaambie masuala ya kujenga..mwisho wa siku utagundua kumbe PESA ndo JIBU LA MAMBO YOTE...

Ronaldo Saudia Pale kapanga five star hotel..milllions of money...

TUTAFUTE KUWA NA CASH AND LIQUID ASSETS..

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom