Mwanaume tajiri anafaidika vipi na ndoa zaidi ya ngono tu?

Ndoa is all about Company.
Pesa hai-apply kwenye Ndoa, usije ukadanganywa. Ukiona mwanaume anatafuta Mwanamke wa kuoa Kwa sababu anadai anapesa na sio Kwa sababu ya upweke. Basi jua bado hajafikia kuingia ndoani.

Pesa haina uwezo wa kuondoa upweke. Bali MKE/Mume unayempenda na anayekupenda automatically anaweza kuondoa upweke
 
subiri upate na ukimwi kwa huo utajiri wako
 
Umeongea point ya msingi sana.

Kisaikolojia mtu ambaye ana rafiki wa karibu ambae anapata kupiga nae stori na kupeana moyo kwenye mambo mbalimbali basi mtu huyu anakuwa hana upweke tofauti na mtu ambaye hana rafiki wa karibu.

Dhana ya ndoa inatupa watu ambao ni zaidi ya marafiki ambao tutalala nao usiku pamoja,tutaamka pamoja.

So mke akiwa rafiki na muelewa,na akiwa mnapeana moyo kwenye changamoto na mkawa watu wa kushukuru hata kama kuna magumu mnapitia basi utakuta wiooa wanakuwa sio wapweke.

Shida ni kwamba wengi wameoa wanawake ambao hawawezi kuwafanya marafiki.
Wameoa wanawake ambao hawawezi kupiga stori zingine za maisha.
Wameoa wanawake ambao hawawezi kushea nao mambo mbalimbali.
 
Mimi sio mwanaume lakini
Familia ni jambo la Msingi sana kama likijengwa katika misingi ya baba kusimamia nafasi yake ipasavyo na mama kusimamia yake.
1. Mnaendeleza kizazi, watoto ni baraka na faraja
2. Unapata mshauri wako, msiri wako, rafiki yako, mafariji wako, mtani wako, mwandani wako na mambo mengine mengi ndani ya mtu mmoja
3. Hakuna raha kama kula maisha na mtu mnaeongea lugha moja UKIWA MALAYA MALAYA huwezi kuelewa.
 
Uzuri ni kwamba Mtu mwenye pesa kama hizo ulizotaja huwa hana mawazo ya kijinga kama haya.
Usibishe mkuu...sema hujawahi ona ila wapo. Mimi yupo mwamba namfahamu, kipato chake chaweza kuwa 100ml+ kwa mwezi. Yuko kwenye 35+. Hajaoa, na amezalisha wanawake tofauti....saivi anatoka na ma super star kina mobeto nk. Yaani kiufupi wapo sana tu.
 
Kumbe unazungumzia Diamond? Nilijuanninwewe mwenyewe😅😅
 
Perfect
 
Kwanza lipia tangazo, halafu ndoa ni heshima, unatakiwa uishi na familia yako, watoto wapate malezi ya wazazi wawili, ili wawe na maadili kama wewe, wacha kuishi kihuni huni.
 
Shida ni kwamba wengi wameoa wanawake ambao hawawezi kuwafanya marafiki.
Wameoa wanawake ambao hawawezi kupiga stori zingine za maisha.
Wameoa wanawake ambao hawawezi kushea nao mambo mbalimbali.
Wameoa kina nani sasa ?....au wameoa 'wanyapara' ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…