Let's be real!!!
PART 1: UHALISIA WAKO MTOA MADA.
Mkuu una shida paala!
"nilimfukuza nyumbani baada ya kushawishiwa na ndugu zangu"
Inakuaje mahusiano yako unaruhusu watu wa nje ndiyo wakushawishi kufanya maamuzi??
Wewe kama mwanaume kichwa cha familia na mtu mzima mwenye akili timamu, pamoja na kuelewa hali halisi ya Mkeo, hujui nini Ufanye mpaka ndugu zako ndiyo wakushinikize kufanya maamuzi ??
Anaeishi na mwanamke ni nani? Kanisa, Ndugu zako au wewe?
Anayepitia magumu kutokana na tabia za Mkeo ni nani? Wewe, Kanisa au ndugu zako?
Mwanamke anatoka nje ya ndoa mpaka ushaidi unao, bado huelewi nini ufanye kutatua tatizo??
Kuna kitu hakipo Sawa....
Njoo part 2.
PART 2: IMANI YAKO KATIKA DINI.
Hapa napo una shida boss.
Unapeleka matatizo yako kanisani ili yatatuliwe ili hali mwenyewe unakiri kuchepuka kwasababu ya UPWEKE.
Mkeo awe chanzo cha wewe kuishi maisha hayo halafu matatizo hayo badala ukae uone nini cha kufanya, unayabeba na kupeleka kanisani kisa kufuata taratibu za Kanisa ili hali UNAVUNJA SHERIA ZA MUNGU kwa kufanya uzinzi, huoni kuna sehemu haupo Sawa??
Halafu inakuaje unaruhusu kushikiwa akili na Dini. (Binafsi ni mkristo pia na ninaye amini katika Mungu, hivyo siongei haya kwasababu ni mpagani, HAPANA).
Kila kitu na kiwe na KIASI katika maisha, Mungu ana sehemu yake ya kufanya na wewe pia una sehemu yako ya kufanya. Inapofikia hatua kuruhusu KILA KITU maamuzi yafanywe na Kanisa ili hali wewe ndiye unayeona na kuelewa undani wa tatizo, hii inaonyesha dhahiri unakabidhi nafasi yako kama mwanaume upande wa pili.
JAMANI MAMBO KAMA HAYA NI MFANO HALISI WA KWANINI ASILIMIA KUBWA YA WAKRISTO WANAISHI MAISHA YA SHIDA NA WENGI HUWA HAWAFANIKIWI KATIKA MAISHA.
Dini kuruhusu Itawale maisha yako kila ENEO pasipo kushirikisha upeo binafsi ni UTUMWA.
Ulishawahi kushirikisha kanisa kuhusu KUCHEPUKA KWASABABU YA UPWEKE??
Nina Imani hilo bado hujalifanya.
Nina mengi ya kuandika, ila Kiufupi ZINDUKA!! Maisha yako yasimamie WEWE na uwe na utashi wa kufanya maamuzi wewe mwenyewe na lile linaloshindikana kabisa Shirikisha watu ukiwa tayari una maamuzi yako binafsi bila kujali washauri watasema nini.
Sasa angalia kwasasa unataka kulazimishwa kusamehe ilihali mwenyewe unakiri nafsi yako inagoma, ila kwa vile ni DINI inataka hivyo unajilazimisha iwe hivyo.
Haya, baada ya kufuata ushauri wa kidini wa KUSAMEHE ili hali wewe bado una kinyongo moyoni, humo ndani mtaishi kwa AMANI au ni mwendo wa KUWA MNAFKI KWA MWENZIO, kuonyesha yameisha ilihali bado una machungu moyoni??
Na kwa hali hiyo unadhani UTAACHA kuchepuka zaidi kuitafuta furaha uko nje??
Maisha wengi huwa wana fake kwasababu ya kuogopa JAMII ITANIONAJE, ili hali magumu unapitia wewe, shida ni zako, na jamii inakutazama ukiteseka, halafu bado unaionea HAYA katika kufanya maamuzi!! Hii kitu naiona kwa wengi sana, hasa kwa hawa watu wanaojifanya kuamini Katika Dini.
Aisee maisha ni mafupi sana kuruhusu kila ushauri wa mtu kuendesha maisha yako.
FANYA VILE MOYO WAKO UNAPENDA, ACHANA NA MENGINE.
Be a man Bro!