Mwanaume ukiwa na kitu hiki hata kama handsome umenikosa

Mwanaume ukiwa na kitu hiki hata kama handsome umenikosa

Huu uzi unahusu saa kweli😂, ukute ni nanii zisizosimama
 
Mimi sipendi saa ya mkononi..navaa african bracelet au culture handmade natengeneza mwenyewe
Onelove!
 
Mtu mwenye akili timamu unavaaje saa mbovu? Ni ushamba mkubwa sana....
 
Hivi unamaanisha saa kama saa au saa ipi inayoendana na majira? 🤔

Maana wengine vichwa vyetu vinatupeleka kwingine kabisa kimawazo
 
Bora hata hao wanaovaa saa mbovu,sisi wengne sura za uso wa kima na hatuvai saa na tunadunda...huwezi kumfurahisha kila mtu!!....
 
Ila mimi mwenyewe nikimuona mwanaume mwenzangu kavaa saa mishale haizunguki, hua najisikia vibaya sana.
Au saa imepauka mikanda.🥺moyo huwa unauma sana.
 
Hello,

Sijui kwanini siwezi kuvumilia hiki kitu, wewe unaweza kuona kawaida lakini kiukweli kwa upande wangu inaniboa. Mwanaume nikimuona hata kama awe smati vipi Halafu kavaa saa ya mkononi haisomi majira aisee

Badilikeni
Una umri gani? Zamani kidogo miaka ya 1980 .... babu zako walizivaa sana, tena kuna zinazoenda pole pole lakini mwenye nayo anaijulia. Ukimuuliza muda ataangalia na atakupa muda kamili. Sasa ukosee uichungulie utasoma majira sio ama imekimbia au ipo nyuma. Halafu kila jioni lazima zichochewe yaani kila 24 hrs. Hizi ni za mshale sio digital.
Pia kulikuwa na mafundi saa wanaendesha maisha kwa kazi hio
 
Leo umevaa saa uko Dar ukaweka muda wa TZ, wiki ijayo ukawa Capetown,muda wa South,Wiki inayofuata ukawa Juba Sudan,Mwezi ujao ni Kingston Jamaica. Saa yangu naipenda mngao wake na bei yake .Why unichukie wakati muda nafahamu kwa simu.
 
Back
Top Bottom