Mwandishi mkongwe Abdallah Majura, ahoji kuhusu redio kujadili michezo asubuhi

Habari za siasa hakuna muandishi wa kuchambua makala za siasa,technology. Ukisikiliza wanapojadili machafuko ya DRC unaona wamesoma mtandaoni na wanakosea mpaka kutafsiri.
 
Hiyo yote inatokana na ushindani lakini pia Kuna jamaa wanaitwa Ipsosy Hawa wanatoa taarifa zao ndio hupelekea hizo redio kuigana na kuwa na vipindi km hivyo
Hii angle sijawahi ifikiria kabisa, usikute agenda za watu za social engineering zinaingizwa humo humo ; Moira it has become too much
Timu zile zile zinazingua miaka nenda rudi lakini watu hawachoki kubishana
 
Aache mambo ya kizee au mnasemaje vijana?
 
Utani watu wanaojua nchi hii kwa sasa kila mahali hadi bungeni ni mpira tu!
 
Kwani mkuu kabla ya kushamili kwa vipindi vya michezo kwenye maredio nchi ilikuwa na maendeleo gani?
Maana vipindi vya michezo vilishamili kipindi cha jiwe baada ya kubana uhuru wa kujieleza na kuongelea siasa.
Tuachage visingizio vya kipumbavu umasikini wa waafrika uko kwenye damu.
 
Na michezo ya bahati na sibu (Kuchezesha droo)

Mambo yamebadilika sana.
Siku hizi nikidamka natune TBC Taifa namsikiliza Hayati Baba wa Taifa.
Najaribu kupata taste ya kipindi cha nyuma.
 
Kufuatilia michezo kwa vijana ni anguko kubwa sana kiuchumi kwasababu michezo hiyo katika kusikiliza vinaenda sambamba na kubeti, kunywa pombe Kali namengine mengi yanayoendana na hayo yasiyo na tija kwa taifa
 
Mpira sio vitu vya maana ?
Unajua ni maelfu ya watz wangapi wanajipatia kipato kutokana na huo mpira?
Unaongelea wamachinga wa kariakoo wanaouza jezi kutokana China?
 
Nina maoni tofauti, Hizo redio zipo kibiashara zaidi kwa hiyo zinaangalia kwenye maslahi na wapi wanapata matangazo
Kama wewe hupendi kusikiliza michezo zipo redio asubuhi tu huzungumzia siasa,dini,kilimo nakadhalika
Kwa hiyo chaguo ni lako
hii ni hoja mfu kabisa haina weledi ndani yake
 
Nina maoni tofauti, Hizo redio zipo kibiashara zaidi kwa hiyo zinaangalia kwenye maslahi na wapi wanapata matangazo
Kama wewe hupendi kusikiliza michezo zipo redio asubuhi tu huzungumzia siasa,dini,kilimo nakadhalika
Kwa hiyo chaguo ni lako
UJAINGIZWA KWENYE MFUMO WA MLETA MADA,,,,UPO VIZURIšŸ¤
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…