Mwanza: Baa ya The Cask yafungwa kwa tuhuma za ukwepaji kodi

Mwanza: Baa ya The Cask yafungwa kwa tuhuma za ukwepaji kodi

Serikali wilayani llemela mkoani Mwanza imeifunga bar maarufu ya The Cask Bar & Grill jijini Mwanza kwa tuhuma za ukwepaji kodi kwa kipindi cha miaka miwili.

Kwa mjibu wa Mkurugenzi wa manispaa ya llemela Kiomono Kibamba, amesema uongozi wa bar hiyo umekwapa kodi ya Serikali na kuendesha biashara zaidi ya moja eneo hilo hilo.

Akizungumza katika eneo hilo la Bar Mkurugenzi wa llemela, Kiomoni Kibamba amesema mmiliki wake amekiuka masharti ya uendeshaji wa biasharaikiwemo kukosa leseni ya biashara kwa kipindi cha miaka miwili.

Pia soma:
- Imekuwaje The Cask Bar waombe radhi kwa wateja wao kuwa na ujumbe wa kuokoa bandari
Hili lina mkono wa DiPiWeldi....

Mark my words...
 
Hata Bar wamewekeza wageni? Hii ni nchi au jalala?

Labda iwe kama sijakuelewa, maana uandishi wako ni wa shida kidogo. Unazunguka zunguka na jambo lililo rahisi kueleza, sijui kwa sababu zipi!
 
OKOA BANDARI DPWORLD
Dah!

Kumbe?

Sasa watu humu wanazungukazunguka na visababu, kumbe sababu yenyewe ipo wazi hapa!

Sasa sijui CHADEMA hili limewaingia vipi, maanake ni wahusika wakubwa wa mkasa huu.

Kunyamazia tu haitoshi. Haya ni baadhi ya mambo yasiyofaa kabisa kutokea ndani ya nchi.
 
Mkurugenzi wa Ilemela amejitoa kafara kwa kukiuka maelekezo ya Rais kwamba biashara zisifungwe; huyu mkurugenzi ni moja ya watu wanaoishi katika utawala uliopita. Kukiuka kauli ya mwenye nchi ni dharau na natabiri soon anatumbuliwa.
Huyu Mama sio tumbua tumbua ovyo!, utasubiri sana!. Sasa tuko kwenye era ya reasoning and logic!
P
 
Ok.Hivi hilo jina "cask" mwenye baa alimaanisha nini? It sounds hideous!Ni kama kifupi cha casket.Yaani jeneza.[emoji848]

IMG_0132.jpg
 
Dah!

Kumbe?

Sasa watu humu wanazungukazunguka na visababu, kumbe sababu yenyewe ipo wazi hapa!

Sasa sijui CHADEMA hili limewaingia vipi, maanake ni wahusika wakubwa wa mkasa huu.

Kunyamazia tu haitoshi. Haya ni baadhi ya mambo yasiyofaa kabisa kutokea ndani ya nchi.
Huyo mwenye hiyo bar hana akili au anajuwa anachokifanya.
 
Back
Top Bottom