Mwanza inapokea 10% tu ya mizigo kutoka Dar huku Kigoma ikipokea 41% ya mizigo. SGR ya Mwanza ni White Elephant project

Mbona husemi bwana Ladogosa amejibuje hilo, unakuja na maoni ya upande mmoja?
Ndiyo maana ya mjadala...

Kama na wewe ulifuatilia mjadala huo, ungeweza kusema tu kuwa, hata hivyo DG wa TRC ktk kulitolea ufafanuzi hilo, amejibu hivi na vile...

Anyway vyovyote iwavyo...

Wote tunajua kuwa mpango ni kujenga reli ya SGR kwenda hadi huko Kigoma...

Kinachogomba hapa ni vipaumbele (priorities). Kwamba, tunajua kama kweli tutasambaza SGR nchi nzima, basi itatuchukua miaka hata 30 ijayo kukamilisha project hii...

Jambo muhimu ilikuwa tuanze kujenga kuelekea wapi ili tuanze kuvuna faida haraka...

Ni ujinga kuanza kuelekeza reli ya SGR utakayoijenga kwa awamu kadhaa na kuchukua miaka 30 kuikamilisha awamu zote, kwenye eneo ambalo mahitaji yake ya usafirishaji mizigo ni 10% badala ya kuanza na eneo ambalo linasafirisha mizigo 41% kuelekea huko...!!
 
Mkuu, kuna sababu zake za kujenga hii reli katika vipande vipande namna hiyo.

Ujenzi wa Mwanza - Isaka hauwezi kuishia hapo na kubaki bila kutumika. Maana yake ni kwamba Makutopora hadi Isaka ni lazima ijengwe kwa kuhimizwa na hiyo iliyojengwa tayari toka Mwanza hadi Isaka.

Hakuna kichaa yeyote atakayeingilia ujenzi wa vipande hivyo viwili; hakuna atakayekubali hasara hiyo.

Unaona ya sasa hivi, toka Pugu hadi Morogoro inakamilika, hata kabla ya kipande cha Dar Stesheni hadi Pugu. Haitawezekana hicho kipande kisijengwe hadi Pugu.
 
Hujui kitu unabaki unacheka cheka
 
Mkuu, umeeleza vizuri sana, lakini kutokana na mada ilivyowasilishwa sidhani kwamba mleta mada ataelewa ulichoeleza hapa.

Isaka itakuwa ni Bandari.

Wote wanaokwenda kuchukuwa mizigo Dar hawana sababu tena ya kwenda huko. Hata hiyo 41% anayodai mleta hoja, sehemu kubwa itakuja hapo. Rwanda, Burundi, eneo kubwa la DRC , mashariki hadi kaskazini, na Uganda, hiyo itakuwa ni bandari yao ya kuchukulia mizigo.

Mizigo inayosafirishwa toka Mombasa, kupitia Uganda na kupelekwa DRC; ya nini usumbufu wote huo kama mtu anakwenda Isaka na kubeba mizigo yake?

Tushindwe tu sisi wenyewe kuendesha Bandari zetu, za Dar na hiyo Isaka kwa ufanisi, vinginevyo Mombasa watalizwa.

Lakini bado atakuwa haelewi!
 

Mtaalamu wa uchumi Bw. Walter Nguma azungumzia faida je SGR Reli ianze Kigoma au Mwanza ?
 
Wewe akili yako ni matope tu. Upeleke sgr kigoma uache kanda ya ziwa ? Rudi tena darasani.
 
Miradi ya kipuuzi na isiyo na tija kama hii hata kwa wanaoishabikia sio ya kuipelekea pesa.

Hivi huko serikalini kuna watu kweli wanaofikiria? Yaani baada ya kukamilika waanze tena kutuongezea kodi eti kulipia kujiendesha? Huu ni wehu
BBC ndio mtaa gani kwanza tuanzie hapo. Nchi HII hatuongozwi na uzandiki wa BBC.
 
Mabandiko yako yote huwa ya kipumbavu tu. Huna lolote endelea kuota ndoto huku miradi ya daraja la Busisi, sgr ikikamilishwa. Ama sivyo kajinyonge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…