Mwanza inapokea 10% tu ya mizigo kutoka Dar huku Kigoma ikipokea 41% ya mizigo. SGR ya Mwanza ni White Elephant project

Mwanza inapokea 10% tu ya mizigo kutoka Dar huku Kigoma ikipokea 41% ya mizigo. SGR ya Mwanza ni White Elephant project

Tungeomba watu waje na data zinazoonyesha mizigo ya ndani toka Mwanza ni ipi hasa ukilinganisha na Kigoma. Pili je unafikiri kufikiria nchi za nje/majirani ni kosa? Ukiwa mchumi huwezi kuacha kufikiria nchi jirani ili uweze kuendesha reli yako ya umeme. Tulisitazame kikanda tulitazame kiuchumi zaidi.
 
Nadhani mimi na wewe sote nia yetu nzuri katika hili na hoja kutofautiana mimi napenda tu. Nilivyosema mizigo ya Congo waje wachukulie Isaka sikuwa na maana gari zitatoka Congo hapana ni kama tungejenga reli mpaka Kigoma SGR kwa hoja uliyotoa kuwa 41% mizigo inaenda Congo kupitia Kigoma haina tofauti na kuchukuwa Isaka kwa maana haya malory yangefanya route fupi kutoka Isaka mpaka Kigoma halafu hapo usafiri wa majini. hata SGR inegefika Kigoma ni bado usafiri wa majini ungetumika.
Unasema magari yaje Isaka kubeba mizigo ya Kongo, kisha iipeleke Bandari ya Kigoma kupakiwa kwenye Meli kwenda Kongo.
Hii inaingia akilini?
Pale Kigoma, Stesheni ya Treni iko Bandarini.
Mzigo unapakuliwa kutoka kwenye Treni na kuingizwa kwenye Meli.
 
Ubinafsi wa utawala uliopita ndio tatizo, yule mtawala alikuwa mbinafsi mno bila kungalia maslahi mapana ya Kitaifa!
 
Baada ya kilimo cha Pamba kufifia, na Wafugaji wa Ng'ombe kuhamia Mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Mbeya baada ya kukosa malisho kutokana na Uharibifu mkubwa sana wa Mazingira, mchango wa Kanda ya Ziwa katika Uchumi wa TZ ni mdogo.
Kilichobakia huko ni Dhahabu ambayo HAISAFIRISHWI KWA TRENI.
Ujenzi wa SGR kwenda Mwanza ulichochewa na kukosa uzalendo na ukabila, kwa Kisukuma "primitive nonsense", kwa maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Msikie huyu na data sijui za wap. Hiv kagera si ipo Kanda ya ziwa? Eti eh

Kagera inadhalisha karibu asilimia 80 ya kahawa yote nchini.

Na ukifuatilia zao Hilo ni moja ya too nchini kuingiza kipato

Na bado 70 percentage ya ndizi zote hutoka kagera
Screenshot_20210622-152326.jpg
 
Mkuu naomba kuuliza hio mizigo inayoenda kigoma ambayo haina meli za mizigo( juzi mama samia katoka ku sign mkataba wa ujenzi wa meli ya kwanza ya mizigo kigoma yenye uwezo wa kubeba tani 2800), meli za abiria zimekufa na bandari iliyokufa hua inavukaje kwenda kongo?Asante
SGR ikielekezwa huko itafufuka😆
 
Msikie huyu na data sijui za wap. Hiv kagera si ipo Kanda ya ziwa? Eti eh

Kagera inadhalisha karibu asilimia 80 ya kahawa yote nchini.

Na ukifuatilia zao Hilo ni moja ya too nchini kuingiza kipato

Na bado 70 percentage ya ndizi zote hutoka kageraView attachment 1828375
Kwa Mwendazake, Kagera haijawahi kuwa sehemu ya Kanda ya Ziwa. Wala Mara.
Ndiyo sababu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa haupo Musoma, upo Chato!
 
Unasema magari yaje Isaka kubeba mizigo ya Kongo, kisha iipeleke Bandari ya Kigoma kupakiwa kwenye Meli kwenda Kongo.
Hii inaingia akilini?
Pale Kigoma, Stesheni ya Treni iko Bandarini.
Mzigo unapakuliwa kutoka kwenye Treni na kuingizwa kwenye Meli.
Hivi hujiulizi kwanini kama Kigoma muhimu kiasi hicho mpaka leo hawana barabara ya lami? sasa hiyo asilimia 41 ya mizigo si wanachukulia Dar sasa Isaka sio kwamba nafuu kwako kuliko Dar. SGR haiwezi kujengwa kwa kutegemea mizigo ya Congo tu Mwanza mizigo inaenda na kwenda Dar inachangia 25% ya pato nchi nzima sio Kigoma.
 
Kwa Mwendazake, Kagera haijawahi kuwa sehemu ya Kanda ya Ziwa. Wala Mara.
Ndiyo sababu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa haupo Musoma, upo Chato!
Hiv wangejenga huo uwanja w chato maeneo ya kajunguti huko misenyi bukoba Kama ilivyopanga awali wasingepata hasara hiz . Kule ni karibu na kilimo cha kahawa inayozalishwa 80 percentage,ndizi, vanilla na miwa nikimaanisha kagera sugar. Halafu ule uwanja ukawa wa ndege za mizigo kupeleka ulaya Kama walivyo huko uganda
 
Kigoma port:
2014-15 ilihudumia Tani 99,336 mapato 2B
2015-16 ilihudumia Tani 137,570 mapato 2.7 bilioni
2016-17 ilihudumia Tani 136,573 mapato bilioni 4.14
2017-18 ilihudumia Tani 196,844 mapato bilioni 6.75
2018-19 expected Tani 200,500 expect 10% more than kilichopatikana 2017-18.

Source Manager wa Bandari ya kigoma akihojiwa na Global Tv
 
Wakuu mnogage.

Kwa mujibu wa BBC ikimhoji mtaalam wa Uchumi imebainika kwamba mzigo unaoingia bandari ya Dar es Salaam kuelekea Nchi za jirani via Central corridor ni asilimia 10% tu ya mzigo huo unaelekea bandari ya Mwanza wakati asilimia 41% huelekea bandari ya Kigoma.

Cha kushangaza imekuaje reli ya SGR ijengwe kuelekea Mwanza? Wananchi wa nchi hii tunazidi kubebeshwa mizigo ya misumari Kisa maamuzi ya kisiasa.Mpaka hapo tunazika pesa na kuzalisha white elephant project,very sad.
Huwezi anzisha mradi wa kitaifa kwa ajiri ya Nchi jirani aisee....mizigo inayokwenda kigoma inaingia bandarini na kuvuka border na Ile ya mwanza inaishia mwanza na kanda yote kapata mahitaji yao.

Sent from my PIC-LX9 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom