Mwanza inapokea 10% tu ya mizigo kutoka Dar huku Kigoma ikipokea 41% ya mizigo. SGR ya Mwanza ni White Elephant project

Tungeomba watu waje na data zinazoonyesha mizigo ya ndani toka Mwanza ni ipi hasa ukilinganisha na Kigoma. Pili je unafikiri kufikiria nchi za nje/majirani ni kosa? Ukiwa mchumi huwezi kuacha kufikiria nchi jirani ili uweze kuendesha reli yako ya umeme. Tulisitazame kikanda tulitazame kiuchumi zaidi.
 
Unasema magari yaje Isaka kubeba mizigo ya Kongo, kisha iipeleke Bandari ya Kigoma kupakiwa kwenye Meli kwenda Kongo.
Hii inaingia akilini?
Pale Kigoma, Stesheni ya Treni iko Bandarini.
Mzigo unapakuliwa kutoka kwenye Treni na kuingizwa kwenye Meli.
 
Ubinafsi wa utawala uliopita ndio tatizo, yule mtawala alikuwa mbinafsi mno bila kungalia maslahi mapana ya Kitaifa!
 
Sema lengo lako SGR iwafikie Waha wapenda treni ili waitumie kwa usafiri kwenda Dathramu, hapo kwenye mizigo unazunguka tu.
 
Msikie huyu na data sijui za wap. Hiv kagera si ipo Kanda ya ziwa? Eti eh

Kagera inadhalisha karibu asilimia 80 ya kahawa yote nchini.

Na ukifuatilia zao Hilo ni moja ya too nchini kuingiza kipato

Na bado 70 percentage ya ndizi zote hutoka kagera
 
SGR ikielekezwa huko itafufuka😆
 
Kwa Mwendazake, Kagera haijawahi kuwa sehemu ya Kanda ya Ziwa. Wala Mara.
Ndiyo sababu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa haupo Musoma, upo Chato!
 
Unasema magari yaje Isaka kubeba mizigo ya Kongo, kisha iipeleke Bandari ya Kigoma kupakiwa kwenye Meli kwenda Kongo.
Hii inaingia akilini?
Pale Kigoma, Stesheni ya Treni iko Bandarini.
Mzigo unapakuliwa kutoka kwenye Treni na kuingizwa kwenye Meli.
Hivi hujiulizi kwanini kama Kigoma muhimu kiasi hicho mpaka leo hawana barabara ya lami? sasa hiyo asilimia 41 ya mizigo si wanachukulia Dar sasa Isaka sio kwamba nafuu kwako kuliko Dar. SGR haiwezi kujengwa kwa kutegemea mizigo ya Congo tu Mwanza mizigo inaenda na kwenda Dar inachangia 25% ya pato nchi nzima sio Kigoma.
 
Kwa Mwendazake, Kagera haijawahi kuwa sehemu ya Kanda ya Ziwa. Wala Mara.
Ndiyo sababu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa haupo Musoma, upo Chato!
Hiv wangejenga huo uwanja w chato maeneo ya kajunguti huko misenyi bukoba Kama ilivyopanga awali wasingepata hasara hiz . Kule ni karibu na kilimo cha kahawa inayozalishwa 80 percentage,ndizi, vanilla na miwa nikimaanisha kagera sugar. Halafu ule uwanja ukawa wa ndege za mizigo kupeleka ulaya Kama walivyo huko uganda
 
Kigoma port:
2014-15 ilihudumia Tani 99,336 mapato 2B
2015-16 ilihudumia Tani 137,570 mapato 2.7 bilioni
2016-17 ilihudumia Tani 136,573 mapato bilioni 4.14
2017-18 ilihudumia Tani 196,844 mapato bilioni 6.75
2018-19 expected Tani 200,500 expect 10% more than kilichopatikana 2017-18.

Source Manager wa Bandari ya kigoma akihojiwa na Global Tv
 
Iko hivi mleta mada ni mtu wa kaskazini, huwa ana chuki na wivu na kanda ya ziwa na watu wake hasa wasukuma, nina mjua kupitia nyuzi nyingi huwa anapondea sana waskuma. Kwa hiyo ni mwendelezo wa wivu wa jamaa kwa MWANZA.
 
Huwezi anzisha mradi wa kitaifa kwa ajiri ya Nchi jirani aisee....mizigo inayokwenda kigoma inaingia bandarini na kuvuka border na Ile ya mwanza inaishia mwanza na kanda yote kapata mahitaji yao.

Sent from my PIC-LX9 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…