Mwanza: Mmiliki wa mabasi ya J4 aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa aachiwa huru

Kwa spidi hii ya bwana DPP tegemea yule Mende wa gesi ya mkopo kurudi uraiani January mwakani.

Hivi rushwa wanapokea pesa taslim au benki transfer?
Hizi Rushwa ni sawa na intercontinental ballistic missiles.

Ni za Benki
 
Unaongea tu
 
Muuaji mwingine ni dikteta Putin[emoji16]
Acha ujinga wako, haijalishi nyuma ya mauaji Kuna sababu zipi.

Kuua ni kuua tu .... Kwahiyo siku hizi, mtu akikutendea baya, ni Kuua tu, kwakua nyuma yake una sababu?.
 
Aachiwe tu, hao wanafamilia wachukue kampunga, maisha yaendelee, mtu kaajiri mamia ya watu akae jela kufanya nini? Mtaani yamejaa majitu kama Mdude yanajaza nafasi tu
 
Aachiwe tu, hao wanafamilia wachukue kampunga, maisha yaendelee, mtu kaajiri mamia ya watu akae jela kufanya nini? Mtaani yamejaa majitu kama Mdude yanajaza nafasi tu
Akili za UVCCM hizi.
 
Nimekuuliza sio ugomvi !! Wangapi wanaachiwa ? Kuna mengi mzee na kuwekwa jela kwa mda ni kama sheria hata ukiua jambazi unaweza kushikiliwa kwa muda then ndo unaachiwa.

Fuatilia sana hizo mambo wengine majambazi.
Bush lawyer advise.. tikiti maji
 
We mwalimu usitake udharaurike bure.

Mahakamani ni ushahidi usio na mashaka, ukikosea Mahakama ya Rufaa inamuachia mtu
Sijaelewa katika habari ya mtoa hoja, ameachiliwa na mahakama ya rufaa au Dpp kaondoa shauri hilo mahakamani?
 
Inatia hasira uchungu ila mwisho wa Siku Mungu mwema mwisho wao utakuwa mbaya sana kama si wao watoto wao
 
Wekeni hukumu hapa tuone ni mazingira gani jamaa kachomoa pini. Inatokea kabisa mzee mmoja aliachiwa huru baada ya kumchapa shaba askari polisi aliekuja mkamata usiku nyumbani kwake amelala na mke wake. Mzee akawaambia polisi wasithubutu kugusa geti, jamaa wakazama ndani kibabe. Akawachapa risasi mmoja akakata moto pale pale.
Mzee alikomaa kwamba hawakuwa polisi ila majambazi,jamhuri inakazania ni polisi,mzee alipigwa kifungo cha maisha badae akachomoa pini huko huko kwa pilato kwa rufaa. Japo mzee alijua kweli ni askari ila akaamua kuwachapa shaba kibabe!
 
Upande wa utetezi mtuhumiwa alitetewa na Wakili Msomi Peter Kibatala.

Kuna watu huwa wanabeza uwezo wa Kibatala kuwa hashindi kesi huyu jamaa ni moto
Kibatala ni Wakili wa Mchongo,anajua kupenyeza rupia Mahakamani,Kama huna pesa hawezi shinda kesi yako!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…