Mwanza: Yaliyojiri Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA baada ya kuondolewa zuio la mikutano

Sisi washauri huru tuliwashauri siku nyingi, angalia ushauri wangu huu wa 2010 https://www.jamiiforums.com/threads/ccm-imechokwa-chadema-haijajipanga.87532/ humo nilisema
leo ni 13 years baada ya ushauri huu, Chadema bado inategemea mikutano ya hadhara!, haina media yake!. Haipo kwenye grassroots, halafu watu wanawaza kuingia Ikulu 2025!.
Hili la urais wa 2025, nimeisha washauri!. https://www.jamiiforums.com/threads...weli-iachane-na-2025-lengo-liwe-2030.2057813/
p
 
Upinzani (hasa Cdm) kwa sasa wanategemea hisani ya Ccm ili kufanya siasa, alafu bado tunaamini kuna upinzani hapa nchini ?... Mzaha huu...

Hakuna haki za kikatiba tena, demokrasia yetu ya kiini macho hatimaye imetekwa hadharani...

JokaKuu Pascal Mayalla Kiranga denooJ
 
Safi sana,habar zifike kuzimu kwa yule mjinga aliyesema kuwa ataiua Chadema!
 
Hoja ya kuandaa mrithi wa Mbowe ni hoja muhimu!, ila wakati sio ndio huu!, this is long overdue!. Thanks God ndani ya Chadema, kuna able man mmoja tuu!, the one and only, Heche!.
P
Hiki kinachoendelea kitatusaidia kupata uelekeo mpya wa siasa za upinzani. Mbowe amefanya kazi kubwa sana lakini kila jambo lina ukomo wake. Amuachie chama Lissu ajipange na safu yake mpya.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Umeongea vema kwa muono huo wa kwako. Lakini tunaweza kujiuliza swali kubwa zaidi ili tuwezw kupata picha kubwa zaidi ya tofauti katika mitizamo yetu.

● Je matarajio mengi kama unavyosema ya wanachadema yalikuwa yapi?...je matamanio hayo kwa nini wanachadema humkuyatekeleza ndani ya miaka saba namnadhani Leo mnaweza kuyatekeleza baada ya juhudi za mwenyekiti kuweka mazingira na kufanikiwa kuweka uwanja wa ninyi kufanya yale mtakayopenda kuyafanya?

● Nini kimefanyika wakati hakuna maridhiano ndani ya miaka saba ya kiza kwa siasa za majukwaani?

● Hawa watanzanio unaowasemea kwamba hawataki Maridhiano wanataka njia gani ambayo waliweza kuifanya wakati wa awamu iliyopita na hii iliyopo?

● Mariadhiano si utapeli. Ni uungwana wa watu waliostaarabika kuamua kuchagua njia ya kiuungwana kupambana. Kuyafananisha Maridhiano ya Seif kule Zanzibar na CCM na maridhiano haya yaliyotupa uhuru wa mikutano ni kuikosea fursa iliyopo katika kukuza chama.

● Kwamba ni bora kutokuwa na maridhiano?...fine yasiwepo. Je tumefaidika nini na tmepoteza nini wakati wa nje ya makubaliano?


Nadhani CHADEMA mngetulia kidogo. Mjipange namna ya kuenenda ili kuongeza wanachama na kushinda chaguzi zijazo. Hii ya kuona Mwenyekiti wenu hana nia njema na Chama ambacho amekijua na kukijenga toka ujana mpaka uzee wake huu haitawasaidia.

Mpeni nafasi kama ambavyo mlimpa nafasi ya kuendelea na mazungumzo ya maridhiano na mwisho mkapata mlichopata. Kama kunamapungufu na hofu zenu juu ya mwenendo wake (kama ambavyo amekiri kwamba mna haki na mko sawa kabisa kufikiria namna mnavyofikiri) myamalize ndani ya chama.

Na wanachama muwe na akiba ya maneno. Mwanasiasa mzuri ni yule anayebakiza maneno yake. Hayasemi yote. Mdude Chadema alikuwa anapibga wazi wazi juu ya mazungumzo ya Mwenyekiti wenu na CCM ila Leo ndio wa kwanza kujjaribu suti ambazo anaamini atazivaa baada ya kushinda ubunge katika mazingira aliyoyatengeneza Mbowe kwenye Mazungumzo na Mh. Rais!

Vumilianeni Kiongozi. Ila kuweni makini kwa kuhoji kupitia vikao vya chama. Mtatutikisa kidogo CCM ila tutawashinda si kwa sababu ya Mbowe kwamba kachoka, ni kwa sababu CCM tunanarithishana itikadi kwa wazazi kwa watoto ha ha ha ha
 
Tuna
Walaumu CHADEMA sisi wananchi tunanafasi ipi ya kufanya yafanyike?.

CHADEMA walidai haki hizo za kikatiba, wakaitisha maandamano ambayo ni haki ya kikatiba, wananchi hamkutokea wala kuunga mkono!

Leo mnakuja hapa na kuuponda upinzani?....mlitaka wafanye nini?

Umesahau kuwa nguvu za mamlaka za kuongoza nchi ni za wananchi?
 
Mkianza hoja za nani awe nani ndani ya chama na si chama kifanye nini na nini ili kushika dola mtakiua chama!

Huu si wakati wake. Hata sisi CCM ambao tuna dolea na serikali hatuwazi kwa namna hii ya hovyo!
Hoja ya kuandaa mrithi wa Mbowe ni hoja muhimu!, ila wakati sio ndio huu!, this is long overdue!. Thanks God ndani ya Chadema, kuna able man mmoja tuu!, the one and only, Heche!.
P
 
Mkianza hoja za nani awe nani ndani ya chama na si chama kifanye nini na nini ili kushika dola mtakiua chama!

Huu si wakati wake. Hata sisi CCM ambao tuna dolea na serikali hatuwazi kwa namna hii ya hovyo!

Mkuu imebidi nicheke, kuwa hata nyie CCM hamuwazi hivyo, kwani nani anawaiga nyie CCM? Yaani hakuna chama nakidharau kama hicho, kiasi huwa nashangaa eti kuna watu wanasema wanajifunza kupitia CCM!
 

Sipingi usemacho Boss. Ila narudia tena, hayo maridhiano ni utapeli kama utapeli mwingine. Ni bora kutokufanya Siasa kuliko kufanya siasa kwa uratibu wa CCM.

Na kuhusu CCM kushinda uchaguzi sio kwasababu mna uwezo wa kushinda, bali mfumo uliopo na katiba hii ndio inawapa nafasi hiyo. inshort hakuna uchaguzi hapa Tanzania, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Uchaguzi upo Kenya boss.
 
Ile siku Mama anaruhusu mikutano ya hadhara, wote waliokuwa ukumbini walishangilia na baada ya hapo wanapigwa beche!.

Mimi nilimshukuru pia ila sikuishia kwenye kushukuru tuu kitutusa, nilimshukuru na kuzungumzia need to put a mechanism in place kuzuia viongozi wetu wasizigeuze haki zetu as favours, haki ni rights, ni stahili stahiki na sio hisani, huruma au favours za rais aliyeko madarakani!.
P
 
Kuna ka clip kapo kule kwa Kigogo kana dakika 1 na sek 25, yani nmekadawload nimeweka kwenye flash kabisa kila saa nakasikiliza!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna ka clip kapo kule kwa Kigogo kana dakika 1 na sek 25, yani nmekadawload nimeweka kwenye flash kabisa kila saa nakasikiliza!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ni haki yako kusikiliza, tena na vile umekapata kwa kigogo sio kakudelete kabisa. Inaonekana ww ni mzee, ndio maana umeona ukisema umekapata kwa kigogo itaonekana na ww unaenda na wakati,,😂😂
 

..kufanya siasa ni HAKI ya KIKATIBA Watanzania.

..Nadhani ume-conclude kwamba CCM wamepoka au wamepora haki hiyo ya Watanzania.

..Katika mazingira hayo sikutegemea uvilaumu vyama vya upinzani. Nilitegemea uilaumu CCM kwa kuvunja katiba na sheria.

..Kuvilaumu vyama vya upinzani ni sawa na kumlaumu binti aliyebakwa, badala ya kumlaani aliyebaka.

..Upinzani Tanzania upo, isipokuwa ni upinzani unaodai haki kwa njia za AMANI.

..Wapo baadhi yetu ambao wanatamani wapinzani wawalazimishe CCM kufuata Katiba, lakini tukubaliane kwamba Tanzania hakuna wapinzani wa aina hiyo.
 
Kuna ka clip kapo kule kwa Kigogo kana dakika 1 na sek 25, yani nmekadawload nimeweka kwenye flash kabisa kila saa nakasikiliza!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
WALAU LEO UMEPATA CHA KUANDIKA ,HUENDS UKALIPWA MAANA SIKU ZILIKUWA ZIMEPITA NJAA INGEKUWA BILA UCHAWA NA UMALAYA WA KISIASA HUWEZI KUISHI.
 
Makamanda hatuipendi CCM maana ilishakuwa na moyo wa kifedhuli.

WanaCCM wana roho mbaya kama mbwa mwitu aliye ndani ya kundi la kondoo.

Leo hii wazazi wanashindwa hata kupeleka watoto shule kwa kukosa pesa ya sare za shule. Kaya zinashindwa hata kula milo miwili kwa siku.

Kundi moja tu la wanaCCM wanatafuna mali za umma kwa ujanjaujanja na ujuaji.

Alafu mwenyekiti wa chama chetu anakiri hadharani kuwa yeye yupo na hilo kundi la wanaCCM.

Makamanda tumeumia sana ila hatuna cha kufanya. Mbowe anaiona Chadema kama mali yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…