Mwanza: Yaliyojiri Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA baada ya kuondolewa zuio la mikutano

Mwanza: Yaliyojiri Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA baada ya kuondolewa zuio la mikutano

Alichohutubia Mbowe kinaonyesha ukomavu wa kisiasa KWA vyama vya UPINZANI nchini!

Huwezi kushika DOLA kama siyo rafiki KWA wenye DOLA!

Lakini angependekeza nini Serikali ifanye KWA wananchi kutokana na hali iliyopo kimaisha!kama mfumuko wa bei!!!

Yaani"Chadema tunataka serikali ifanye hivi au vile kuhusu wananchi KWA maana Hali ya maisha KWA WANANCHI imekuwa ngumu:-

1.........



2..........



3..........

Hapo ingekuwa Safi!

Labda tutarajie hayo WAKATI ujao!!
 
Ukute anayewakagua wanafunzi kama wamekeketwa ni mtu mzima aliyekeketwa miaka mingi iliyopita. Kwani kuketa imekuwa dhambi mpaka waanze kuwakagua? Huo ni udhalilishaji kuchunguza uchi wa wanafunzi
 
Kuna watu wanaendesha propaganda mfu eti cdm ilileta wafuasi wake kwa kuwasafisha kwa malori kutoka mikoa jirani hivi hayo malori yangeruhusiwa na traffic kupita barabarani huku polisi kibao wakiwa doria jijini Mwanza na vitongoji kuangalia usalama wa mkutano !
 
Unapiga upande wa kulia. Piga Vertical kama hii

20230121_162517-jpg.2490218
Kwa
Unapiga upande wa kulia. Piga Vertical kama hii

20230121_162517-jpg.2490218
Jibu hao ni watu au sii watu na hao utasema umehudhuriwa na wengi akuna kiwango Cha idadi itakayohitajika na tambua na mkutano mwingine wataingezeka kwa maana tambua kuwa watu walishatishwa hawana uhuru
 
Acha kutuletea picha ya Horizontal. Leta picha ya vertical kama hii.
Siku hizi hamna drone?

20230121_162517-jpg.2490218
Mbona unaumia Bure ndugu wewe unashabikia ccm sidhani kama 1977 wakati ccm inazaliwa wewe ulikuwa umezaliwa au kama ulikuwa umezaliwa basi ulikuwa mchanga ukiona mtu haipendi CCM ni kwamba matendo yaliyoko ccm ni rushwa ufisadi roho mbaya na wanafiki ila opposition no full clean ukiwa mchafu huwezi kuoppose na usikute wewe unajikomba CCM ili upate teuzi kama akina sabaaya na akina makonda na jamii kama ya Jerry muro
 
wapo watu wanatamani maridhiano yasifanikiwe.
Ni kweli inasikitisha, tena wengi wao wamo ndani ya CCM. walitamani Police wapige mabomu na Mbowe na viongozi waandamizi wadhalilishwe na kuswekwa ndani maana bado wanadhani nchi ya Tanzania ni mali ya CCM.

Yes ni muda wa kumshukuru Rais though ni wajibu wake kuhakikisha haki sawa kwa wote.
 
Mnataka siasa za vita?
Yaani walitaka mbowe atowe matusi Kwa rais mkivu kama samia ni mweelewa mlitarajia afanye maovu kama mtangulizi wake mama kakubali maridhiano karuhusu uhuru wa mikutano ulitaka asipongezwe Mimi siyo ccm ila mwenyekiti anajitahidi kuondoa madoadoa kati ya watanzania she is our mother na mbowe ni kati ya wenyeviti waliojaliwa hekima na busara yeye na viongozi wake wamesimama vema Hadi tumepewa uhuru wa mikutano
 
Una macho makali Sana mzee....
Mkuu Proved , Mbowe ni muungwana na hivyo ndivyo wafanyavyo waungwana wote, ukipendwa, pendeka!, ukibebwa, bebeka!, ukishikwa shikamana!, ukiaminiwa jiaminishe!, ukipewa, toa!, ukijua kupokea, ujue na kutoa!.
Mbowe amependwa, amemebwa, ameshikwa, ameaminiwa, amepewa, na amepokea!.
P
 
Ujumbe ulio katikati ya bandiko lako. Uki capture ujumbe lazima ucheke [emoji28]

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Mkuu MTAZAMO , humu JF, watu wenye uwezo to read in between the lines ni wachache, hivyo ukiandika kitu, hata akitokea mtu mmoja tuu akaelewa ulichoandika, hiyo ni faraja tosha na motivation to keep writing.
Thanks.
P
 
Tindo
Nadhani mgewea aiba ya Maneno kidògo juu ya hotuba ya ĺeo ya mwenyekiti Mbowe. Mngesubiri mfanye tafakuri ya kina ya siasa za majukwaani zinavyokuja namna nyingine baada ya miaka saba za kusitishwa kwake.

Wengi wenu wanasiasa mmepitia nyakati ngumu ngumu sana hasa ninyi wa upinzani mpaka badhi yenu mkaacha siasa na wengine kuwasaliti na kuunga juhudi. Umekuwa muda mgumu sana kwenu na mna mengi ya kuyasema katika majukwaa kiasi kwamba inawawia vigumu muanze na lipi.

Mkutano wa Leo abadani ulikuwa ni kuamsha na kupima nguvu yenu katika siasa za mikutano ya hadhara. Liikuwa ni jukwaa la kusemea hasa mambo makubwa mliopitia na kujaribu kuweka mambo "sawa" juu ya tuhuma za ulambishwaji asali na pia sehemu ya Mwenyekiti kama kiongozi wa hama kucheua nyongo ya kadhia aliyopitia mpaka kufikia mikutano ya hadhara kuruhusiwa tena. Nilidhani mgempa nafasi ya kusikiliza na kuyaweka katika vitendo aliysema mwenyekiti na si kumshambulia kiasi kwamba mnaona kwa kihotuba cha Leo eti amechoka na aachie nafasi kwa wengine!...yani kweli kwa hatuba ya leo mnafika amazing kubwa kama hili?

Lazima mjue kuogelea kuendana na mkono wa maji na si kupingana nao. Mueleweni mshindani wenu (ccm) na muone namna bora ya kushinda huku mkiheshimu nguvu alizonazo. Mnataka kuendelea na siasa za awamu zilizopita ambazo ziliwasambaratisha na mkaishia kuumizwa na kutendewa visivyo na hata kuporwa chaguzi na hamkuwa na kufanya?...ndio siasa hizo mnataka muendelee nazo awamu hii?

Tambueni miaka saba iezalisha wapiga kura wapya wengi tu ambao wanahitaji hoja na maridhiano.

Mbowe toka anaanza mchakato wa maridhiano miongoni mwenu Waachadema mlimpinga tena hadhaani na hata vikao vyake mlichukizwa navyo. Leo vimeleta matunda na mikutano ya hadhara kuruhusiwa mnamuona tena hafai lakini matokeo ya kazi zake mnaona zinfandel!

Jipeni muda. Mikutano ya hadhara minne hadi mitano itawapa picha ya kwa nn Mbowe amesema aliyosema leo. Na matunda yake yataonekana.
CHADEMA IMARA NI CCM Mathubuti!

Nashukuru kwa bandiko lako lenye wingi wa busara, ni hivi, naheshimu mchango wa Mbowe kwa ujenzi wa CDM na demokrasia kwa ujumla wake. Ila nitakuwa najidanganya mwenyewe kusema hadi sasa Mbowe anasimamia tunachokiamini.l wafuasi wengi wa CDM. Ni bora tusifanye siasa kabisa tutapata ufumbuzi mwingine, sio huo wa maridhiano ya Mbowe.

Maridhiano na CCM ni utapeli wa mchana kweupe. Na mfano halisi upo huko Zanzibar. Maalim Seif alikiingiza chama chake kwenye muafaka fake, alichofanyiwa uchaguzi wa 2015 kila mtu aliona. Na uchaguzi wa 2020 akapigwa katafunua. Mikutano iko kihalali na sio hisani. Kiongozi mlevi wa madaraka tu ndio anaweza kuvunja sheria. Kuumizwa na kufanyiwa vitimbi na dola, sio sababu ya kukaa kwenye maridhiano ya kuwapamba CCM.
 
Kwa mlengo wa Mbowe hivi sasa nafikiri Lissu ndio wakati yupo njia panda kisiasa kuliko wakati wowote.

Hapa tumaini lililobakia ni Lissu pekee! Mkutano wa jana Mwanza badala ya kuinua hamasa za upinzani zimetatanisha watu tu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Kabisa....hata chama chake atakipeleka huko huko, Cdm waandae mrithi wa Mbowe mapema na wakati ndio huu.

Pascal Mayalla Tindo

Mbowe anapaswa kupingwa hadharani na popote pale kama tunataka kuendelea kuiona CDM. Tena ni kama wafuasi wengi wa CDM wamechelewa kujua hilo. Nimekuwa nikisema, Mbowe alistahili kukaa pembeni baada ya blunder ya kumpa Lowassa nafasi ya kugombea urais. Lakini hakutoka, kibaya zaidi akagombea uenyekiti uchaguzi uliopita!

Matokeo yake ndio haya ya kuingia maridhiano fake, na kwakuwa anajua msimamo wake ni wa maslahi yake binafsi, Imebidi aingie kwenye mkutano akiwa ameweka vitu vizito kichwani. Inshort sina imani yoyote na Mbowe, hasa tokea siku ile atoke gerezani na kwenda ikulu moja kwa moja bila kushirikisha viongozi wenzake wa CDM.
 
Chadema wamehalalisha watawala kuamua hatma ya namna ya kufanya siasa nchi hii kuwa hisani. Kwamba Mbowe anasema kuongea na CCM ni kama kutongoza demu! Seriously? Dah!

Nimeona sehemu hata mzee Mtei alimshtua anapitiliza! Seems chairman kuna mtu kashika remote ya kichwa chake.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Chadema wamehalalisha watawala kuamua hatma ya namna ya kufanya siasa nchi hii kuwa hisani. Kwamba Mbowe anasema kuongea na CCM ni kama kutongoza demu! Seriously? Dah!

Nimeona sehemu hata mzee Mtei alimshtua anapitiliza! Seems chairman kuna mtu kashika remote ya kichwa chake.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app

Alikuwa ameweka vitu vizito kichwani, maana anajua viongozi wenzake hawaamini anachokitaka, na wananchi pia. Hii ndio maana akawa anaongea lugha za kihuni. Kwa mkutano muhimu kama ule wa jana kiongozi kupanda jukwaani ukiwa umepiga vitu ni lack of seriousness. Ni juu ya wafuasi wote wa CDM wenye ni njema na chama kumpinga waziwazi. Apigwe pembeni hata kwa Mbatia formula.
 
Back
Top Bottom