Mwelekeo wa Ndoa yangu umefikia pabaya sana

Achana na mambo ya haramu mtoto wa watu umemzalisha maziwa yashalala kama ndala hutaki kumuoa ndo mgogodro ulipo then unaenda nje kuzalisha wa pili Sasa jifanye nunda kao huko nje kama hautokuja kurogwa
Dah!! Huyu sijui atamwagiwa mafuta ya,moto!?!?
 
Ambacho sijasema ni kuwa nilikutana nae akiwa na mtoto, na kibaya nilijua hilo kwa baadae sana kwa hiyo hajazalia kwangu
Hakukuambia ana mtoto? na je huoni haoni matumaini ya ndoa kwako ndio maana amekuwa na hali hiyo ya sasa maaana mpaka unaamua kuishi naye maanake hapo kabla hakuwa na taabia hizo. Mkuu mpe elimu huyo dada kama hajawahi kukucheat na baba mtoto wake wa kwanza angalia uwezekano wa kumrudisha kwenye hali yake.
Suluhisho sio kumwacha.
 
Mkuu Kwanza Mimi ni miongoni mwa wapinga mahali, sidhani Kama kutoa mahali kutaifanya ndoa yako iwe imara, nasema no!! ,Pili huyo mke wako sioni sababu ya wewe kuendelea kuwa naye kwa kigezo Cha kuhofia watoto kuteseka, yaani umekumbatia mzinga wa nyuki, nyuki wanakugonga huku unajipa matumaini ya kupata asali, hakika utaumia

Ni kweli Maisha ya ndoa yana changamoto , lakini kwa kiwango mlicho nacho hiyo sio ndoa, yaani mmesubiri kifo kiwatenganishe ili mmoja wenu awe huru na ashangilie, hii siyo ndoa. Ujue kuwa Maisha ya dunia hii ni mafupi sana, hivyo fanya lolote lakini hakikisha unayaishi kwa Raha, Kama Mama watoto wako Ni changamoto mpe likizo akajifunze, lete mke mwingine naye akizingua fukuza lete mwingine, Babu yangu alioa wanawake wanne kwa nyakati tofauti, nadhani hicho ndo kilimsaidia yeye kufa akiwa na umri wa miaka 90.Lakini kwa Maisha yako usipokuwa makini hata 60 huifikishi, hii ni utokana na kero unazozipata kwa familia yako.
 
Pili huyo mke wako sioni sababu ya wewe kuendelea kuwa naye kwa kigezo Cha kuhofia watoto kuteseka, yaani umekumbatia mzinga wa nyuki, nyuki wanakugonga huku unajipa matumaini ya kupata asali, hakika utaumia
Wrong advice!
 
Kama Mama watoto wako Ni changamoto mpe likizo akajifunze, lete mke mwingine naye akizingua fukuza lete mwingine,
Hovyo kabisa. Yani washauri ndo nyinyi!!? Alafu uwe balozi wa nyumba kumi utavunja ndoa zote.
Wacha avune alichopanda. Mke ni lazima aoe na watoto ni lazima alee.
 
Ndio kitu nafkiria ila natafta njia ambayo haitamuathiri pia ila sina tena ham ya kuishi nae nataman nimpangie safar ya kwenda kwao nimpe hata M5 then akifika ndio nimwambie apambane na maisha yake asirud tena
Afu watoto sasa mkuu?

Wana umri gani?

Sema inabidi utulize akili sana, wanawake wengi wanafanana tabia..tena unaweza kusema Bora hata huyo unayemuona kimeo

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Saf ndugu yangu nashukuru maana umepatwa na uchungu kuona mwanaume mwenzio anapata shida shkran mkuu
Huyo anakupoteza hata usimsifie...amini nakwambia[emoji848]

Wewe mtoe out huyo wife wako ongea nae kiupendo muulize shida ni nini atakwambia tu then msolve tatizo

Mwanamke kashakuzalia watoto wawili ni upendo mkubwa sana kwako mkuu, labor isn't a joke mzee baba!

Kaa nae kwanza msikilize, usije kujuta mbele nakwambia[emoji848]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Maisha hayakuridhishi ukamzalisha mtoto wa kwanza.

Maisha hayakuridhishi ukamzalisha mtoto wa pili.
 
Mi ka wewe tuu saa hii nahangaika na talaka aliyoiomba yeye lakini akabadili mtizamo et ameghairi anataka ndoa tena baada ya kunikuta mi nimekaza nataka apewe talaka yake.

Hugo mama watoto atakusumbua na ashajua uzaifu wako atakupiga tukio hilo mwenyewe utajuta huruma zako.

Nb: pengine analilia mahari kwann usimuoe kabisa???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…