Mleta mada nimemwelewa vizuri hatimaye anachotaka kujua Ni Mwamposya katokea wapi kihuduma,baba yake wa kiroho nani aliyemkuza kufikia hapo na elimu yake ya theolojia alusoma wapi na aliwekwa wakfu na nani kuwa na huduma hiyo
Nijibu miswali hiyo ya kidini ya kifarisayo kama ifuatavyo .Mitume waliamini sana kuwa mtu kuwa mhudumu wa Yesu lazima apitie taratibu walipitia wao!!!
Luka 9:49-50
Yohana akasema, “Bwana, tumemwona mtu akitoa pepo wachafu kwa jina lako, nasi tukamzuia, kwa sababu yeye si mmoja wetu.”50Yesu akamwambia, Msimkataze, kwa kuwa yeye ambaye si kinyume chenu yu upande wenu.
Hajapitia mivyuo yao ya theolojia wakamzuia yule hakuwemo kundi la mitume 12 walioa attend chuo cha Yesu darasani kwao hawajawahi muona au kwenye kidini chao
Yesu akasema ninyi hamumujui mimi.namjua
Ndio maana kazi ya kuweka nani awe kwenye huduma yeyote kati ya tano kazi hiyo hajakabidhi kwa kanisa hasa kabaki nayo mwenyewe mtu alyepewa na Mungu Mwenyewe rahisi kumjua kuliko aliyejipa au kupewa na dini yake kisa kasoma lichuo lao lan theolojia Kazi ya kuweka watumishi Mungu wa kweli Mungu kabaki nayo mwenyewe
Efeso 4:11-13
Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo
Waliowekwa na Mungu mwenyewe utaona matokeo na kazi zao.Yesu Mwenyewe alitamka kama hamjuamini angalieni kazi nitendazo
Kanisa lolote kama linadhani laweza pora kazi ya Mungu ya kusimika wahudumu wa kanisa hakitaweza yeye ndie huweka
Kanisa likiweka wake mbeleni lazima wataonaekana kupwaya watashangaa akina Mwamposya ambao hawakusoma mivyuo yao ya theolojia na mitaratibu yao ya kidini yao wanawapiga bao!!
Tatizo la kanisa ineonekana ni kudhani lenyewe ndio lenye mamlaka ya kuweka wahudumu wa huduma tano.Wakati Biblia inaeleza wazi kuwa hiyo ni kazi ya Mungu
Hata mitume kabla kuweka mtu huduma walifunga waliomba na kuongea na Mungu kabla kumwekea mikono mtu kuwa mhudumu huduma yeyote kati ya tani sasa hivi sifa maliza tu chuo cha Biblia au thelojia na kutimiza Vigezo vya kidini wanakupa huduma iwe upadri au huduma tano yeyote!!
Naomba nijibu kidogo ulichosema.
1. Kwanza kuhusu Luka 9:49-50, Yule mtu walimkuta anatoa pepo kwa jina la Yesu Kristo. Hilo ndilo la muhimu, alitumia Jina la Yesu Kristo kutoa mapepo na sio maji Wala mafuta. Kama wanafunzi wa Yesu wangemdaka huyo jamaa anatumia maji kuponya watu basi jibu la Yesu Kristo lingeweza kuwa tofauti.
Lazima ujue kwamba kuendelea kutumia zana za upako ni dalili za kuonesha kwamba Jina la Yesu Kristo alijitoshelezi hivyo tunalisaidia kwa kutumia chumvi au maji au mafuta.
Kuna maeneo wanatumia Hadi pipi au keki za upako. Shida ipo wapi kutumia jina la Yesu Kristo?. Kwanini usitumie jina la Yesu pekee mpaka uanze kuwambia watu wakanyage mafuta na kunyunyiza mafata kwenye majumba yao?.
Kazi ya shetani ni kulishusha jina la Yesu Kristo na kulifanya halina nguvu.
2. Pili, kuhusu Waefeso 4:11-13. Lazima uelewe zile ni huduma tano.
Mitume
Manabii
Waalimu
Wachungaji
Wainjilisti
Hizo huduma tano unapewa na Mungu sio unajipa mwenyewe. Baada ya kuokoka na ukajazwa Roho Mtakatifu Kuna huduma Mungu anakupa na wewe utaifahamu maana itakuwa ina imba ndani yako. Sasa hizi ni huduma sio vyeo au ngazi za madaraka.
Naomba nitoe mifano;
A. Kwanza mitume, mitume kazi yao kubwa ni kutembea ulimwenguni kote na kufungua kazi ya Mungu. Tena hutakiwa kwenda maeneo yaliyoshindikana au yasiyomjua Kristo Yesu. Ndio maana Paulo Kama mtume alitembea karibia dunia nzima akifungua kazi ya Bwana Hadi uarabuni. Sasa Leo tuna mitume wa vyeo sio huduma, ndio maana utakuta mtu anajiita mtume ila anasimamia kanisa. No mtume kwa huduma Hana kanisa bali anazunguka sehemu mbali mabli kufungua makanisa. Mitume wanatakiwa kwenda Somalia au Sudan au Iraq ambako injili haijafika, lakini leo ili utambulike kama mtume lazima ufanye miujiza au uponyaji basi.
B. Pili, manabii, manabii kihuduma Ni Jicho na mdomo wa Mungu. Kihuduma nabii hawezi kuchunga kanisa , Bali anaweza kuwa mshirika wa kawaida kanisani lakini mwenye uwezo wa kuona mambo ya mbele au mambo ambayo wengine hatuyaoni. Pia nabii husema Yale ambayo Mungu anataka kuonya kanisa au nchi au kundi fulani etc. Hivyo nabii kihuduma sio wa kuchunga kanisa bali kutoa mafunuo ambayo yanatoka kwa Mungu, kunifahamisha taifa yatakayokukuta mbele, kulionya taifa kuhusu dhambi na etc. Hivyo ni muhimu kuwa na huduma ya kinabii kanisani ili kanisa likomae.
Tatizo ni kwamba unabii wa Leo umekuwa ni cheo. Unabii Kama hudumu ni mchache Sana, ndio maana manabii wengi Leo hawaoni ya mbele au kkusema ya kutoka kwa Mungu ili kunenga ufalme wake. Utasikia Nabii anakuuliza unanifahamu au tunafahamian, anaanza ninakuona upo Mwanza, Mara naona jina Grace halafu watu wanachanganyikiwa. Kuna uganguzi na unabii. Uganguzi unabase kwa mwanadamu basi ila unabii ni kutoka mbinguni ili kuujenga ufalme wa Mungu duniani na kuonya kuhusu dhambi.
Niishie hapo kwa leo, ila ni muhimu kutofautisha utume na unabii wa kihuduma na utume na unabii wa kicheo.