Mwenye historia ya Nabii Mwamposa kabla ya kuanza huduma yake

Mwenye historia ya Nabii Mwamposa kabla ya kuanza huduma yake

JF,

Kwa heshima na taadhima ningependa kujua Nabii Mwamposa amefikaje fikaje hapo alipo na namna Mungu anavyoendelea kumtumia.

Nadhani ni muhimu watumishi Hawa wawe wanatuwekea historia zao ili kuweka mazingira halisi ya mahusiano yao na Mungu wetu kabla ya kufikia hatua hiyo...wengine utakuta waliishi maporini na milimali wakimtafuta.

Mungu kabla hawajafanikiwa
Huu Unabii wa Watu kunya, kukojoa, kujifungua, kutapika Kobe, Hirizi, Mjusi, Mende, panya, tandu, wadudu, Nyoka, paka kufa nje ya Nyumba ni Unabii na Utume toka Kwa Nani? Anayemtukuza Mbona hakuwahi kuwafanyia Wafuasi wake hivyo? Anyway Kizazi Cha Kulogwa, kuchawiwa, kutaka Mafanikio ya Kimwili kimepata Nabii.
 
Hao mitume hawakuibukia tu kama uyoga.

Yesu aliwachagua mwenyewe. (Vetting).

Akaaa nao kipindi chote kabla ya kupaa. ( walipitia training).

Hivyo ni muhimu sana kupata mafunzo na kukidhi vigezo vya kazi husika kabla ya kuifanya.
Si kweli
 
Huu Unabii wa Watu kunya, kukojoa, kujifungua, kutapika Kobe, Hirizi, Mjusi, Mende, panya, tandu, wadudu, Nyoka, paka kufa nje ya Nyumba ni Unabii na Utume toka Kwa Nani? Anayemtukuza Mbona hakuwahi kuwafanyia Wafuasi wake hivyo? Anyway Kizazi Cha Kulogwa, kuchawiwa, kutaka Mafanikio ya Kimwili kimepata Nabii.
Ni kwamba hawa jamaa wanahubiri jinsi ya kuitawala dunia(urafiki na dunia) wala hawafundishi kuhusu ufalme wa Mungu. Sasa sote twamjua mtawala wa dunia hii, ndicho kizazi cha manabii wake.
 
Alianza uinjilist wa kukaa na kuhubiri barabarani Mke wake akawa anaona aibu akasema tutafute kazi akasema hayupo tayari Mke wake akamtosa naye akajiwekea nadhiri kuwa hatuaacha kumtumikia Mungu hadi Ajue Mungu huyu ni nani ndiyo akampa hicho kipawa Chake..

I do not know lakini I think hadi leo hana Mke tena hata yule alipotaka kumrudi alikataaa.. A little I know though sina uhakika ready to be corrected
Anaishije bila mke?!
 
Alianza uinjilist wa kukaa na kuhubiri barabarani Mke wake akawa anaona aibu akasema tutafute kazi akasema hayupo tayari Mke wake akamtosa naye akajiwekea nadhiri kuwa hatuaacha kumtumikia Mungu hadi Ajue Mungu huyu ni nani ndiyo akampa hicho kipawa Chake..

I do not know lakini I think hadi leo hana Mke tena hata yule alipotaka kumrudi alikataaa.. A little I know though sina uhakika ready to be corrected

Kama hana mke lazima anatafuna kuondoo wake. It's just common sense
 
naomba unithibitishie ni mganga yupi wa Kienyeji ambaye amemponya mtu akajitokeza hadharani na kusema ameponywa na mganga Fulani? au unaongelea hawa wanasiasa wanaotoa kafara ya ufumbaji wa macho wapiga kura? au?

Kwa kifupi hakuna Mganga wa Kienyeji yeyote ambaye anaweza kuponya Ugonjwa .. Yeye atatibu ila hawezi kumponya.. Mwenye uwezo wa Uponyaji ni Mmoja tu naye niyule aliyempa uhai huyo mganga na huyo Mgonjwa tu ambaye Ni Mungu.
But even devil can do miracles, unakumbuka issue ya Musa na Farao? [emoji137][emoji137]‍[emoji3601]
 
Unafahamu kuwa hata shetani anaponya? Kwahiyo kufunguliwa kwa watu siyo hoja.

Je, wajua kwamba jina Yesu linatumikq hata ktk nguvu za giza? Kwahiyo kutajwa kwa jina la Yesu kisikuzubaishe.

Mwamposa mhuni Kama wahuni wengine. Umewahi kumshuhudia akishuka ama kupata gari lake? Kama bado tuulize sisi tuliyowahi kuwa waambata wake tukujuze. Unaibiwa wewe.
Tujuze sasa mbona Kama umepanic? Lete hoja yako tuone how valid it is!
 
Basi yule jamaa ni mshirikina kwa taarifa yako. Anapopanda gari baada ya ibada huwa anavua nguo zote na kubaki na boksa tu huku wapambe na walinzi wake wakiwa wamemzunguka.

Ndiyo maana ninyi waumini wake hamjawahi kumuona akipanda gari lake baada ya ibada. Uliza kila mmoja atakuambia hajawahi kumuona


Na wakati wa kushuka anapoingia ibadani huwa mikonoo yakoe inakuwa mfukoni alikoweka hirizi.
Umeonaje au kuyajua haya Kama wewe siyo mchawi?!
 
Kinaweza tumika kwa namna mbalimbali. Yesu alitemea mate udongo akampaka mtu akaona. Eliya/Elisha alimwambia mtu akaoge mto yordan mara 7. Na mafuta yamezungumziwa mara nyingi ktk biblia kuwapaka wagonjwa, wafalme n.k na hata sisi Waroman huwa tunapakwa mafuta wakati flani mapadre.

Kipawa au Karama haipo hivyo. Wewe inaongelea mafunuo. Mafunuo yanakuwa na ujumbe ndani yake. Tofautisha karama na mafunuo.

1. Kuhusu Yesu kutemea mate udongo ulikuwa ni ufunuo sio Karama ya uponyaji. Ina maana aliondoa laana ya ardhi iliyomtengeneza mwanadamu na ndio maana alipompaka yule kipofu akaona.

Mafunuo yanafanyika Mara moja tu Basi. Ndio maana humuoni Yesu akipaka watu matope. Sasa Mawamposa yeye mafunuo anafanya kila siku, huo ndio uongo wenyewe.

2. Kuhusu Elisha kumwambia Naaman akaoge Jordan ilikuwa sio Karama bali mafunuo. Ndio maana humuoni Elisha tena alimwambia mtu mwingine akaoge Jordan.

Ujumbe ni Kwamba kujiishusha na kutii kunaweza kukupa uponyaji. Naaman alikuwa jemedali wa Vita, hivyo alijua kwamba Elia akimwekea mikono atapona lakini, Elisha akampa sharti la kwenda kuoga Mto Jordan na kweli akapona.

Hivyo ni vizuri kutofautisha karama ya uponyaji na mafunuo. Karama ya uponyaji Inafanya kazi kwa jina la Yesu Kristo aliye hai lakini Mafunuo unaweza kupona bila Karama ya uponyaji, ni maelekezo kutoka kwa Mungu.

Sasa manabii wa uongo hutumia mafunuo na kulazimisha kuwa karama ya uponyaji. Nao hutumia maandiko kujustify wanachokifanya. Huwezi kuwa na Karama ya uponyaji, lakini daily ni kutumia mafuta na maji au udongo, huo unakuwa ni uchawi au uganga. Ita watu waombee kwa jina la Yesu Kristo wapone.
 
Sio mafunzo pekee ndio mwamuzi

Yuda Iskariote akiposalisiti Yesu replacement yake kanisa lilifunga na kuomba Mungu nani ashike nafasi yake

Mungu akawaambia akawaonyesha kuwa mpeni Matiya

Sasa hivi mivyuo ya theolojia mtu akidoma mivyuo ya dini yao wanamuweka kazini bila hata kuomba Mungu kuwa huyo mtu kweli Mungu kamuita ili Mungu aseme mwenyewe sababu kazi ya kuweka wahudumu hudums tano yoyote ni yake

God factor imeachwa ndio masna makanisa ulaya na marekani waliingiza hadi mishoga kanisani kuwa mapadri au wachungaji matokeo ikapigania ndoa za jinsia moja na ushoga na usagaji ikiwa na mivyeti yoye ya digrii za vyuo vya theolojia vya dini zao

Nikusahihishe kuhusu matiya, mitume walipiga kura na kura ikamwangukia matiya. Lakini kazi ya matiya haikuwa na matokeo, ndio maana Mungu mwenyewe akaamua kumleta Mtume Paulo.
 
Sio mafunzo pekee ndio mwamuzi

Yuda Iskariote akiposalisiti Yesu replacement yake kanisa lilifunga na kuomba Mungu nani ashike nafasi yake

Mungu akawaambia akawaonyesha kuwa mpeni Matiya

Sasa hivi mivyuo ya theolojia mtu akidoma mivyuo ya dini yao wanamuweka kazini bila hata kuomba Mungu kuwa huyo mtu kweli Mungu kamuita ili Mungu aseme mwenyewe sababu kazi ya kuweka wahudumu hudums tano yoyote ni yake

God factor imeachwa ndio masna makanisa ulaya na marekani waliingiza hadi mishoga kanisani kuwa mapadri au wachungaji matokeo ikapigania ndoa za jinsia moja na ushoga na usagaji ikiwa na mivyeti yoye ya digrii za vyuo vya theolojia vya dini zao

Padri yeyote anayetetea ushoga sio mtumishi wa Mungu.
 
Kuna namna mbili ya kuwapima watu ea Mungu
1. Mtazamo wa kibinadamu , ambapo kwa mtazamo huu hakuna mbinguni, dunia wala kuzimu aliekamilika mbele za watu wote.
2. Mtazamo wa Mungu: hapa unaweza pata watu waliokamilika, Mungu mwenyewe malaika na wanadam wenye kumpendeza.

Anachokifanya mwamposa sio kigeni
hata Yesu mwenyewe alikua akiongelewa hivi.


Yohana 7:45-52
[45]Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta?

[46]Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena.

[47] Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! NYINYI NANYI MMEDANGANYIKA?

[48]Ni NANI KATIKA WAKUU AMWAMINIYE, AU KATIKA MAFARISAYO?

[49] LAKINI MAKUTANO HAWA WASIOIFAHAMU TORATI WAMELAANIWA.

[50]Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao),
[52]Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya! Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.

Please usimlinganishe Yesu na Mwamposa. Tatizo mnadhani kwa sababu Yesu Kristo alifanya hivi na mimi nifanye hivyo. Yesu alifunga siku 40 bila kula Wala kunywa. Kuna binadamu anaweza hilo?. Msitumie Yesu Kristo kuhalalisha unabii wa uongo.
 
Kwanini atumie maji na mafuta?. Kwanini asikemee pepo kwa jina la Yesu Kristo. Paulo akasema alitokea mtu anahubiri injili tofauti na hii msimsikilize.
Paulo Mwenyewe alitumia leso na nguo kutoa pepo hakukeme tu kasome hapo

Matendo 19:11​

Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida; hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka.
 
Mleta mada nimemwelewa vizuri hatimaye anachotaka kujua Ni Mwamposya katokea wapi kihuduma,baba yake wa kiroho nani aliyemkuza kufikia hapo na elimu yake ya theolojia alusoma wapi na aliwekwa wakfu na nani kuwa na huduma hiyo

Nijibu miswali hiyo ya kidini ya kifarisayo kama ifuatavyo .Mitume waliamini sana kuwa mtu kuwa mhudumu wa Yesu lazima apitie taratibu walipitia wao!!!

Luka 9:49-50​

Yohana akasema, “Bwana, tumemwona mtu akitoa pepo wachafu kwa jina lako, nasi tukamzuia, kwa sababu yeye si mmoja wetu.”50Yesu akamwambia, Msimkataze, kwa kuwa yeye ambaye si kinyume chenu yu upande wenu.

Hajapitia mivyuo yao ya theolojia wakamzuia yule hakuwemo kundi la mitume 12 walioa attend chuo cha Yesu darasani kwao hawajawahi muona au kwenye kidini chao

Yesu akasema ninyi hamumujui mimi.namjua

Ndio maana kazi ya kuweka nani awe kwenye huduma yeyote kati ya tano kazi hiyo hajakabidhi kwa kanisa hasa kabaki nayo mwenyewe mtu alyepewa na Mungu Mwenyewe rahisi kumjua kuliko aliyejipa au kupewa na dini yake kisa kasoma lichuo lao lan theolojia Kazi ya kuweka watumishi Mungu wa kweli Mungu kabaki nayo mwenyewe

Efeso 4:11-13​

Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo

Waliowekwa na Mungu mwenyewe utaona matokeo na kazi zao.Yesu Mwenyewe alitamka kama hamjuamini angalieni kazi nitendazo

Kanisa lolote kama linadhani laweza pora kazi ya Mungu ya kusimika wahudumu wa kanisa hakitaweza yeye ndie huweka

Kanisa likiweka wake mbeleni lazima wataonaekana kupwaya watashangaa akina Mwamposya ambao hawakusoma mivyuo yao ya theolojia na mitaratibu yao ya kidini yao wanawapiga bao!!

Tatizo la kanisa ineonekana ni kudhani lenyewe ndio lenye mamlaka ya kuweka wahudumu wa huduma tano.Wakati Biblia inaeleza wazi kuwa hiyo ni kazi ya Mungu

Hata mitume kabla kuweka mtu huduma walifunga waliomba na kuongea na Mungu kabla kumwekea mikono mtu kuwa mhudumu huduma yeyote kati ya tani sasa hivi sifa maliza tu chuo cha Biblia au thelojia na kutimiza Vigezo vya kidini wanakupa huduma iwe upadri au huduma tano yeyote!!

Naomba nijibu kidogo ulichosema.

1. Kwanza kuhusu Luka 9:49-50, Yule mtu walimkuta anatoa pepo kwa jina la Yesu Kristo. Hilo ndilo la muhimu, alitumia Jina la Yesu Kristo kutoa mapepo na sio maji Wala mafuta. Kama wanafunzi wa Yesu wangemdaka huyo jamaa anatumia maji kuponya watu basi jibu la Yesu Kristo lingeweza kuwa tofauti.

Lazima ujue kwamba kuendelea kutumia zana za upako ni dalili za kuonesha kwamba Jina la Yesu Kristo alijitoshelezi hivyo tunalisaidia kwa kutumia chumvi au maji au mafuta.

Kuna maeneo wanatumia Hadi pipi au keki za upako. Shida ipo wapi kutumia jina la Yesu Kristo?. Kwanini usitumie jina la Yesu pekee mpaka uanze kuwambia watu wakanyage mafuta na kunyunyiza mafata kwenye majumba yao?.

Kazi ya shetani ni kulishusha jina la Yesu Kristo na kulifanya halina nguvu.

2. Pili, kuhusu Waefeso 4:11-13. Lazima uelewe zile ni huduma tano.
Mitume
Manabii
Waalimu
Wachungaji
Wainjilisti

Hizo huduma tano unapewa na Mungu sio unajipa mwenyewe. Baada ya kuokoka na ukajazwa Roho Mtakatifu Kuna huduma Mungu anakupa na wewe utaifahamu maana itakuwa ina imba ndani yako. Sasa hizi ni huduma sio vyeo au ngazi za madaraka.

Naomba nitoe mifano;

A. Kwanza mitume, mitume kazi yao kubwa ni kutembea ulimwenguni kote na kufungua kazi ya Mungu. Tena hutakiwa kwenda maeneo yaliyoshindikana au yasiyomjua Kristo Yesu. Ndio maana Paulo Kama mtume alitembea karibia dunia nzima akifungua kazi ya Bwana Hadi uarabuni. Sasa Leo tuna mitume wa vyeo sio huduma, ndio maana utakuta mtu anajiita mtume ila anasimamia kanisa. No mtume kwa huduma Hana kanisa bali anazunguka sehemu mbali mabli kufungua makanisa. Mitume wanatakiwa kwenda Somalia au Sudan au Iraq ambako injili haijafika, lakini leo ili utambulike kama mtume lazima ufanye miujiza au uponyaji basi.

B. Pili, manabii, manabii kihuduma Ni Jicho na mdomo wa Mungu. Kihuduma nabii hawezi kuchunga kanisa , Bali anaweza kuwa mshirika wa kawaida kanisani lakini mwenye uwezo wa kuona mambo ya mbele au mambo ambayo wengine hatuyaoni. Pia nabii husema Yale ambayo Mungu anataka kuonya kanisa au nchi au kundi fulani etc. Hivyo nabii kihuduma sio wa kuchunga kanisa bali kutoa mafunuo ambayo yanatoka kwa Mungu, kunifahamisha taifa yatakayokukuta mbele, kulionya taifa kuhusu dhambi na etc. Hivyo ni muhimu kuwa na huduma ya kinabii kanisani ili kanisa likomae.

Tatizo ni kwamba unabii wa Leo umekuwa ni cheo. Unabii Kama hudumu ni mchache Sana, ndio maana manabii wengi Leo hawaoni ya mbele au kkusema ya kutoka kwa Mungu ili kunenga ufalme wake. Utasikia Nabii anakuuliza unanifahamu au tunafahamian, anaanza ninakuona upo Mwanza, Mara naona jina Grace halafu watu wanachanganyikiwa. Kuna uganguzi na unabii. Uganguzi unabase kwa mwanadamu basi ila unabii ni kutoka mbinguni ili kuujenga ufalme wa Mungu duniani na kuonya kuhusu dhambi.

Niishie hapo kwa leo, ila ni muhimu kutofautisha utume na unabii wa kihuduma na utume na unabii wa kicheo.
 
Kuna shuhuda nyingi ukifatilia vizuri niza uongo tena uongo mkubwa. Na wanao zitoa wako trained kabisa kwa ajili ya hiyo kazi.

Ukiwa na akili kama za bata huwezi elewa ila ukifatilia vizuri mtiririko wa shuhuda na matukio yaliyomo utaelewa.
 
Back
Top Bottom