econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Paulo Mwenyewe alitumia leso na nguo kutoa pepo hakukeme tu kasome hapo
Matendo 19:11
Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida; hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka.
Soma vizuri Biblia, inasema Mungu akafanya kupitia mikono ya Paulo Miujiza kupita kawaida. So wameanza kwa kukupa introduction kwamba aliyekuwa anafanya miujiza sio Paulo ni Mungu. Sasa Kuna alama pale ya ;. Hiyo alama ; ni muhimu kuifahamu hiyo alama. Kwenye tafsiri ya Biblia alama ; inamaaniasha kwamba inatenganisha mstari mmoja na kuleta maana nyingine tofauti.
So walipoweka alama; kwenye mstari wa 11 Sura ya 19 wakamanisha kwamba Ina maana mahali ambapo Paulo hakuwepo basi w walichukua Lesso na Nguo za hao wagonjwa wakampelekea Paulo akaziombea ndipo wakaleta kwa hawa wagonjwa wakawekewa na kupona. Au Paulo mwenyewe aligawa lesso alizoziombea na kuwapa wakawaponyeshe wagonjwa. Kumbuka kipindi hicho watumishi walikuwa wachache ila wenye shida walikuwa wengi. Sasa Leo unakuta nabii anauzia watu Lesso yupo nao hapo kanisani kila siku.
Hivyo huo Mstari wa Matendo 19:11, haumaanishi kwamba Paulo alikuwa anaombea watu kwa kutumia lesso na nguo zake no, bali lesso zilitumika pale ambapo wagonjwa walikuwa mbali na uwepo wa Paulo. Kama Mgonjwa alikuwa karibu basi kulikuwa hakuna haja ya kutumia Lesso.