Mwenye neno lolote aniambie japo kupoza akili yangu

'Mkabidhi BWANA kazi zako na mawazo yako yatathibitika'
 
Well saidπŸ‘
 
South Africa Kama unaenda fata maisha utapata lakini Kama unaenda fata mengine utarudi maiti.
Kazi okozi kwa magraduate wengi waliokimbia south baada ya kuchoka kutembeza bahasha bongo.
Ni Kazi za ulinzi kwenye haya makampuni makubwa ili uweze isoma ramani kwanza,ukishakuwa mzoefu unabadili kazi.
Sawa na ulaya kazi ya kwanza kwa mgeni ni kubeba box ukishakuwa mwenyeji huwezi beba box kazi zipo nyingi tu.
Nenda kihalali fully documents, ogopa wabongo kaa nao mbali hata ukisikia wanaongea kiswahili.
Bora ukajichanganye na wa Kenya
 
Tatizo umebeba matamanio makubwa sana.tuliza kichwa focus kwenye masomo fata moja mbili tatu usiruke namba.
 
Kwann usiitumie hio nguvu kazi ya hao ndugu zako shambani,lima mazao yenye Uhakika wa kuvuna hata kwa mvua ndogo mfano kunde, karanga,haya mazao demand yake kwa mjini ni kuwa kilo moja ya karanga lishe ufika hadi elf 4.
Kunde si chini ya elf 2 kilo.
Heka moja unavuna gunia 8-10.
Lima Heka 20.
 
Mwache mwenzako asome kwanza[emoji23][emoji23]
Asome!!!? Shule itamsaidia nini?? Hiyo elementary education aliyoipata inamtosha, shule imeua vipaji vya wengi, shule imekula mitaji ya wengi, atafute cha kufanya kupitia hiyo ada anayoenda kutupa shuleni[emoji23]unaweza ukasema havina mashiko ila ukisoma between the lines utaona vinafikirisha.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Unaijua output ya kilimo cha mkono???


Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Unaweza ukapanda zao la nyonyo mbarika Castro oil hata eka 30 uhitaji kulima ni kuchoma tu majani au kama ardhi ni kame au jangwa unapanda tu yanakuwa kwa umande hata kiangazi yanastawi baada ya miezi 3 unavuna mbegu zake unaanika unakamua mafuta.
Unaweza ukaexport au yatumia Kama malighafi ya kuzalisha sabuni za miche unauza unapata pesa ya kuondoa umasikini wa familia.
Huku kila mmoja ukimpatia ujuzi wa maarifa ya uzalishaji.
 
Wewe jamaa hapana kwakweli πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…