Mwenyekiti, Katibu Mkuu CHADEMA kigugumizi cha nini sakata la Wabunge wa Viti Maalum?

Mwenyekiti, Katibu Mkuu CHADEMA kigugumizi cha nini sakata la Wabunge wa Viti Maalum?

Nakuonea huruma kwa kupeleka Imani yako kwa Lissu, mwenye kichwa kinacho waka moto.
 
Mbowe na mnyika mkumbuke tuliwachangia fedha msifungwe. Hao kina Halima halikadhalika. Uchafuzi wa Oktoba umewaacha watu na vilema, wengine wamekufa. Leo hii mnakisaliti chama!! Wallahi, wasipofukuzwa uwanachama, CHADEMA bye bye. Katafuteni kazi nyingine.

Mkuu umenena vyema na bila ya kupepesa macho.

Hili lisichikuwe wiki!

Idda, Halima, Esther na wenzenu habari ndiyo hiyo. Karata pekee mlinayo huko ni kubadili mawazo au kuhamia CCM kabsaaa!
 
Hicho chama kipya nahisi kitang'olewa fizi kabla hata hakijaota meno.Uniparty system at work.Watu wamejipanga aisee.Cha msingi tuhamishie katiba ya China huku.
 
Hiki ndo ambacho nilikua nakiwaza, nadhani tumemfahamu Tundu Lissu kwa muda mrefu, ni wakati wa kuanzisha chama chake sasa, hakika watu wenye misimamo kama yake tupo na labda itakua ndio njia mpya kuelekea serikali mpya. Ila kwa Chadema i think tumeona sura harisi ya walio wengi kule katika uongozi, tamaa na kutokujiamini na kutochange mbinu vinawamaliza very slowly, God forbid !!!!
TL akianzisha chama nahisi kitang'olewa fizi kabla hakijaota meno.Vitabaki vya ubwabwa tu.
 
Toeni tamko kuhusu akina Mdee. Mkikaa kimya kama mlivyofanya Kwa Aidan, CHADEMA mnaizika.
Wafukuze, hawana tofauti na wauaji ambao wamewaua akina Mawazo, Ben na wengine.
Mawazo alikufa ili nyinyi muwe wasaliti
Tusubiri press kwanza
 
Na sasa ndo mtambue kwanini Lissu alipita kufanya kampeni bila back up ya mwenyekiti na katibu wa chama.
 
Ukimya wa Mbowe unasema kila kitu tatizo mnataka mpaka mtafuniwe, Mbowe hajaongea toka maandamano yakose watu, yule ni mfanyabiashara anajua kusoma alama za nyakati... chama bila ruzuku kitakufa, bora lawama kuliko fedheha
Hivi ndo kinakufa sasa.Any way tusubiri press kwanza
 
Upatikanaji wa viti maalum lazima ufuate utaratibu wa chama na sheria za nchi.

1. Maswali ya msingi ya kujiuliza je hao waliokwenda huku wamepatikana kupitia vikao halali vya chama au wamejipeleka wenyewe?

2. Pili je sheria ya kuwasilisha majina hayo NEC na bungeni imefuatwa au imekiukwa?

Kama hayo hayajafuatwa ni uhuni tu kama uhuni mwingine mwingi tulioushuhudia katika utawala wa awamu hii ya tano na hauwezi kuwa ni kwa maslahi ya nchi hata kidogo!
Tusubiri press kwanza
 
Ilishasemwa mara nyingi tu: "Upinzani Halisi Utatoka Ndani ya CCM". Hata Kenya, upinzani wa uhakika ulianza kushika kasi baada ya KANU kugawanyika.
 
Mbowe hana cha kupoteza yeye anaangalia ruzuku tu,jishangae wewe mishipa ya shingo imekutoka kujifanya unakijua chama kuliko Mbowe na mkwe wake.

Hivi vyama ni biashara za watu,ukiingilia maslahi ya watu unatolewa kama CHACHA.
CCM ni biashara ya nani?
 
Unataka Mbowe na Mnyika wawe wanalopoka kama jiwe la Chato....

Sasa ni zamu yenu koropekeana ninyi kwa ninyi. Dhambi ukishaitenda na ukawa mnafiki hutaki kukiri itakutafuna. Hii dhambi ya kutaka kuwagawa Watanzania kwa kujenga chuki kupitia uongo itawatafuna mpaka iwamalize.

Kipindi cha kampeni CHADEMA kupitia Tundu wameliharibu mno taifa na sasa chama kinatafunwa na dhambi hiyo hiyo.

Tundu hafai kuwa kiongozi wa Chama ngazi ya juu sembuse uongozi wa Taifa. Tundu ni mwanaharakati na wanaharakati wengi wanaongozwa na mihemko na hisia. Hawana dira kama viongozi. Slaa alikuwa kiongozi na ndiyo maana aliweza kuiunda CHADEMA kuwa Taasisi imara kama chama.
 
Back
Top Bottom