Mwenyekiti Mbowe, kweli Rais Samia amefanya mazuri ila sifa kwake zimezidi!

Mwenyekiti Mbowe, kweli Rais Samia amefanya mazuri ila sifa kwake zimezidi!

Sijui Kinana alimwbia we lewa, maana haeleweki. Anyway ngoja nitafute ugali wa wanangu
 
Kuna mengi Raisi Samia anafanya vizuri. Kuhusu bei ni tatizo la kidunia sio Tanzania pekee. Kuanzia China, US , EU tatizo la bei ni kila mahali. Mimi nipo Texas na bei ni tatizo mpaka huku.

..she is not doing enough.

..hakuna anayesema Ssh hafanyi chochote.

..hivi huko Marekani mkilalamika mfumuko wa bei Biden na Democrats huwa wanawajibu hata Tanzania, Lesotho, Yemen, kuna mfumuko?
 
Sasa usije ukakuta unajichanganya mwenyewe mkuu wangu 'econo'.
Hayo ya "sirini", ndiyo hayo hayo yahusuyo hiyo Katiba; kwa sababu mambo ya katiba siyo mambo rafiki kwa CCM hata kidogo.

Sawa mkuu nimekuelewa.
 
Upinzani wa Tanzania ushaparaganyika...

Hatuna vibrant upinzani zaidi ya wajanja wajanja!

Mbowe is compromised, hata warudi Lissu na Lema, hatuna watu wenye strong challenge dhidi ya CCM.

CHADEMA washapoteza misingi yao ya kupigania kihalisia haki za wanaoteswa na CCM
 
Tukiombee chama,

Kinapitia wakati mgumu,ambapo Kwa uongozi wa CCM ulivyo dhaifu, CDM ingetakiwa iwe inapeta tu!!!

Chama na viongozi wake wakae wayamalize,

Naamini mikutano ijayo hawatotuangusha.

Ameeen
Udhaifu upi? Binafsi naona Wana ccm awamu hii Wana vingi vya kujivunia kuliko miaka iliyopita.

Kwa mfano mkutano wa Leo zaidi ya kusema Rais kakopa,maisha magumu kwani Kuna jipya?
 
Upinzani wa Tanzania ushaparaganyika...

Hatuna vibrant upinzani zaidi ya wajanja wajanja!
Sasa hawana ajenda ila Wanategemea matukio na upepo 😁😁.

Mbaya zaidi Huwa hawana alternative ya wanachokosea ila kutukana kwenye mitandao na kujiona Wana akili kumbe zero brain
 
Amepoteza hii nafasi. Ametumia muda mrefu kuwakaripia viongozi wenzake wa Chadema kuliko kuikosoa CCM. Ametumia mrefu mno kulalamikia dhana kuwa amelamba asali kuliko kuwazungumzia wanachama wenzake ambao bado wako ndani. Mimi nilitegemea angetumia nafasi hii kuunganisha na kuwatia moyo wanachama wenzake lakini badala yake ametuonyesha kuwa kuna mpasuko ndani ya chama chake na hataki kukoselewa. Ameni disappoint sana. Angalau viongozi wenzake waliomtangulia walionyesha kuwa bado moto unawaka ndani ya matumbo yao.

Amandla...
Anzisha chama na wewe uvunjiwe hotel, ufungiwe account, upewe kesi za uhujumu uchumi na ugaidi halafu uje hapa kubwabwaja upumbavu wako huo.

Mbowe hakuna watanzania wanachomdai ameshafanya kila kitu na now yupo 60years +

Wakina Mnyika, Heche, Lissu na Pambula ndio wanatakiwa kufanya kazi zake !!!

Acheni kumuandama mtu ambaye kapambana Sana Sana wabongo hata mtetewe vipi hamjitambui!!

Hata kama ni kweli amepewa asali acheni tu ale maana anatetea wapumbavu!!
 
Anna Nkya, kwa tanzania tulivyo, Mbowe ana haki ya kumshukuru Samia. Samia angeliweza kukaza kama magufuli na hakuna cha kumfanya maana Tanzania tu waoga wakubwa, mimi, wewe na yule. Kenya ingelikuwa hakuna haja ya kumsifia maana wana uwezo wa kulazimisha la kisheria wanalotaka kulifanya (kumbuka wakati wa kumwapisha Raila miak hiyo, polisi/serikali walitishia kuwa watafyatua wakidiriki kuja kwenye kuapishwa, walimiminika watu kuzidi ilivyofikiliwa, meaning walikuwa tayari kufa!). Wewe unaweza, tupo hapa na fake IDs. Woga. Hivyo kwa Samia kufungua mikutano, ni vema akashukuliwa! anna
Wanaona Mbowe kakosea naomba watangulie jela Ili tuone..
Waongee tuu jambo la kuhatarisha uslama wa Nchi au kupotosha
 
Yaani mwamba Hajasema Neno lolote linalogusa maisha ya Wananchi zaidi yakusifia watawala. Leo hii mbowe anawaambia Wananchi walipongeze jeshi la police[emoji848][emoji848]
Bila Mbowe kupambana wale waliofungwa jela wangeozea huko huku nyie wapuuzi wa mitandaoni hamna mlichowasaidia..

Mbowe kawajua Watzn,utasifiwa sana kwenye mitandao ila kuchukua hatua huwezi kuwaona ni kama wajumbe tuu.
 
Niseme hapa waziwazi, ni kwa TAHADHALI TU!

Kilichomshinda Magufuli baada ya kutumia maguvu yote yale; hatimaye Samia anaweza kukimaliza kwa sauti nyororo kabisa.

CHADEMA inaweza kusambaratika na watu wasijue ni kipi kimetokea!
 
Anzisha chama na wewe uvunjiwe hotel, ufungiwe account, uolewe kesi za uhujumu uchumi na ugaidi halafu uje hapa kubwabwaja upumbavu wako huo.

Mbowe hakuna watanzania wanachomdai ameshafanya kila kitu na now yupo 60years +

Wakina Mnyika, Heche, Lissu na Pambula ndio wanatakiwa kufanya kazi zake !!!

Acheni kumuandama mtu ambaye kapambana Sana Sana wabongo hata mtetewe vipi hamjitambui!!

Hata kama ni kweli amepewa asali acheni tu ale maana anatetea wapumbavu!!
Angalia wanaokuunga mkono ndio utajua kuwa mpumbavu ni wewe na sio sisi.

Amandla..
 
..she is not doing enough.

..hakuna anayesema Ssh hafanyi chochote.

..hivi huko Marekani mkilalamika mfumuko wa bei Biden na Democrats huwa wanawajibu hata Tanzania, Lesotho, Yemen, kuna mfumuko?
Marekani walitaka kuwatosa Democrats kwa sababu ya mfumuko wa bei. Kilichowaponya ni suala la abortion. Na Republicans kusimamisha machizi.

Amandla...
 
Nahisi Mwenyekiti kuhutubia akiwa CHAKALI ina maanisha kuvaa miwani ya mbao kufisha tuhuma za yeye kulamba asali.

Ila tulisoma CUBA tunajua na yeye mwenyewe anajua hana jinsi maana ile kesi ya ugaidi umewekwa PENDING akienda tofauti wana review imekuwa fimbo ya kumchapia na kuwanyamazisha.

Sawa maridhiano ni mazuri lakini awaoni gharama za maisha kusababishwa na mfumuko wa bei,na ufisadi etc
Makosa yalishafanyika 2015 baada ya mwenye chama Mbowe kujiamulia peke yake. Kazi iliyofanyika tangu 2005 ilisambaratishwa 2015 kwa kumsumamisha mgombea ambaye CHADEMA wenyewe walimwita fisadi kwa miaka kadhaa. CHADEMA wangebaki na watu wenye misimamo kama Dr Slaa wangekuwa bora zaidi ya leo. SHORTCUT IS A WRONG CUT
 
Uamuzi wa kumsimamisha Lowassa 2015 ulikuwa sahihi kwa sababu:
a. Aliwasaidia kupata wabunge wengi kuliko ambavyo wangepata kama wangemsimamisha Slaa. Walifanya vizuri kuziba pua zao kwa manufaa ya muda mrefu. Na ukweli ni kuwa hata wangemsimamisha Yesu asingeshinda.
b. Ultimately Slaa alionyesha rangi yake halisi kwa kuhamia upande wa pili. Mimi nahisi angeweza hata kuachia ngazi wakati wa uchaguzi. Slaa amepoteza credibility yeyote aliyokuwa nayo.

Amandla...
 
Mambuzi yalikua yanategemea mbowe amtukane bibi ushungi ili akamatwe wafurahi. Kalagabaho imekula kwenu [emoji1787][emoji1787]
Mkuu nilikimbilia Aljazeera kufuatilia mkutano sikukuta LIVE,imekuwaje na wewe umetuambia tufuatilie Live huko na kwenye International media nyigine?
 
Uamuzi wa kumsimamisha Lowassa 2015 ulikuwa sahihi kwa sababu:
a. Aliwasaidia kupata wabunge wengi kuliko ambavyo wangepata kama wangemsimamisha Slaa. Walifanya vizuri kuziba pua zao kwa manufaa ya muda mrefu. Na ukweli ni kuwa hata wangemsimamisha Yesu asingeshinda.
b. Ultimately Slaa alionyesha rangi yake halisi kwa kuhamia upande wa pili. Mimi nahisi angeweza hata kuachia ngazi wakati wa uchaguzi. Slaa amepoteza credibility yeyote aliyokuwa nayo.

Amandla...
Kwa hiyo Mbowe alikuwa sahihi kujiamulia nje ya vikao halali vya chama? Kumbuka Slaa alihamia CHADEMA baada ya CCM kukata jina lake Dodoma mwaka 1995. Wajumbe wilayani walimpitisha kuwa mgombea ubunge wa Karatu dhidi ya kigogo wa wakati huo Mzee Qorro. Kamati kuu ikakata jina ndo akahamia CHADEMA. Kwahiyo Slaa sio mtu anayependa ubabaishaji. Hakukuwa na namna yoyote aendelee kukaa pamoja na watu waliomfanyia uhuni.
 
Kwa jinsi ulivyosimulia historia ni dhahiri kuwa hakuwa mtu wa principles bali aliangalia zaidi atafaidika vipi. Hakuhamia CDM kwa sababu alizipenda sera zao au msimamo wao bali ilikuwa ni hasira ya kunyimwa ugali CCM. Ndio maana siku zote anasema hajawahi kurudisha kadi yake ya CCM. Na aliondoka Chadema kwa sababu tu aliona amenyimwa ugali ambao ni stahili yake. Angekuwa ana integrity asingerudi CCM hata alipoahidiwa ugali wa ubalozi. Na alipokuwa kule alitumika bila kinyongo kuwa vuvuzela wa CCM.

Mbowe alikuwa sahihi kumtema kama alivyowatema Sumaye, Mashinji na wakina Halima.

Amandla...
 
Back
Top Bottom