GE2025 Mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu achukua Fomu ya Urais Oktoba 2025

GE2025 Mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu achukua Fomu ya Urais Oktoba 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kweli Siasa ni Sayansi, kama mchezo Chadema imefungiwa kufanya Siasa hadi kesi yao ya mgawanyo wa Mali itakapoamuliwa.

Wakati huo huo Mwenyekiti wake, Bwana Tundu Lissu yupo Mahabusu miezi mitano hii inaelekea Kwa kesi ya Uhaini šŸ™Œ

Samia, anaenda kuvunja rekodi ya mtangulizi wake hayati JPM kwenye huo Uchaguzi

Yeye atakwenda kushinda Kwa asilimia 99.5 huku ACT akienda kuambulia hiyo asilimia 0.5 iliyobaki

Maana hakuna tena Ushindani wa Chadema Mwaka huu

Hapo siasa ni sayansi haijatumika Bali mabavu yametumiaka.
 
Nadhani ndiyo kitu wanachopanga kwasasa, japo kuna mtu alinidokeza kwamba huyo Bwana ataendelea kukaa Mahabusu hadi Uchaguzi upite

Ndiyo maana wameamua kutengeza trick ya kuficha mashahidi kisha baada ya Uchaguzi, DPP anasema hana nia ya kuendelea na kesi

Kesi bado haijaanza. Bado committal proceedings.
 
Kesi bado haijaanza. Bado committal proceedings.
Ndiyo lakini hujaona hizo danadana Kaka?

Hao watu wataendelea kumshikiria hadi Uchaguzi upite

Wanachoogopa Tundu Lissu ana nguvu za ushawishi pamoja na kujua kupangilia hoja zake
 
Ghiriba ya roho ni Zaidi ya sikununu, Sina choyo wala chuki ya nafsi, muda ukiwadia naenda kutumia haki yangu ya msingi kikatiba! Ni mitano tenaaaaaa kwakishindo kikubwa mnooooooooo!
 
Mungu asipo ingilia kati swala la lisu, Atahukumiwa kunyongwa, Aje atolewe kwa msamaha na Samia baada ya kua Rais.

Hii itamuondokea Sifa ya kuja kugombea kama Rais Siku za usoni
Si rahisi. Hiyo hukumu itazua taharuki, hata kabla ya huo msamaha inaweza leta tatizo kimataifa na kitaifa.
 
Yeye achukue tu ila wakumchagua ndo kipengele
 
Back
Top Bottom