Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan, na mgombea mwenza, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo Agosti 9, 2025 wanaenda katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuchukua fomu kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Msafara wa Magari yaliyomsindikiza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM), Samia Suluhu Hassan wakati akielekea kuchukua fomu kwenye Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)
Rais Samia ametumia dakika 27 tangu alipoingia ndani ya ofisi za INEC na alipotoka alikuwa ameongoza na mgombea mwenza, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zuber Ali Maulid na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda.
Nje ya ofisi hizo, wagombea hao wakiwa na begi jeusi lililoandikwa “Fomu za Uteuzi”, walipiga picha na makundi tofauti ya makada kabla ya kuondoka.