Mwigulu Nchemba ang'aka kuagiza mabasi 60, asema hana biashara hata ya bajaji

Mwigulu Nchemba ang'aka kuagiza mabasi 60, asema hana biashara hata ya bajaji

Kwani kosa kumiliki company ya magari au kuwa na hisa
Ni kosa kupata utajiri kupitia fedha za umma.

Watu wanajiuliza kapataje huo ukwasi maana historia yake wanaifahamu.
 
Sisi raia hatuna haki hiyo?
Ninhakinyako ni hela yako tu

Mbunge anapokea milioni 12 kwa mwezi atashindwa kusomesha Feza ada ya milioni 9 kwa mwaka unalipa mara Tatu? Yaani kila miezi minne.unalipa milioni 3

Kwa mwaka mbunge anapata milioni milioni 144 nje ya posho ada Feza milioni 9 akiwa.na watoto wanne ni milioni 36

Ukichukua milioni 144 ukatoa milioni 36 anabaki na milioni 108 balance mfukoni cha ajabu nini?.

Mbona watu wa kawaida tu wanasomesha watoto shule za Feza

Mbona kitu kidogo sana kwa waziri
 
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amefadhaishwa kuambiwa ameagiza mabasi 60, amedai hana hata biashara bajaj. Mwigulu amesema hakuna haja ya kuchafuana.

Dokezo - Waziri aagiza mabasi 60, Kampuni ya Esther

=====

Mwigulu Nchemba: Imekuja tozo, mtu anasema ona waziri huyu ameagiza mabasi 60 kwenye kampuni yake, mimi sina kampuni hata ya bajaj. Hivi unaweza ukatoka chuo tu ukawa na bweni la wasichana na wavulana la kusaidia halafu uwe na kampuni ya biashara, sina biashara hata ya bajaji.

Kisa tozo, hii ni dhamana tu, hatuna haja ya kuchafuana. Unahangaika kuchafua mtu.

Jf inanguvu hadi imemtowa waziri alikojificha.Hongereni na heri sana kwa jf.Tunamsubiri mh waziri wa kilimo aje atowe ufafanuzi wa yanayoendelea ktk kuandikisha wakulima.
 
Kwa nini asisomeshe kwenye shule za kata kama shule ya msingi mbagala?
Wewe hupangiwi wanao usomeshe wapi huwezi mpangia mwingine asomeshe wapi

Pambana na hali yako na wanao Ya mzazi mwingine mwchie.mwenyewe
 
Ile Tanganyika sijui nini ada per year ni milioni 50 lakini hapo ana watoto wa 4
Kwani mshahara wake kwa mwaka hautoshi kulipia M 200 kwa watoto aliozalisha mwenyewe....!!! Ukichanganya na tozooo!????[emoji849][emoji849][emoji849]
 
Wapi imeandikwa kuhusu watoto wa mawaziri wasome shule fulani? Hizo ni roho cha kichawi na umaskini.
Kweli kwa maana anatafuta pesa kuhudumia Familia yake. Nadhani watoto na Familia yake ni wahanga wa kulambishwa asali wasiyojua malino yake
 
Documents zote zinasomeka Ester. Aweke cheti cha ndoa hapa muone miujiza.
Hapa sio mahakamani

Kwenye sheria za makampuni mtu yeyote aweza mali kwa jina lake

Kama documents zinasomeka Esther yeye hawezi msemea huyo Esther ni sawa na kwenda kuhoji saluni ya mke na mwanaume kujitia ohh saluni yangu
 
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amefadhaishwa kuambiwa ameagiza mabasi 60, amedai hana hata biashara bajaj. Mwigulu amesema hakuna haja ya kuchafuana.

Dokezo - Waziri aagiza mabasi 60, Kampuni ya Esther

=====

Mwigulu Nchemba: Imekuja tozo, mtu anasema ona waziri huyu ameagiza mabasi 60 kwenye kampuni yake, mimi sina kampuni hata ya bajaj. Hivi unaweza ukatoka chuo tu ukawa na bweni la wasichana na wavulana la kusaidia halafu uwe na kampuni ya biashara, sina biashara hata ya bajaji.

Kisa tozo, hii ni dhamana tu, hatuna haja ya kuchafuana. Unahangaika kuchafua mtu.

Ni mara chache sana mwenye kosa la jinai kukiri kosa mbele ya vyombo alivoalika mwenyewe!

Hata anae fumaniwa hakubali kosa... japo kafumaniwa!
 
Kumekuwa na uongo mwingi sana kwa viongozi wetu, na hapa Kuna watu huusika kuwachafua kwa maslahi yao.

Mwigulu anasema hamiliki hata kampuni ya bajaji, ilaa anashangaa kuhusishwa na kumiliki kampuni ya mabasi.

Tuache kuwasingizia uongo hawa viongozi. Kama huna ushahidi ni bora ukakaa kimya.

Hawa wanaosema Waziri Mwigulu anamiliki mabasi ndio haohao walisema Lowassa anamiliki kampuni ya Richmond, Ila mwisho wa siku ndio haohao wakageuka na kuanza kumsafisha huku wakizungusha mikono
Unamsemea bro, waache wafu wazike wafu wao. Au Na wewe unafaida tozo? Issue hapa ni hizi tozo hazina mashiko hata chembe ni uonevu wa wananchi.
 
Tumepiga mwizi wa baskeli mpaka tumeua huku akikana yeye siyo mwizi. Tulipoanza kumchoma moto mama yake akatuletea baskeli yetu na kusema "Baskeli yenu hiyo muacheni mwanangu" Mwiguru na mabasi mtapiga mpaka mtaua
 
Back
Top Bottom