Mwigulu Nchemba ang'aka kuagiza mabasi 60, asema hana biashara hata ya bajaji

Mwigulu Nchemba ang'aka kuagiza mabasi 60, asema hana biashara hata ya bajaji

Tujue ada, kwanini wasisome shule hizi za bure? Si elimu imeboreshwa kuna shida gani kuwa mfano watoto wao wasome hizi changanyikeni?
Acha mawazo ya kijima kwani wewe imezuiwa kupeleka mwanao unapopataka, mwishowe utataka kujuwa Hadi anacheka Mara ngapi kwa siku,
 
Unatosha kuwadanganya wafaidika wenzio, sisi tunaoumizwa na tozo zisizo na uhalali huwezi kutudanganya. Acha tuendelee na kampeni, bora hela iibiwe na mwizi anayehangia maisha kama Mimi kuliko mwizi anayetumbua maisha kama wewe.
Tozo Ni kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu Nazani umesikia faida kubwa na hatua iliyopigwa kutokana na tozo zetu, kuwa mzalendo kwa maendeleo ya Taifa letu
 
Ni hivi, Lowassa alikuwa mwizi, na alipewa nafasi ya kugombea na viongozi wa CDM kwa kuwahonga na sio kwamba alikuwa msafi. Huyo Mwigulu ni mwizi na asitegemee kukanusha ndio atakuwa sio mwizi. Kama yuko madarakani kwa wizi wa kura na anasema alishinda kwa kishindo, unaweza kumwamini kwa lolote?
Leta ushahidi wako hapa, kwa Sera zipi ambazo mgombea wa upinzani angeweza kumshinda mh Mwigulu? Nyinyi mmezoea siasa za vimatukio tukio vya kupita Kama ukungu hivyo hamuwezi kuitikisa ccm
 
Lisemwalo lipo, kama hajanunua hayo mabasi ila atakuwa na mahela ya kufa mtu
Mahel mangapi? Kwani akiwa na hela au asipokuwa na hela ndio kwamba zitaongezeka kwenye mifuko yako Kama usipojibidisha? Pambana kutafuta fursa ya kusonga mbele, usiwe na wivu maana itafifisha uwezo wako wa kutafuta fursa na kubaki na Roho ya kwanini,
 
Yeye kama waziri wa Fedha lazima ajue kuna mabasi 60 yameingizwa .... hakuna haja ya kumtaja mwenye mbasi walau angekubali kuwa kweli kuna mtu kaagiza hayo mabasi na kiwango cha kodi kilicholipwa.

Kwa yeye kukataa kutoa ufafanuzi basi kuna walakini ..... Hawa jamaa kwenye matumizi ni wepesi sana kusema ni kiasi gani kinatumika na asante kwa Maza ..... ila kwenye makusanyo wanafichaficha ..... hii ni kwa sababu ya makandokando yao!!
Acha mawazo potofu, hayo magari umeyaleta wewe, akubali kitu kisicho Cha kweli ili aufurahishe moyo wako? Wewe ndio weka huo ushahidi wako hapa Kama unao na siyo kuleta hoja zisizo na mashiko
 
Kwa aliyesoma kitabu cha The Beautiful Ones Are Not Yet Born, atajua kwanini yeye ni mmiliki na anasema hamiliki. You own something by assigning someone as owner.
Hiki kitabu nilikipenda sana, ntakitafuta niwe nacho
 
Sema nini wakuu, leo kuna ID moja hivi haijapita kabisa kwenye huu uzi ila jana, juzi ilikuwa ikitetea sana juu ya lile dokezo la mabasi 60, sasa ni wazi napata picha ID hiyo ni ya muhusika wa hayo mabasi...teena anavyoijua Singida hakika ni yeye kabisa huyo.
 
Mahel mangapi? Kwani akiwa na hela au asipokuwa na hela ndio kwamba zitaongezeka kwenye mifuko yako Kama usipojibidisha? Pambana kutafuta fursa ya kusonga mbele, usiwe na wivu maana itafifisha uwezo wako wa kutafuta fursa na kubaki na Roho ya kwanini,
Mimi ni Binti msomi, mchapakazi, najiamini na ninakipato changu. Kutoa wazo kama Hilo katika nyuzi kusikufanye kuniona am broke as hell, pambanua na faragua hoja kwa hoja attacking my personal life it's not a good thing, Mwigulu ni kiongozi na akikosea au asipokisea atazungumziwa Hadi maisha yake binafsi.
 
Mimi ni Binti msomi,mchapakazi, najiamini na ninakipato changu. Kutoa wazo kama Hilo katika nyuzi kusikufanye kuniona am broke as hell, pambanua na faragua hoja kwa hoja attacking my personal life it's not a good thing, Mwigulu ni kiongozi na akikosea au asipokisea atazungumziwa Hadi maisha yake binafsi.
Naomba unisamehe Kama nitakuwa nimeonekana kukushambulia wewe binafsi, Maana Mimi napendaga kujielekeza katika hoja iliyo mezani na siyo kumshambulia mtu, Ndio maana Mimi huwezi Nikuta nikimtukana mtu hata Kama natofautiana Naye kimtizamo.
 
Leta ushahidi wako hapa, kwa Sera zipi ambazo mgombea wa upinzani angeweza kumshinda mh Mwigulu? Nyinyi mmezoea siasa za vimatukio tukio vya kupita Kama ukungu hivyo hamuwezi kuitikisa ccm

Kwani mgombea anashinda kwa sera au mvuto? Ni nani anapiga kura kwa kuangalia sera dogo? Kama serikali ingekuwa inafanya kazi kwa kuangalia sera, Mbowe angeongea jana asingejibiwa na mawaziri leo hii? Au sera siku hizi ni vyombo vya dola na tume isiyo ya uchaguzi? Ni hivi, Mwigulu ni mwizi fullstop.
 
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amefadhaishwa kuambiwa ameagiza mabasi 60, amedai hana hata biashara bajaj. Mwigulu amesema hakuna haja ya kuchafuana.

Dokezo - Waziri aagiza mabasi 60, Kampuni ya Esther

=====

Mwigulu Nchemba: Imekuja tozo, mtu anasema ona waziri huyu ameagiza mabasi 60 kwenye kampuni yake, mimi sina kampuni hata ya bajaj. Hivi unaweza ukatoka chuo tu ukawa na bweni la wasichana na wavulana la kusaidia halafu uwe na kampuni ya biashara, sina biashara hata ya bajaji.

Kisa tozo, hii ni dhamana tu, hatuna haja ya kuchafuana. Unahangaika kuchafua mtu.

Esther ni mabasi ya nani?
 
Kumekuwa na uongo mwingi sana kwa viongozi wetu, na hapa Kuna watu huusika kuwachafua kwa maslahi yao.

Mwigulu anasema hamiliki hata kampuni ya bajaji, ilaa anashangaa kuhusishwa na kumiliki kampuni ya mabasi.

Tuache kuwasingizia uongo hawa viongozi. Kama huna ushahidi ni bora ukakaa kimya.

Hawa wanaosema Waziri Mwigulu anamiliki mabasi ndio haohao walisema Lowassa anamiliki kampuni ya Richmond, Ila mwisho wa siku ndio haohao wakageuka na kuanza kumsafisha huku wakizungusha mikono
huna akili.
 
Labda awadanganye nguchiro wenzake, huyo hawezi kuwa masikini.
Mara nyingi nakuambia huna akili hata kidogo. Mwigulu anaachaje kuzungumzia maskini ikiwa nchi yetu ni maskin? Au unataka aseme sisi matajiri donor country Kama alivyokuwa akisema Magufuli?

Kujifanya wewe ni tajiri huku ukiwa ni maskini wa kutupwa ni ujinga uliopitiliza.

Tanzania ni maskini na watu wake ni maskini wa kutupwa. Ukweli ni huo
 
Back
Top Bottom