Mwigulu Nchemba awaambia Watanzania wahamie Burundi wasipoweza kulipa tozo za miamala

Mwigulu Nchemba awaambia Watanzania wahamie Burundi wasipoweza kulipa tozo za miamala

Mama nakushauri apunguze mawaziri jeuri kama huyu Mwigulu....anamharibia pia kiburi hicho hata kwa mama hata muheshiku kisa Dr wa Uchumi.......ampumzishe aone kama nchi haitaenda....anajiona yeye ndie next President....Mama tupe zawadi ya Eid
 
Badala ya kujibu swali aliloulizwa kua serikal ina mtazamo gn juu ya swala la kinyonyaj yeye anasema hapaswi kutiliwa shak ni daktari, unaeza ona apa uwezo wake ulivo mdogo
 
Kwenye hili swala la tozo sisi raia tumelilalamikia limetuumiza,sasa imekuwaje bwana mwigulu atunange na kutuambia twende burundi kama hatutaki kutozwa hizo tozo mpya ilihali SASHA alikuwa yupo ziarani huko? Ni nini kimetokea hapa katikati WADAU? Ina maana alikuwa anamaanisha nini mpaka aseme hivyo?

Ok na kama ni bahati mbaya aliteleza kwann asitolee mfano hata Rwanda basi au uganda yeye kalenga tu burundi?
Naomba kuwasilisha.
 
Raisi wake alikuwa na ziara huko, na pia makamu wa raisi.!
 
PhD amepata awamu ya 5 kabla hajaingia mgogoro na Maaskofu wa KKKT
Hayo majina ni yakwake aliyoanza nayo shule???

Hajaiba majina ya Mtu mwingine baada ya yeye kufeli darasa la 7?
 
Huyu ni shetani unakumbuka alivyomfanya Tundu Lissu mtu wa kwao mkoa mmoja Singida,je watu wengine atakuwa na huruma nao?

Fikra pana hii,Mama Samiah ametulia,halioni hili na litacost utawala wake.
Kwani hakushirikishwa?

Hakutia saini?
 
Jeuri ya namna hii huwa wanakuwa nayo Wanasiasa wa Tanzania tu. Sababu wanajua Wananchi wa Tanzania wanaowalipa mishahara na posho. hawana la kuwafanya.

Ni kauli iliyojaa dharau, kebehi, kiburi, ujivuni, ubazazi, ubaradhuli na ulaanatullah. Huyu amejikinai. Hawajali wananchi maskini wa Tanzania. Na watanzania sababu ni wapole sana nadhani hatuna la kufanya.

Tumpongeze anaupiga mwingi sana.

Huyu Mwigulu huwa anajiona ana akili sana kuzidi wachumi wote kumbe hayo madigrii yake ni makaratasi tu na ufaulu wake tunaujua ulijaa kuhonga honga hadi kufikia hapo alipo. Hebu muangalie akiwa anaongea hana tofauti na 'rum pen' mwingine wa mtaani, haongei kisomi, ndo maana Hayati Magufuli alimtmbua baada ya kimuona ni gumashi tu hilo
 
Mi sijawahi msikia akiongea jambo kisomi. Ni mtu mpuuzi tu.

Huyu Mwigulu huwa anajiona ana akili sana kuzidi wachumi wote kumbe hayo madigrii yake ni makaratasi tu na ufaulu wake tunaujua ulijaa kuhonga honga hadi kufikia hapo alipo. Hebu muangalie akiwa anaongea hana tofauti na 'rum pen' mwingine wa mtaani, haongei kisomi, ndo maana Hayati Magufuli alimtmbua baada ya kimuona ni gumashi tu hilo
 
Huyu jamaa ni mpuuzi sana,udakitari wa falsafa sio kujitapa,ni matendo,yeye kuwa na ka PHD ka uchumi,anajiona mwamba,amefanya tafiti ngapi na wapi zilizoleta tija?watu waliokuwa wamebobea kwenye uchumi kama Prof Ndulu,walikuwa na CV nzito kuanzia UN,sasa huyu kasoma hajawahi hata kufundisha,au kufanyia kazi hako ka PHD lake,anatutambia hv
PhD yenyewe ni ile ya thesis, bila course work ya darasani, na ameitafuta akiwa Waziri, unatarajia nini? Kwa mfumo wa Elimu ya Juu hapa TZ, mtu anaweza kununua tu PhD kirahisi sana. Hoja yako ni ya msingi sana, PhD nyingi ni paper works, wanakusanya literature nyingi na kuandika chapters mtu akiwa hata baa pale UDASA, ARISA etc na Ofisini Chuoni, hawana hela na muda wa kufanya utafiti na kukusanya real data, data nyingi zinapikwa tu, wanawalipa vijana vipanga ili wawafanyie kila kitu, halafu yeye anaenda tu kutunukiwa cheti. Mwigulu kuonyesha kuwa ni punguani, ameshindwa kujua kuwa aina ya PhD yake watu wanaijua na siyo ile hasa ya kutamba nayo mbele ya PhD za wachumi bobezi, Mwigulu mdahalo wa mada hot ya kiuchumi hawezi kwenda!

Pili, hakuwa hata na sababu ya kurukia kwenye PhD, ni sawa na kutumia bunduki SMG kuulia sisimizi, swali aliloulizwa lilikuwa simple sana. Ila Mungu anajua kuumbua wanafiki.
 
Ni vigumu sana kumtofautisha Mwigulu na Mwendazake. mwigulu ana character zote za Magufuli
Magufuli hakuwa mjinga design hii ndiyo maana alikuwa anafanikiwa kiasi kisicho wahi kutokea.
 
Mwigulu Nchemba awaambia Watanzania wahamie Burundi wasipoweza kulipa tozo za miamala. Kitendo Cha waziri wa Fedha kuwaambia Watanzania wakimbilie burundi na Rais kupiga kimya Kwa kauli hiyo, sisi Watanzania tumeanza kumuelewa vibaya au tofauti kupitia kauli hiyo.

Kwani kauli ya waziri ni kauli ya serikali.
 
Mwigulu Nchemba awaambia Watanzania wahamie Burundi wasipoweza kulipa tozo za miamala. Kitendo Cha waziri wa Fedha kuwaambia Watanzania wakimbilie burundi na Rais kupiga kimya Kwa kauli hiyo, sisi Watanzania tumeanza kumuelewa vibaya au tofauti kupitia kauli hiyo.​

Kwani kauli ya waziri ni kauli ya serikali.
Ndiyo kwasababu waziri ni sehemu ya serekale ya ccm.
 
Halafu kaanza ziara kwa msafara kama vile yeye ndio Rais, anapofika mahala anasimama kutoa speech kwa wananchi kutafuta umaarufu.

Rais Samia acha acheke na huyu kima, atavuna anayopanda.
Wananchi walijuaje kuwa bwana pesa atapita.Rushwa ilishatangulizwa kwa makada ili auze jina.Ulinzi mkali as if amebeba BOT yote.
Jaji mkuu mwenyewe sijawahi on a msafara na ulinzi mkubwa kama wa Mwigulu.
 
Back
Top Bottom