Uchaguzi 2020 Mwigulu Nchemba: Rais wetu ni Magufuli, waambieni waliowatuma enyi wenye tamaa ya Madaraka

Uchaguzi 2020 Mwigulu Nchemba: Rais wetu ni Magufuli, waambieni waliowatuma enyi wenye tamaa ya Madaraka

Hii kitu Tume Huru inawatesa watu ila sijui kama wanafahamu Tume Huru ikoje. Nakumbuka upande wa Zanzibar walikubaliana na kuwa na kinachoitwa Tume Huru. Wajumbe wa Tume hii wakatoka CCM na CUF kwa idadi sawa. Mwenyekiti wa Tume ile alikuwa Mzee Jecha, sasa jana mzee Jecha kachukua form ya kugombea Urais kwa ticket ya CCM ghafla naona watu wanaibuka wanasema mnaona sasa tulisema Zanzibar hakuna Tume Huru hamkusikia Jecha kachukua form kwa ticket ya CCM. Wamesahau kwamba walikuwa na Tume Huru yenye wajumbe kutoka vyama viwili na hivyo Jecha alikuwa wa CCM lakini ndani ya Tume Huru anavyojitokeza kuchukua form, Tume inageuka kutokuwa Huru. Tume Huru ni ipi? Inatakiwa kuwaje? Labda wanataka Tume yenye wajumbe toka nje ya nchi
 
MIJITU MINGINE ILIKUWEPO NDANI TANGU UJANA WAO HADI SASA, LEO NDIO WAONE HATUNA TUME HURU?? MLISHAISHI MAISHA YENU TANGU ASUBUHI, JIONI YENU MNATAKA KUTUHARIBIA AMANI YA NCHI YETU, VIJANA TUKO MACHO, "HATUTATUMIKA" HATUTARUHUSU TAMAA ZENU ZA MADARAKA KUVUNJA AMANI YA NCHI YETU.
 
Msimamizi naye ni Muwakilishi wa Mwananchi kama tunavyoaminishwa kuwa Mbunge ni Muwakilishi wa Wananchi.

Wabunge mnalipwa na serikali, Wanainchi hatuwalipi chochote, anyway..tunachangishwa (kodi) mpaka tunabaki hoi alafu mnapewa mamilioni mpate maisha mazuri kuliko ya Wananchi...na siku zote anayemlipa Mpiga ngoma ndiye anachagua wimbo.

Muangalizi ni kama jirani tu anayetamani kuja kukaa katikati ya Mbunge (muwakilishi wa Mwananchi choka mbaya) na Serikali (Tajiri anayemlipa Mbunge) ili aone kama Mpiga ngoma analazimishwa kupiga ngoma fulani tu na upande mmoja au na Wananchi nao wana nafasi ya kuchagua wimbo?.

Sasa hamumtaki Jirani...kwani mna cha kuficha?

Ni sawa na kuwe na mechi ya Yanga na Simba na Haji Manara aseme hatutaki Muamuzi tuna muamuzi wetu Mo Dewji....hebu tuwaulize na Yanga (Wananchi) kama nao hawamtaki jirani/Mtu baki aje asimamie pambano..au ni ubabe ubabe?
 
kwa sasa hatuhitaji dereva mwengine.....tunamuamini dereva tuliye anza nae safari atatufikisha salama, Magufuli ndiye atakeye tufikisha 2025 salama.
 
Mwigulu huitetei nchi, bali unajipendekeza kwa rais kwakuwa anaweza kukupa madaraka, ambayo yatakufanya ww, familia yako na ukoo wenu kuepukana na umasikini. Huna historia ya kuitetea nchi, bali siku zote umekuwa na utamaduni wa kukitetea ccm, maana huko ndio una nafasi ya kuepukana na umasikini. Isitoshe we sio mtu muadilifu, bali ni mtu wa siasa za chuki, ukatili na uhasama. Unajipa jukumu la kumtetea rais kwani kwa yale uliyoyafanya, cheo cha urais tu ndio kinaweza kukupa cover. Lakini kwa maneno marahisi ww sio mzalendo, bali ni muhuni mwenye madaraka ya kujipendekeza.
 
Mwigulu wewe naamini ktk demokrasia. Kila mtanzania ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa na hilo halina option.

Mwacheni Membe agombee kwani wananchi ndiyo watakao amua
 
Back
Top Bottom