Mwigulu Nchemba: Serikali imekusanya bilioni 48 kutoka kwenye Tozo za miamala ya simu kwa wiki nne

Mwigulu Nchemba: Serikali imekusanya bilioni 48 kutoka kwenye Tozo za miamala ya simu kwa wiki nne

Kama tunakusanya pesa zote hizi ndani ya wiki 4 basi inabidi Supika aongeze tozo ya kupumua
 
Nukuu moja ya Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Wonston Churchill inasema:
Kutaka maendeleo ya nchi kupitia kodi ni kama vile mtu anaingia ndani ya ndoo na anajaribu kuinua hiyo ndoo kwa mkono wake - yaani kwa mkono wa hiyo ndoo😂😂
 
Deni la Taifa limefika ngapi na wanarejesha ngapi au hawana hata habari ya kulipa?
Au ndio kukopa harusi na kulipa Matanga
 
Hamna alichokisema zaidi ya kutetea, na kudai kwamba bado wanaendelea kulifanyia kazi watatoa tamko siku sijazo. Mwelekeo inaonyesha kwamba serikali haiko tayari kupunguza wanaongea na kampuni za simu wapunguze taarif zao.
Na tayari wamekusanya mabilioni tangu tozo ianze
 
Juzi tu hapa nimeona wananchi Muleba wanajenga kituo cha Afya kwa pesa zao. Ingependeza Waziri akatuonesha vituo vya Afya anavoongelea
Hutokaa uone Kama ambavyo hujui pesa za Muungano zimeenda wapi mpaka Sasa, mtu aliependa kuona matokeo ya anachokisema wameshamuua wajipigie vizuri.
CCM oyeee
 
Mtaani pesa imekuwa adimu halafu alisema watatoa pesa kufanya mzunguko, je wamefikia wapi?
 
Watanzania ni wavivu wa kuyatafakari mambo kwa kina ... Wengi ni wafuata mkumbo..

Naona kuna hata MATAGA yanapiga kelele.. Ila yalikuwa yakimshangilia Magufuli alivyoigeuza nchi yote ka pocket money yake...

Miradi yote kaanzisha yeye...pesa zote alikomba yeye...

Watu tuliishi ka madigidigi na bado alikuwa akitutukana...na kufilisi watu na kuwafungia biashara zao.

Wapumbavu na wavivu wa kufikiri wanafikiri Rais Samia kuna pesa yeyote kaikuta..

Tutafakafi mambo kwa kina na sii kusubiri kutafakariwa.

Hii miradi Mama ana uwezo wa kuisusa. Anaongozwa na Busara

Wapumbaavu wana CCM ambao mnajitoa akili makusudi kabisa dawa yenu inachemka.

Mama songa Mbele..

Una maadui wengi.
Uko sahihi kabisa jamaa alijenga kila kitu Chato kuanzia sgr, ndege, vivuko, meli, madaraja, mashule, mahospital, viwanja vya ndege yaani kila kitu hata makao makuu ya nchi alihamishia Chato.

Na alipomaliza kukomba kila kitu hazina akaamua afe ili aache nchi haina chochote matokeo yake mama yako kaachwa hakuna pesa anakomaa kubrand nchi aliyoikuta tupu na uzuri kwakuwa ni jiniazi anaupiga mwingi mno maana hahitaji matokeo anahitaji porojo tu Kama vile kusema pesa za Muungano tumebadilishia matumizi lakini mpaka Sasa hatujui matumizi yake ila tunashangilia, pesa za tozo tunajenga miundombinu ya hospital na barabara ambazo hatutokaa tuzuone ila porojo.

Tunapenda porojo kuliko matokeo halisi ya kazi.
 
Waziri angesema milioni moja imeenda kituo namba...cha Afya siyo kutuletea mambo ya jumlajumla wakati walisema zinaenda kujenga barabara vijijini na juzi wamekopa kwa kigezo hichohicho cha barabara vijijini
Tuko zama za porojo na sio matokeo
 
Watanzania ni wavivu wa kuyatafakari mambo kwa kina ... Wengi ni wafuata mkumbo..

Naona kuna hata MATAGA yanapiga kelele.. Ila yalikuwa yakimshangilia Magufuli alivyoigeuza nchi yote ka pocket money yake....
Bado unahangaika kuonesha JF kwamba Samia ni bora! Naona kama ziko tenge wewe! Una hakika Samia alikuta hakuna pesa? Nini kimekuonesha upuuzi huo? Zilizoibiwa BoT akaunda tume kisha sema matokeo? Walizogawana wizara ya fedha wakasimamishwa, umesikia lolote tena? We are dealing with hopeless people who, unfortunately, are getting support from hopelessly cultured people.
 
Uko sahihi kabisa jamaa alijenga kila kitu Chato kuanzia sgr, ndege, vivuko, meli, madaraja, mashule, mahospital, viwanja vya ndege yaani kila kitu hata makao makuu ya nchi alihamishia Chato...
Mnavyomganda Mama ni kama vile amekaa miaka Nane... Kumbe maskini ya Mungu she is hardly 6 months in the office..
 
Mheshimiwa Waziri Mwigulu Nchemba , kama miamala kwa siku moja inafikia milioni 11 (11,000,000), Endapo mkaamua kutoza kiasi cha Tshs 1,000 kwa kila muamala, ndani ya Mwaka Mzima mtakuwa na mapato ya Takribani Shilingi (11,000,000*1000*365)= 4,015,000,000,000 tena na zaidi, kwa kuwa miamala itaongezeka zaidi ya hiyo milioni 11.

Hiki ni kiasi kikubwa sana katika kuchangia mapato ya Serikali kutoka kwenye tozo mpya inayoanza. Gradually mwakani mnaweza kuongeza kuwa 2000 kwa muamala. Tunawaomba sana, kwa kuwa mnaenda bungeni kurekebisha, mchukue modality kama hii. Hongereni kwa kazi inayoendelea.
 
Mwigulu Nchemba ana kiburi kweli kauli zake utadhani analeta ligi na wananchi.
 
Back
Top Bottom