Mwigulu Nchemba, tafadhali kafute mabango yako barabarani!

Mwigulu Nchemba, tafadhali kafute mabango yako barabarani!

nimeyaona sabasaba lindi upande wa kulia mnazimmoja mtama na nyangao kwanza mi nashangaa si angeenda kuandika kwenye nyumba za CCM WENZIE!!!!!!??
 
Mwigulu na Maropee walivyosikia Kikwete kasema Urais awamu hii atamuachia kijana wakajua wameula teh. Ati kajiuzulu cheo cha unaibu katibu mkuu wa ccm bara.
 
Ndani ya ile gari ya STG kulikuwa na makopo kibao ya rangi
 
rais mtarajiwa ni makini hajachafua mazingira kama nchemba wala hakuwa na mabasi wala team.

Pombe oyeeeee
 
Hivi ni kweli kabisa Mwigulu alijiaminisha angeweza kuwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania..? Najua uhakika wa kuchaguliwa kuwa mgombea wa ccm alikuwa nao kwa sababu wote ni ukoo wa panya.. Lakini uraisi..??!
 
Hata huku tanga kunani pia..nadhani alikodi vijana kwa ajili ya hiyo kazi maalum..
 
Ayalipie kodi,siyo anatuchafulia mazingira bure tu.
 
Namshauri Mwigulu akaweke 2025 badala ya 2015. Si mbaya ni maandalizi yajayo. Na hiyo itamsaidia kila akipita njiani yatakuwa yanamkumbusha nia yake na hivyo kuongeza jitihada katika uteendaji. Kweli katika miezi kuelekea kutangaza nia Mwigulu alionekana kujitambua. Kumbe watu wengine wanaamua kuwa na uchizi tu. Wakati mwingine wanakuwa watu wa maana. Hongera Mwigulu naomba uendelee kuwa mzalenda hivyo hivyo kwani sina wasiwasi utaendelea kuwa waziri kama CCM ikishinda.
 
Naona google km tangazo la dogo janja..yataning`inia muda mrefua sana.
 
Namshauri Mwigulu akaweke 2025 badala ya 2015. Si mbaya ni maandalizi yajayo. Na hiyo itamsaidia kila akipita njiani yatakuwa yanamkumbusha nia yake na hivyo kuongeza jitihada katika uteendaji. Kweli katika miezi kuelekea kutangaza nia Mwigulu alionekana kujitambua. Kumbe watu wengine wanaamua kuwa na uchizi tu. Wakati mwingine wanakuwa watu wa maana. Hongera Mwigulu naomba uendelee kuwa mzalenda hivyo hivyo kwani sina wasiwasi utaendelea kuwa waziri kama CCM ikishinda.
Ni ushauri mzuri lakini aandike katika akili za watu kwa kufanya kazi kwa bidii na kukemea rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma na si kwa kutuchafulia madhali ya mazingira na structures zetu!!!!
 
Habari ndugu Mwigulu,

Wananchi wa Mbeya tunakuomba uje ufute maandishi yako uliyoweka kwenye mitaro na madaraja mbalimbali hapa Mbeya kwamba wewe ni rais 2015.

Kutokana na jina lako kuondolewa mapema bila maelezo huko Dodoma, wananchi wa Mbeya tunahitaji uje usafishe mji wetu haraka iwezekanavyo.

Nawasilisha ndugu Mwigulu Nchemba.
 
Sio mby pekee, hata mawe yetu hapa Kitonga Iringa umeyachafua, uje na huku Mafinga ufute,utumie staili ile ile uliyotumia kuandika.
 
Back
Top Bottom