Mwigulu Nchemba: Wafanyabiashara msiogope kuweka fedha benki hazitachukuliwa

Umesahau mwanzilishi wa haya ni nani?
 
Mambo ya Robin Hood,je hiyo pesa ambazo serikali iliwanyanganya au kupora pesa hizo kutoka kwenye account zao iziirejeshe
Samahani tu haitoshi.irejeshe pesa zao with interest ndio itapojenga imani kwa wananchi wake.
 
Zitafutwe kwenye account gani? Yule mungu mtu wenu ndo alikuwa anatenda yote haya. Watanzania Tunapumua sasa baada ya jitu lenye roho mbaya kunyakuliwa.
 
Safi sana.
Huu ni mwanzo mzuri.
Nafikiri sasa makusanyo ya TRA ya kutegemea adhabu Penalty) yatapungua kama sio kuisha kabisa.
Wafanyabiashara walio wengi wanadaiwa mamilioni sio kwa kutolipa kodi halali,bali kwa kutofaili nyaraka mbalimbali kwa muda mrefu. Jambo hili ndio linalowaliza Wafanyabiashara walio wengi hasa wa kati na wadogo.
Hii mimi naona ndio shida kubwa inayowakabili wafanyabiashara.
Madai ya kodi kama hizi yakifutwa (waived) biashara zitasisimuka upya.
 
Moja ya Legacy ya Magu ilikua kupora fedha za wafanyaniashara kinguvu. Sasa madhara hake ndio hayo hata kupata kodi stahiki itakua ngumu sana
 
Nyooo ili mkanikate kodi sizileti ng'ooo tena sahiv nimebuni mbinu mpya nimetengeneza fire break point kwenye sehemu nilipozihifadhi ili zisiungue
 
Mwigulu anasema watu waweke fedha bank hazitachukuliwa tena. Nani anamuamini Mwigulu? Ikumbukwe yeye ni mtuhumiwa pia kwenye utawala ule dhalimu. VP wa sasa ndio alikuwa waziri wa fedha wakati pesa zinaporwa, hapo unategemea nani awe na imani na serikali ya majizi?
 
Wizara zote Mama kapatia ila hapa tumepigwa
 
Kumbe ni kweli walinyan'ganya watu fedha zao!
Watawarudishia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…