Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, ameweka wazi mpango mpya wa Serikali unaolenga kutatua changamoto ya mitaji kwa vijana wanaohitimu masomo yao nchini. Akizungumzia hali ya upatikanaji wa mikopo, Nchemba amebainisha kuwa Serikali imeanza mchakato wa kuangalia uwezekano wa kijana kutumia cheti chake cha kuhitimu kama dhamana ya kukopa fedha za kuanzia maisha au biashara.
"Tumeanza kuwaza kwamba kijana aweze kutumia cheti chake alichohitimu kuweza kukopa baada ya kuhitimu, ili kuondoa kikwazo cha kukosa dhamana ambacho kimekuwa kikiwakwamisha wahitimu wengi,"
"Tumeanza kuwaza kwamba kijana aweze kutumia cheti chake alichohitimu kuweza kukopa baada ya kuhitimu, ili kuondoa kikwazo cha kukosa dhamana ambacho kimekuwa kikiwakwamisha wahitimu wengi,"