Mwigulu: Vijana watumie vyeti vya chuo kama dhamana ya mikopo baada ya kuhitimu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, ameweka wazi mpango mpya wa Serikali unaolenga kutatua changamoto ya mitaji kwa vijana wanaohitimu masomo yao nchini. Akizungumzia hali ya upatikanaji wa mikopo, Nchemba amebainisha kuwa Serikali imeanza mchakato wa kuangalia uwezekano wa kijana kutumia cheti chake cha kuhitimu kama dhamana ya kukopa fedha za kuanzia maisha au biashara.

"Tumeanza kuwaza kwamba kijana aweze kutumia cheti chake alichohitimu kuweza kukopa baada ya kuhitimu, ili kuondoa kikwazo cha kukosa dhamana ambacho kimekuwa kikiwakwamisha wahitimu wengi,"

Your browser is not able to display this video.
 
Mi sijui kama watatekeleza maana CCM wanapenda sana kutoa ahadi ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Ila kama wakitekeleza itakuwa vyema. Now the question is whether they'll do it or not
Ngoja tuone mda ni hakimu mzuri
 
Ninacho faham mimi ni kwamba dhamana hutumika kama fidia pale unaposhindwa kulipa mkopo. Sasa mtu kachukua milioni tano kawaachia licheti la ugavi mnalipileka wapi? Au vyeti ni biashara siku hizi alaf hamsemi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ