TANZIA Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala

TANZIA Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala

B I A S H A S H A R A (ogopa hii kitu) kwenye mabiashara kuna Dhuluma, kudhulumiwa, kuibiana kwa namna mbali mbali, moyo wangu unanituma tu kwenye kudhulumiana!, tunaweza kudhani mambo mbali mbali na pengine kuituhumu serekali lakini ikawa sivyo kabisa, baadhi ya wafanya biashara pia huwa ni majambazi wakubwa na biashara kuwa kama kivuli tu.
 
Attachments

  • images (13).jpeg
    images (13).jpeg
    10.9 KB · Views: 1
Ajali, R.i.p brother😭
 
Attachments

  • 2F08A2BB-22A6-40E4-AD97-2A9F4A631056.png
    2F08A2BB-22A6-40E4-AD97-2A9F4A631056.png
    560.8 KB · Views: 2
Hivi watanzania tumelogwa? Mpaka lini hawa polisi watafanya tofauti na utaratibu unaopaswa mpaka kufikia hatua ya wananchi kukata tamaa kiasi hiki na kuwaacha wafanye watakavyo huku wananchi wakiwa wameinamisha vichwa chini kama kondoo?
Tunahitaji mageuzi mapema sana kwa mustakabali wa vizazi vyetu hakika nawaambia....
Kule Zaire/Congo miaka ya Mobutu askari aliambiwa na boss wake, umepewa silaha unasemaje huna hela. Anakuja dukani anachukua bidhaa kama mali yake. Anaenda barabarani anasimamisha gari anakuamuru unatoa hela. Iko siku watafika huko.
 
Dah uchunguzi uanzie kwa walioupeleka mwili hapo hospitali, hii itatoa a lead ya walipoupata na mazingira gani then mambo yatajipambanua tu
Huo uchunguzi ataufanya nani ndugu yangu na kwa kutumia ushahidi gani?maana hata ukienda leo ukauliza hapo mwili ulikopatikana watoe wajihi wa aliyeupeleka na kuwakabidhi hawajui hata waanzie wapi.

Upo udhaifu Tanzania hii namna miili inavyokabidhiwa hospital,hawaulizi chochote kama ID zaidi ya jina ambalo mtu anaweza akabahatisha lolote akajiandika.
 
Kule Zaire/Congo miaka ya Mobutu askari aliambiwa na boss wake, umepewa silaha unasemaje huna hela. Anakuja dukani anachukua bidhaa kama mali yake. Anaenda barabarani anasimamisha gari anakuamuru unatoa hela. Iko siku watafika huko.
Pale idadi kubwa ya watanzania watakapofikia hatua ya kupiga mioyo konde na kusema "LIWALO NA LIWE"
Mbaya zaidi ni kwa wavaa uniform za kaki na wanasiasa....
 
Halafu ku a jitu litakuja na ma labi... majora yake lilopoke kifo ni nini tu? Nchi limekuwa la kipumbavu sana hiki!
 
Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi, aliyepotea tangu Desemba 11, 2024 amekutwa amekufa na mwili wake kukutwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
View attachment 3177965
Ulomi aliyekuwa akifanya biashara za fedha za mitandao ya simu maeneo yaa Sinza Kijiweni na Mwenge alipotea tangu 11 Desemba 2024.

Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro zinaendelea, baada ya simu zake kuita bila kupokelewa.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Desemba 16, 2024 baba mkwe wa Ulomi, Japhet Munisi amesema alipigiwa simu leo asubuhi na mke wa marehemu, akimjulisha kuwa amepata taarifa kuwa mwili wa mumewe uko hospitali.

Pia, Soma:

Mfanyabiashara Ulomi apotea, familia na Polis wanamtafuta
TRA: Hatuhusiki na kupotea kwa mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi
Polisi waanza kumtafuta Ulomi anayedaiwa kupotea
Eti alipata ajali 👇👇

View: https://x.com/millardayo/status/1868689113215328409?t=VZdpX4A-LBemYNm544VF2A&s=19
 
Kinachonishangaza mamlaka za serikali zinazohusika ikitokea mtu katekwa zinatoa majibu mepesi sana mpaka unashangaa hivi huyu amewezaje kupewa nafasi ya uongoz kama hii? Mkuu wa nchi naye Yuko kimya hata kulaani ?
Ukiacha na Mkuu wa Nchi, Kuna mtu anaitwa Mkuu wa kitengo cha usalama wa Taifa, He is so relaxed, Hakuna anae msumbua, ningetegemea mpaka sasa, angekua ameitwa kujieleza mbele ya bunge la Jamhuri ni kwann anazani bado anastahili kuwepo kwenye hyo nafasi
 
Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi, aliyepotea tangu Desemba 11, 2024 amekutwa amekufa na mwili wake kukutwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
View attachment 3177965
Ulomi aliyekuwa akifanya biashara za fedha za mitandao ya simu maeneo yaa Sinza Kijiweni na Mwenge alipotea tangu 11 Desemba 2024.

Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro zinaendelea, baada ya simu zake kuita bila kupokelewa.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Desemba 16, 2024 baba mkwe wa Ulomi, Japhet Munisi amesema alipigiwa simu leo asubuhi na mke wa marehemu, akimjulisha kuwa amepata taarifa kuwa mwili wa mumewe uko hospitali.

Pia, Soma:

Mfanyabiashara Ulomi apotea, familia na Polis wanamtafuta
TRA: Hatuhusiki na kupotea kwa mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi
Polisi waanza kumtafuta Ulomi anayedaiwa kupotea
Inawezekana akina Soka wameporwq uhai wao kama hivi🥶
 
Vifo vingine vinatokana na dhuruma kuiba wake za watu nk. Sidhani kama kufikiria serekali ya fisiemu inauwa hawa watu wote ni sahihi
let be reasonable guys. Serekali haiwezi kuuwa watu hovyo ikuuwe ww nani!!?? Yani serekali ije ikuuwe ww tigopesa kuweni na heshima kidogo basi
Sasa kama kuna raia wanajichukukia sheria mkononi,kazi ya serikali ni kuangalia tu,uhalifu ukitokea?
 
Dah uchunguzi uanzie kwa walioupeleka mwili hapo hospitali, hii itatoa a lead ya walipoupata na mazingira gani then mambo yatajipambanua tu
Kwamba hujui wanaopeleka ni squad ya kuteka na kuua kama walivyopeleka mwili wa Mzee Kibao?
Huwezi kuona ajabu kwamba wanasema mwili " umekutwa hospitali" Badala ya mwili umeletwa hospitali na watu xxx baada ya KUMKUTA sehemu xxx ? Mkuu haya mambo ni systematized na wanajua wanachokifanya! Kamanda alipowahi kusema tu uongo kwamba aliuza sijui gari aliyokodi Kwa ajili ya harusi, tra wakakana nk tayari red light ishawaka! Wamemtafuna
 
Katika Dunia ambayo watenda maovu ndio watunga Sheria usitegemee haki
Je tukate tamaa kama wananchi wa kawaida kwamba nothing can be done to change the situation and lead our country into a true and rightful way of governance and transparency?
 
Back
Top Bottom