TANZIA Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala

TANZIA Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala

Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi, aliyepotea tangu Desemba 11, 2024 amekutwa amekufa na mwili wake kukutwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
View attachment 3177965
Ulomi aliyekuwa akifanya biashara za fedha za mitandao ya simu maeneo yaa Sinza Kijiweni na Mwenge alipotea tangu 11 Desemba 2024.

Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro zinaendelea, baada ya simu zake kuita bila kupokelewa.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Desemba 16, 2024 baba mkwe wa Ulomi, Japhet Munisi amesema alipigiwa simu leo asubuhi na mke wa marehemu, akimjulisha kuwa amepata taarifa kuwa mwili wa mumewe uko hospitali.

Pia, Soma:

Mfanyabiashara Ulomi apotea, familia na Polis wanamtafuta
TRA: Hatuhusiki na kupotea kwa mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi
Polisi waanza kumtafuta Ulomi anayedaiwa kupotea

Huyu ni yule aliyenusurika kutekwa mtaani kwake hivi karibuni?
 
Huyu kaka hakuumwa lakini leo anakutwa amefariki.

Mnaotenda huu ukatili mtakosa amani ya moyo hata kama mnaishi kwenye mahekalu na kuendeshwa kwenye VX.

Hizi damu na masononeko lazima zitawawesesha kupita maelezo.
Ajali ya bodaboda ya kikatili sana
 
This is alerting! Maana yake raia tujilinde wenyewe hakuna mtu au mamlaka nyingine iliyo na wajibu wa kulinda usalama wa raia
 
Ajali ya bodaboda ya kikatili sana

Kama ilitokea ajali Ubungo External ,wasamaria wakampeleka hospital ya makuburi ,Je hospital ilipokea majeruhi bila PF3? Kama ilipokea bila PF3 ndiyo utaratibu huo? Kama walienda kuchukua PF3 mbona ndugu walivyokuwa wanamtafuta kwenye vituo vya polisi walisema hawajamuona? Kwanini polisi wasiseme kuna majeruhi wa boda tulipokea PF3 ebu nendeni hsopital flani mkamtambue?

Ajali ilitoke Ubungo ila simu yake mara ya mwisho ilizimwa Chang'ombe ,benefit of doubt(Labda vibaka walichukua baada ya "ajali").
 
1734377594918.png
 
Achunguze nani? Project ya wakubwa hii, ndio mana bibi kimya, waziri kimya, vyombo vya usalama hawasemi kitu.
 
Hivi watanzania tumelogwa? Mpaka lini hawa polisi watafanya tofauti na utaratibu unaopaswa mpaka kufikia hatua ya wananchi kukata tamaa kiasi hiki na kuwaacha wafanye watakavyo huku wananchi wakiwa wameinamisha vichwa chini kama kondoo?
Tunahitaji mageuzi mapema sana kwa mustakabali wa vizazi vyetu hakika nawaambia....
Polisi hawana ufuatiliaji kuhusu mtu aliekufa labda labda labda waliofiwa wawe na mawe na waajiri polisi wao private wachunguze ila sio wale wanaolipwa na Serakali
 
Back
Top Bottom