TANZIA Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala

TANZIA Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala

Mbona kwenye habari wamesema wazi kwamba aliagiza vifaa vya ujenz wa nyumba yao ndio akapigiwa simu vimefika lakini wakala wa clearing anamujitaj aende bandarini vikakaguliwe kwa msingi kwamba TRA wanataka awepo ili kuepusha kama kuna uharibifu au upotevu..

Ndio kwenda na piki pik na kupotea mazima... Kaubukia mortuary ya Mwananyamala RH
Hao hao mawakala wadakwe wahojiwe vizuri na wachunguzwe yani hakuna uhalifu usioacha alama , ukishakuwa tajiri bila kuwa na akili za kimafia unakufa mapema
 
Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi, aliyepotea tangu Desemba 11, 2024 amekutwa amekufa na mwili wake kukutwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
View attachment 3177965
Ulomi aliyekuwa akifanya biashara za fedha za mitandao ya simu maeneo yaa Sinza Kijiweni na Mwenge alipotea tangu 11 Desemba 2024.

Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro zinaendelea, baada ya simu zake kuita bila kupokelewa.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Desemba 16, 2024 baba mkwe wa Ulomi, Japhet Munisi amesema alipigiwa simu leo asubuhi na mke wa marehemu, akimjulisha kuwa amepata taarifa kuwa mwili wa mumewe uko hospitali.

Pia, Soma:

Mfanyabiashara Ulomi apotea, familia na Polis wanamtafuta
TRA: Hatuhusiki na kupotea kwa mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi
Polisi waanza kumtafuta Ulomi anayedaiwa kupotea
Aiseeee🙌🏿🙌🏿
 
#HABARI Mwili wa Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi, aliyepotea tangu Disemba 11 umekutwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar Es Salaam, Ulomi ambaye alikuwa anatambulika kwa kufanya biashara za fedha za mitandao ya simu maeneo ya Sinza Kijiweni na Mwenge alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha baada ya kuaga kuwa anakwenda maeneo ya Mbagala kukagua kontena lake baada ya kuitwa na watu waliodai walikuwa wanashughulikia kulitoa bandarini.

Baba mkwe wa Ulomi Japhet Munisi amesema alipigiwa simu leo asubuhi na mkwe wa Ulomi kuwa amepata taarifa mwili wa mumewe uko hospitalini na alipofika hospitali alikuta askari polisi wako hapo pia ambapo alipowauliza kuhusu kinachoendelea walimjibu kuwa wanafanya uchunguzi kwanza ndipo watatoa taarifa. #EastAfricaTV
 
Back
Top Bottom