TANZIA Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala

Hao hao mawakala wadakwe wahojiwe vizuri na wachunguzwe yani hakuna uhalifu usioacha alama , ukishakuwa tajiri bila kuwa na akili za kimafia unakufa mapema
 
Aiseeee🙌🏿🙌🏿
 
#HABARI Mwili wa Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi, aliyepotea tangu Disemba 11 umekutwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar Es Salaam, Ulomi ambaye alikuwa anatambulika kwa kufanya biashara za fedha za mitandao ya simu maeneo ya Sinza Kijiweni na Mwenge alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha baada ya kuaga kuwa anakwenda maeneo ya Mbagala kukagua kontena lake baada ya kuitwa na watu waliodai walikuwa wanashughulikia kulitoa bandarini.

Baba mkwe wa Ulomi Japhet Munisi amesema alipigiwa simu leo asubuhi na mkwe wa Ulomi kuwa amepata taarifa mwili wa mumewe uko hospitalini na alipofika hospitali alikuta askari polisi wako hapo pia ambapo alipowauliza kuhusu kinachoendelea walimjibu kuwa wanafanya uchunguzi kwanza ndipo watatoa taarifa. #EastAfricaTV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…