Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Wakati napitia mitandao mbalimbali ya kijamii leo, nimefanikiwa kumuona huyu mwanajeshi wa Tanzania anayelinda amani huko DRC akipekuliwa vikali huko Rwanda wakati akirejea nyumbani Tanzania:
View: https://x.com/MAbdallaziz/status/1896163224720150659/mediaViewer?currentTweet=1896163224720150659¤tTweetUser=MAbdallaziz
Kilichonishangaza sio upekuzi huu bali ni baadhi ya maoni ya wananchi waliokuwa wakichochea Tanzania iivamie Rwanda na kuigalagaza kisa mwanajeshi wake amepekuliwa kinyama wakati Rwanda ni mwanachama wa EAC. "Ina maana hatuaminiani?". Wamesikika baadhi ya wananchi wakihoji mtandaoni.
Kana kwamba hii haitoshi, wananchi wengine wameenda mbali zaidi kwa kuitaka Tanzania kufunga mipaka yake na Rwanda wakidai eti kwa kuwa Rwanda ni landlocked country, watadhoofika kiuchumi ili wawe na adabu.
MAONI YANGU
Watu wengine wanastahili kuhurumiwa kwa kuwa bado ni watoto wadogo hawajui nguvu na jeuri ya Rwanda kijeshi inatoka wapi. Wanachojua tu ni kutaka Tanzania ikurupuke kuivamia Rwanda kijeshi ili wanajeshi wetu waumizwe na washirika wa Rwanda. Hoja yao nyingine eti ni kwamba Rwanda ni ka nchi kadogo na kuwa kana watu wachache ukilinganisha na Tanzania; hivyo kanapigika vizuri tu! Hahaha! Watoto wengine wakishiba wanachekeshakesha sana! Ndugu zangu siku hizi kuwa na idadi kubwa ya wanajeshi sio kigezo cha kushinda vita aiseee! Ingekuwa hivyo, Russia ingeiteka Ukraine ndani ya siku 5 tu!
Acheni masikhara ndugu zangu. Kama mtu umefunga, endelea tu na swaumu zako bila shida. Sio mtu ukila futari lako ukashiba ndii unaanza kuwaza chokochoko usoziweza.
Ukiona mbuzi yupo juu ya mti, muache kama alivyo. Hujui nani kampandisha. Mchokoe pweza uone kilichomtoa kanga manyoya. Never ever taste the poison or measure the depth of a river using both feet! Shauri yako!
We nae huna akili,sasa nchi na nchi ziingie vitani kisa tu mwanajeshi kapekuliwa kisheria,