Mwisho wa Tanzania Pride: JWTZ wadhalilishwa kusubirishwa mpakani huko Rwanda

Maumivu ni makali mno pole sana chawa wa ccm haah
Hakuna kitu unajua kuhusu Tpdf zaidi ya uppuzi wa chuki. Fatilia michango yangu humu jamii forums humu sijawahi kuwa ccm Ila kuhusu jeshi la wananchi uniambii kitu wewe mtusi. Wapuuzi Kama wewe ndiyo wake watu wakija kukwambia muuwe mwenzio mnauwa. Hakuna jw wanatumia kofia nyeusi. Uwe na uelewa
 
Reactions: rr4
Mnawaita wanamgambo wa m23 na bado wanawahenyesha......mkiwaita wanajeshi wa m23 mtapungukiwa nini 😁😁😁
 
hiyo clip umeiona? hawa wanyarwanda ndio walikuwa wakimbizi hapa, tumewahifadhi, wengine wamesoma hapa. ni kwa nini wameamua kutukebehi hivi? kwa nini hawakufanya siri kutusitiri?
 
Haya wameyataka wenyewe.

Tumekuwa tukishauri Sana hapa mtandaoni kwamba Wanajeshi wa nchi yetu warudi nyumbani ili waje kuimarisha ulinzi kwenye mipaka ya nchi yetu hii, lakini inavyoonekana Watawala wa nchi hawataki kusikia ushauri wetu huo. Matokeo yake ndio haya sasa.

Maandiko Matakatifu yanasema kwamba "Aonywaye Mara nyingi naye hushupaza shingo, huvunjika ghafla na hakuna dawa tena."
(Mithali 29: 1)

Kama ni suala la Kulinda Amani, basi Jeshi linapaswa kupeleka Wanajeshi wake katika nchi za mbali, lakini siyo kwenda kulinda amani katika nchi ambazo ni majirani zetu. Hii ni hatari kubwa sana kwa Usalama wa nchi. Wanajeshi Wapiganaji wa Vikosi vya Kulinda amani vinapaswa kupelekwa katika nchi za mbali huko Kama vile kwa mfano Pakistan, Lebanon, Mynmar, Haiti, n.k.

All in all, Wanajeshi wetu wanapaswa kupelekwa kwenda kulinda amani katika nchi zingine lakini muda wote kabisa wanapaswa wasimame katika Upande wa HAKI. Wasiende huko ili kwenda kuwatetea au kuungana na Watawala wa huko ambao ni Wadhalimu. Ujumbe wa Kulinda Amani usititumwe ili kwenda kusaidia au kuungana na upande wa Wadhalimu.

Daima Tukumbuke kwamba 'ukiungana na Wadhalimu basi Wapenda HAKI hawatakuwa upande wako.'
 

They have accepted the Catastrophic Defeat!
 
Hii kitu naiona Mimi peke yangu au wengine mnaona?

Kwanza nasema hakuna jeshi Bora na lenye nguvu East and central Africa Kama jeshi la wananchi wa Tanzania kwa sababu ambazo siwezi kuzitaje hapa!!

We have very strong military lakini tunakosa meno ya amiri jeshi mkuu!!

Rais wangu urais ni zaidi ya kufanya mikutano ya hadhara tu!

Rais wangu unatambua chochoko za mwaka 2013 za Hawa wajinga zilivyozimwa?

Je mgogoro wa Malawi unajuwa ulivyozimwa?

Mtwara unajua mgogoro ulivyozimwa?

Panya Road unajua walivyozimwa mpaka sasa dar watu wanafanyakazi masaa 24?

Umesikia lini Tena mtu akifa mtwara, Au kuuuwawa na Panya road ?

Hii ndio maana halisi ya JWTZ hawafanyi kazi kwa porojo za kisiasa wanafanya kazi kwa mjibu wa report za kiusalama!

Rais wangu Samia fanyia kazi report ya usalama wa mipaka na Hatari ya m23 kuenea mashariki ya Kongo ambayo ipo mezani kwako!

Vijana tunahitaji go ahead tu kwenda kutengeneza historia!! Haiwezekani ndugu zetu kupokwa nchi next tutakuwa sisi na JWTZ haiwezi kukubali

Achana na kupoteza pesa kwenye uchaguzi uchwara wape pesa watu wakalipiganie Taifa efectively.

JWTZ isiguswe wala kuchezewa na yeyote ndio taasisi imara ambayo imebaki Tanzania.

Sioni jeshi la kupambana na JWTZ east and central Africa

Wape vija siraha wape vijana pesa wakalete pesa zaidi na usalama wa Kongo ndio usalama wa Tanzania.
 
Uwongo mkubwa sana huu
 
Sijui kwanini wanafikiri kwamba vita ya nchi na nchi nikama mazoezi ya mpira wa simba na Yanga.
 
Hebu tuanze na ile bandari yetu pendwa na DP World.

Mwaka wa tatu huu sasa, mapato yamepanda kwa kiwango gani ???
 
Pole maumivu ni makali haah
 
Mosi, nmeishia kusoma pale umeandika..Rwanda ikitaka kufika Dar es salaam..nimegundua kichwani hauko sawa, utakuwa unaumwa bila kujua ni mgonjwa..a lot of rubbish umeandika!
Hakuna haja kuendeleza conversation na wewe..sikiliza, km unadhani hiyo nguvu ipo stage something real with Rwanda utapata majibu, nadhani hayo ya CDF kusema nchi ina hadi viongozi ambao si raia wa Tanzania kwako ni porojo sababu akili yako ni ya panzi..haina uwezo ku-troubleshoot short n long consequences za hali km hii kwa nchi! Umeshinda chukua kombe!
 
Walienda mshahara na M23 sio kukinda amani , rudia kwa video vizuli siku waliofika
SEMA SIJAKUELEWA UNACHOMAANISHA, NAONA UMEANDIKA KISWAHILI CHENYE KINYWARWANDA NDANI YAKE, HEBU SAHIHISHA ANDIKA KISWAHILI CHA KITANZANIA NIKUELEWE, SAMAHANI.
 
Sioni cha kushangaza hapo.
1.Jeshi liko chini ya sheria za UN
2. Propaganda za kivita ziliendelea kysema Ukraine inashinda kwa kishindo mwisho umekuwa aibu na Trump ameweka msumali wa moto kwenye kidonda
3. Mission ingekuwa ya aibu kama DRC wangeomba JWTZ iende kama nchi kama Sychelles
 
Mkuu Lord, hii ni mission ya UN ina maana logistics hazikufanyika mapema ili majeruhi wapate fast track service pale mpakani? Au ndio ujeuri wa Fidodido?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…