Wananchi wenye hasira wanasikia mawaidha?! .
Hata hivyo kuna kisa kilitokea Tanga mjini kati ya mwaka 2013/14 hivi kijana mmoja alimpora mdada simu, alivyopiga kelele jamaa wakamkimbiza mwizi wakamkamata, wakampiga , wakamwagia petroli, ile wanatafuta kiberiti Kuna sheikh alikuwa anapita akawaambia " Mswalieni Mtume!, Watu wakaitikia : Allaahumma swalli wa Sallim aleyhi." Baada ya hapo hasira zilitulia na sheikh akawashauri yule mwizi wampeleke polisi, jamaa wakakubali na yule kijana mwizi akawa amepona baada ya kuwa Alisha mwagiwa petroli. Sasa kwa kuwa mji wa Tanga wakazi wake wengi ni waislamu na ambao wamelelewa malezi ya kuheshimu masheikh na maustadhi unaweza kuwapa mawaidha wakakuelewa. LAKINI KWA WANANCHI WA KARIAKOO HATA POLISI AKIJIPENDEKEZA WANAWEZA KUMPIGA PIA!.